Membe: Gaddafi amefikia mwisho lakini hatuwatambui waasi!

Tunisia na Misri hawakukamata SILAHA ... ni tofauti kabisa na kinachotokea LIBYA
Mapinduzi ni mapinduzi haijalishi umetumia mkuki au sauti ya ukali kuiondoa serikali madarakani bila utaratibu.

• Thanks
Reactions: EMT
Membe amesema Tanzania inajua kwamba hatima ya Kanali Muammar Gaddafi kuongoza Libya imekwishafikia, lakini haiwezi kuwatambua waasi wakati bado hawajaunda serikali. “Serikali ni pamoja na kuwa na viongozi walioapishwa, tutawatambua kama watakuwa na mihimili mitatu ya serikali, bunge na mahakama,” alisema Membe.

Hadi sasa nchi za Afrika ziizoitambua serikali ya waasi wa Libya ni pamoja na Kenya, Botswana, Ethiopia, Djibut, Rwanda na Tunisia. Nyingine ni Senegal, Gabon, Gambia, Bokina Faso, Benin na Nigeria. Zingine ni Morocco, Chad, Ivory Coast, na Ghana.

Source: Mwananchi

Nilitegemea jibu la Tanzania kutowatambua NTC Libya. Tanzania katika uchaguzi wa mwisho uliokwisha kulikuwepo na malalamiko kibao, kumbuka hata ripoti ya EU walisema chama tawala kilitumia rasilimali za serikali katika kampeni zake. kama unakumbuka hata jeshi lilijiingiza katika siasa na kutoa vitisho...Katiba yenyewe kuandikwa upya ili kukidhi mazingira ya vyama vingi mpaka rais asusiwe. Tanzania kama nchi zingine ambazo hazijakuwa na demokrasia iliyo wazi hawawezi kusema wanawatambua Baraza la Mpito la Waasi kwani kusema hivyo ni kama unajihukumu mwenyewe....maana yake iko indirect kwamba kukubali kirahisi hivyo ni kama kuhamasisha watu waliokandamizwa na nchi zao hata wao wanaweza kuanzisha mabaraza yao ya mpito na yakatambuliwa. Wenye konfidensi ya hivyo ni wale wako madarakani kwa kushinda kwa wazi na pia wako tayari kuachia ngazi wakishindwa katika uchaguzi.

Sovereignty iko kwa nani?
Mkuu wangu ni vigumu sana kusema kwa sababu Mapinduzi haya yamefanyika Kijeshi na wanaoongoza vikosi hivi ni wataalam kutoka nchi za Magharibi (NATO). Hakuna chama wala mtu ambaye anajulikana kama ndiye kiongozi wa kundi ama vikundi vyenye supreme authority within that territory. Na kama ukikosa hilo sii rahisi ukasema Sovereignty iko kwa nani kwa sababu hata Iraq au Afghanstan unaweza kusema utawala wao pamoja na kwamba wanalindwa na NATO..Sii Libya, but time will tell - tuwe na subra yasije kuwa ya Misri maanake hadi leo nchi bado ipo mikononi mwa wanaJeshi..

Nilitegemea jibu la Tanzania kutowatambua NTC Libya. Tanzania katika uchaguzi wa mwisho uliokwisha kulikuwepo na malalamiko kibao, kumbuka hata ripoti ya EU walisema chama tawala kilitumia rasilimali za serikali katika kampeni zake. kama unakumbuka hata jeshi lilijiingiza katika siasa na kutoa vitisho...Katiba yenyewe kuandikwa upya ili kukidhi mazingira ya vyama vingi mpaka rais asusiwe. Tanzania kama nchi zingine ambazo hazijakuwa na demokrasia iliyo wazi hawawezi kusema wanawatambua Baraza la Mpito la Waasi kwani kusema hivyo ni kama unajihukumu mwenyewe....maana yake iko indirect kwamba kukubali kirahisi hivyo ni kama kuhamasisha watu waliokandamizwa na nchi zao hata wao wanaweza kuanzisha mabaraza yao ya mpito na yakatambuliwa. Wenye konfidensi ya hivyo ni wale wako madarakani kwa kushinda kwa wazi na pia wako tayari kuachia ngazi wakishindwa katika uchaguzi.

This could certainly be part of it.

Lakini vile vile, huwezi kutambua watu ambao hawajaji-organize bado. Hawana serikali, positions zao hazijulikani etc.

Waasi wenyewe kitu pekee kilichowaunganisha ni kumtoa Gaddafi, now that Gaddafi is going, hata hatujui kama wataweza kubaki kitu kimoja.

Membe amesema Tanzania inajua kwamba hatima ya Kanali Muammar Gaddafi kuongoza Libya imekwishafikia, lakini haiwezi kuwatambua waasi wakati bado hawajaunda serikali. “Serikali ni pamoja na kuwa na viongozi walioapishwa, tutawatambua kama watakuwa na mihimili mitatu ya serikali, bunge na mahakama,” alisema Membe.

Hadi sasa nchi za Afrika ziizoitambua serikali ya waasi wa Libya ni pamoja na Kenya, Botswana, Ethiopia, Djibut, Rwanda na Tunisia. Nyingine ni Senegal, Gabon, Gambia, Bokina Faso, Benin na Nigeria. Zingine ni Morocco, Chad, Ivory Coast, na Ghana.

