"MEMBE ni mwekezaji mwambao mwa ziwa Nyasa"

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Inadaiwa kuwa mbali na kutetea maslahi ya Taifa kama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Membe ana maslahi binafsi kule mwambao mwa ziwa Nyasa. Inadaiwa Mhe. Membe ameoa katika kijiji cha karibu na mji wa Mbambabay na pia anamiliki hoteli ya Kitalii ambayo ni miongni mwa hoteli zenye hadhi katika mji mdogo wa Mbambabay ambao upo Wi;laya mpya ya Nyasa ukiondoa hoteli nyingine na Mhe. John Komba na ile ya Shirika la Masista wa St. Agnes African Sisters la watawa la Chipole _ Songea (St. Benadeta Hotel).

mbambabayhotel.jpg

St. BERNADETA HOTEL

30921695.jpg

30920118.jpg

mbambabaymap.jpg
 
Suala la yeye kuoa huko ni mattaer ya public knowledge na hakuna kitu cha ajabu katika hilo. Suala la kumiliki hotel ni ule ule uongo wa kila siku ambao tumeuzoea siku zote. Lakini assuming anamili hotel (which is denied), hiyo ina uhusiano gani na legitimate claim ya nchi yetu kwa uchokozi wa Malawi? After all, malalamiko ya Tanzania yanahusiana na ziwa na siyo sehemu ya nchi kavu ambako ndiko mnakozua amejenga hotel.

Yote kwa yote, hiyo ingekuwa ni sababu ya yeye kulazimisha kutangaza vita ili kuya-secure maeneo hayo lakini kwa vile ni muumini wa diplomasia kwa vitendo na maneno, anajua kwamba madai yetu ya kwamba nusu ya ziwa nyasa ni mali yetu, yatafanikiwa kwa kukaa mezani, siyo kujipiga kifua kwa wapenda sifa wengine na kujisogeza kwa majeshi yetu na kutangaza vita kwa madaraka ambayo hajawahi kuwa nayo na hatakuwa nayo kamwe!
 
napata shida sana kwa vijana kupapukia siasa bila kujua kuchambua, JF kuna kanuni za kukubali na kukataa kama unataka kuwa mwanachama.Napata shida kuona vijana kukurupuka kutoa thread ambazo hazina mashiko kwa masitakabali wa nchi yetu.Ardhi ya tanzania kutambuliwa na kimataifa na majirani zetu ina uhusiano gani na kuoa na pia kuoa mbambabay?legitimate ya taifa ndo hoja na si uwekezaji, je kama angewekeza kwenye ardhi ya kenya angedai iwe ardhi ya tanzania, sababbu kajenga hotel?Vyema wachangiana waleta thread mlete mkiwa na ushahidi wa chanzo na legitimacy ya nchi membe han uwezo wa kuinfkuence ati ni waziri!we mleta thread hii acha umeya utasutwa mchana kweupe , hapa si facebook, kwenye umbeya wa mapenzi.leteni mamabo ya msingi ya kujenga nchi yetu na usitawi wa watanzania.
 
....Kweli Ficha Upumbavu Wako, either Umepotoshwa na kuingia kichwakichwa au ni Hujui tu na bahati mbaya Haujui kuwa Haujui...

...Unazungumzia hoteli ya Membe Mbambabay alafu unaweka picha ya Hoteli ya Masista wa Kanisa Katolic?kwa kimji kidogo kama Mbambabay kama uliweza kupiga picha Hoteli hiyo na kupiga beach ulishindwa vipi kuipiga picha hiyo hoteli ya Membe ya Kufikirika?hii ni thread ya kijinga zaidi kupata kuiona JF...
 
napata shida sana kwa vijana kupapukia siasa bila kujua kuchambua, JF kuna kanuni za kukubali na kukataa kama unataka kuwa mwanachama.Napata shida kuona vijana kukurupuka kutoa thread ambazo hazina mashiko kwa masitakabali wa nchi yetu.Ardhi ya tanzania kutambuliwa na kimataifa na majirani zetu ina uhusiano gani na kuoa na pia kuoa mbambabay?legitimate ya taifa ndo hoja na si uwekezaji, je kama angewekeza kwenye ardhi ya kenya angedai iwe ardhi ya tanzania, sababbu kajenga hotel?Vyema wachangiana waleta thread mlete mkiwa na ushahidi wa chanzo na legitimacy ya nchi membe han uwezo wa kuinfkuence ati ni waziri!we mleta thread hii acha umeya utasutwa mchana kweupe , hapa si facebook, kwenye umbeya wa mapenzi.leteni mamabo ya msingi ya kujenga nchi yetu na usitawi wa watanzania.

...Upo sahihi kabisa, lakini kwa ufafanuzi tu ni kuwa Membe Hana Hoteli yoyote Mbambabay, bali ana nyumba ya kawaida sana ya makazi ukizingatia kuwa ni nyumbani kwa mke wake, nyumba ambayo ata kijana yoyote aliyefanya kazi au kujishughulisha kwa zaidi ya miaka 3 anaweza kuijenga....

...Naamini mwanzilishi wa thread kama kweli alifika Mbambabay atakuwa analijua hilo ila amedhamiria kupotosha kwa makusudi, huu ni upumbavu..
 
Huyu jamaa kaandika asichokijua Mheshimiwa Benard Membe ni kweli ameoa katika Kijiji cha Ndengele na amemuoa Mama Dorcus Masanche,ni uongo ulio dhahiri Mheshimiwa hana Hoteli Mbamba Bay bali ana nyumba tena ya kawaida tu nyumba ambayo yeye huwa anafikia na familia yake anapokwenda kupumzika na kuwatembelea wanafamilia ya mkewe,na kwa sasa baada ya kuanzishwa Wilay mpya ya Nyasa nyumba yake hiyo ndiyo inayotumika kwa makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ndugu Ernest Kahindi.Kuna Hoteli mbili zenye ubora moja ni ya Masista wa Kiromani toka Chipole ambayo ndiyo yeye mtoa uzi kaipiga picha hiyo ilifunguliwa na Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete na nyingine inamilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Mheshimiwa John Komba.
 
Suala la yeye kuoa huko ni mattaer ya public knowledge na hakuna kitu cha ajabu katika hilo. Suala la kumiliki hotel ni ule ule uongo wa kila siku ambao tumeuzoea siku zote. Lakini assuming anamili hotel (which is denied), hiyo ina uhusiano gani na legitimate claim ya nchi yetu kwa uchokozi wa Malawi? After all, malalamiko ya Tanzania yanahusiana na ziwa na siyo sehemu ya nchi kavu ambako ndiko mnakozua amejenga hotel.

Yote kwa yote, hiyo ingekuwa ni sababu ya yeye kulazimisha kutangaza vita ili kuya-secure maeneo hayo lakini kwa vile ni muumini wa diplomasia kwa vitendo na maneno, anajua kwamba madai yetu ya kwamba nusu ya ziwa nyasa ni mali yetu, yatafanikiwa kwa kukaa mezani, siyo kujipiga kifua kwa wapenda sifa wengine na kujisogeza kwa majeshi yetu na kutangaza vita kwa madaraka ambayo hajawahi kuwa nayo na hatakuwa nayo kamwe!

Mbopo/Membe unajitahidi sana kujisafisha lakini in the heart of hearts unajua kuwa wewe ni mchafu toka enzi zile unafanya ufisadi na yule rafiki yako wa kutoka Ethiopia!!
 
hapana mbaya kuoa kwani hayo ni maisha binafci kule umemuona membe tu mbona wapo wazee.watoto na vijana wenzetu wengi wanaopga shughuli zao kule hujui kwamba jamaa wakingangania na wakaachiwa kihivyo cc hatutakula magege na vitui.
 
Unajuwa vitu vingine haviitaji hata nguvu ni utashi na uelewa wa kawaida tu, Sidhani kam JF ilianzishwa kwa dhumuni la kuongelea/kumuongelea mtu au jamii fulani kwa sifa mbaya au nzuri bila kuwa na usibitisho kamili wa kitafiti, mi niliona huyo mtu aliyo zungumzia hilo swala la MEMBE amelileta kibinafsi zaidi, ingekuwa busara kama allikuwa hana uwakiaka wa jambo husika ni bora angelileta JF kwa muonekano wa kuliza cyo kitarifa ili lijadiliwe kwa maoni/mawazo tofauti kwa wana JF. Namini hiyo ndiyo ilikuwa dhamira kuu/sahihi ya JF kuanzishwa. KWA HIYO TUWE NA UWAKIAKA NA MASWALA TUNAYO JADILI.....
NI MTAZAMO TU!!
 
bado napitia michang ya vijana nikiwa tayari, nitachangia.
hata hivyo ni vizuri kuwa makini na mada inayoanzishwa. kiini cha mgogoro ni malwi kuweka kampuni ya kutafiti mafuta jirani na mpaka wa malawi na tanzania kwenye ziwa nyasa. tayari malawi imekubali kusitisha utafiti wa mafuta kwenye eneo hilo.
 
Huyu jamaa kaandika asichokijua Mheshimiwa Benard Membe ni kweli ameoa katika Kijiji cha Ndengele na amemuoa Mama Dorcus Masanche,ni uongo ulio dhahiri Mheshimiwa hana Hoteli Mbamba Bay bali ana nyumba tena ya kawaida tu nyumba ambayo yeye huwa anafikia na familia yake anapokwenda kupumzika na kuwatembelea wanafamilia ya mkewe,na kwa sasa baada ya kuanzishwa Wilay mpya ya Nyasa nyumba yake hiyo ndiyo inayotumika kwa makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ndugu Ernest Kahindi.Kuna Hoteli mbili zenye ubora moja ni ya Masista wa Kiromani toka Chipole ambayo ndiyo yeye mtoa uzi kaipiga picha hiyo ilifunguliwa na Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete na nyingine inamilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi Mheshimiwa John Komba.

Haa...TISS!!

Tulitaka haya..kumbe kapanga Mkuu wa Wilaya???
 
Back
Top Bottom