Source: Mwananchi

Aaaah mie mpaka kichwa kinauma

Ningeshauri wachangiaji wasome protokali za geneva, badala yakujikita kwenye ushabiki, ingekuwa vema mleta hoja au waunga hoja wamekuja na vipengele vya kimataifa ambavyo mhe waziri amevivunja kwa taarifa yake hili tuelimishane na tupunguze kupotoshana mchana kutwa na sijui FRELIMO mbona tuliwatambua n.k, nikama kung'ang'ania kumpeleka mwanao shuleni miguu peku kisa hata wewe ulisoma ukiwapeku( isitoshe ndio maana unafikra peku)

Mbona umoja wa mataifa kwenyewe aliyekua balozi wa libya ktk UN ndio alikua mmoja wa watu wa kwanza kabisa kudefect na kuwatambua NTC, na bado UN imeendelea kumtambua balozi huyo kama mwakilishi wa Libya, unataka kusema UN hawaufahamu uwapo wa hiyo Geneva convention? Halafu si Migiro wa UN ni mTanzania? Mbona hatujamuita ajiuzuru kuonesha kuprotest uamuzi wa UN kuivamia libya na kumtambua balozi wa libya aliyehamia NTC?

sera yetu ya mambo ya nje inasema wazi kuwa haifungamani na siasa za upande wowote, nadhani hawajaitafsiri inavyopasa, ni kama tunafungamana na gadafi hivi.

sera yetu ya mambo ya nje inasema wazi kuwa haifungamani na siasa za upande wowote, nadhani hawajaitafsiri inavyopasa, ni kama tunafungamana na gadafi hivi.

kaka mwezeshaji ndio hivyo kauwawa wamemkimbiza unafikiri wataachakulalamika..

na mpaka sasa bahari beach haijapata mtu kwa hiyo kuweni chonjo kwa hilo..

Fikra mgando. Maamuzi ya kutotambua waasi yasingeweza kuchukuliwa kabla ya utawala wa Gaddafi kuanguka na hili limetokea siku chache tu zilizopita. Pili, uamuazi huu umezingatia pia kikao cha baraza la usalama la AU ambalo Tanzania nayo ilishiriki. Tatu, suala la waasi kuamua kubadilisha alama za nchi yao bila kufuata utaratibu na kama Vienna Convention inavyosema nalo si la kuliangalia kwa jicho jepesi. Hivi kuna ayaejua ni nani anaongoza Libya sasa hivi? Utatambuaje kikundi cha waasi ambao bado hawajashika hatamu za utawala zaidi tu ya kuteka miji na majengo?

Pole wee ukimaliza kuota amka uukute ukweli kuwa Gadaffi hayupo na keshakua historia sasa, wenye nchi ni NTC chini ya uongozi wa Jalil.

Gadafi yuko madarakani kwa miaka 42.
CCM iko madarakani kwa miaka 50.
Wametoka mbali hawa.

Kama kuna mtu slow hapa basi ni wewe, katika foreign policy -ambayo hatuna- kuna overt na covert mission.

Tanzania hatuna hata comprehensive Foreign policy, achilia mbali covert mission zaidi ya kupeleka wanajeshi wastaafu walevi balozini.

Kusema kwamba waacheni waasi waonyeshe wanasimamia wapi hakumaanishi tu forego covert mission, labda kama uko slow ndiyo unaweza ku interpret hivyo.

Moreover, kabla ya kutaka kujipasua msamba kugombea biashara kwenye vita za watu, ingefaa kwanza uwe na cha kufanyia biashara.Tanzania is mostly an importer, kuanzia biskuti, pini mpaka mitambo ya umeme.Hizo export chache tulizonazo mostly ni agri products na minerals ambazo hatuna economic justification ya kuingia katika a diplomatic brouhaha kwa ajili yazo. Angalia usiuze ng'ombe kwa sababu ya kushinda kesi ya kuku.Angalia jitihada za kufanya biashara ya vitu ambavyo huna isikuingize gharama ya mahusiano ambayo ni kubwa zaidi na inaweza kukuharibia biashara kesho ambapo unaweza kupata uwezo wa kufanya biashara.

Tunajua viongozi wetu wanachemka sana, na Membe mchemfu, na the romantic story hapa ni ku buy into the west's oversimplification ya "the tyrant Gaddafi vs freedom fighters". Lakini tuepuke foreign policy ya copy paste.

The west, and not only governments, even individuals, collective has a habit of aligning -really masking- it's own personal ambitions with some lofty altruistic public positions. If our interests do not match theirs, and there is no reason to jump on the bandwagon, let us not.

Wewe ndio slow kabisaaaa. Tusubiri nini sasa? Mlikua mnakula faranga za gadaffi sasa mwanaona aibu kuwatambua NTC hahahaha

Nafikiri aliyoyasema Membe si msimamo wa watanzania bali ni msimamo wake yeye na kundi lake linalomwonea huruma Gadafi kwa sababu wanazozijua wenyewe

Wakati wanaKula faranga za gaddafi waliona rahaaaa sasa wanapatwa kigugumizi kuwatambua NTC.

elaborate

ni swali tu sijui kama nahitaji kufafanua zaidi. Kwa sababu watu hapa wanavyozungumza ni kana kwamba sovereignty iko kwa Rais au institutions. So tuanzie hapa ili tuone kwanini tumefanya makosa toka mwanzo ya kutotambua wananchi wa Libya walioamua kuiondoa serikali yao. Hakuna tofauti kati ya Tunisia, Misri, Libya na hata Syria. Viongozi wetu - kina Membe na wengine- wanataka tuamini kuwa uhalali wa serikali unatokana na viongozi wake! ndio maana wanatuuliza "viongozi wa waasi ni kina nani" ati "Rais wao ni nani"? Well.. ukishakosea kwenye msingi utakosea kwenye hitimisho. Ndio maana nimeuliza hilo ili kuwarudisha watu kwenye msingi kwanza.

Ccm wasiwasi unawasumbuwa, na ndicho kinachowafanya washindwe mambo ya siasa za nje, hiyo sio sababu walio wengi wameshasema

awaridhiki na utawala wa kimabavu aliokuwa akiufanya Ghaddafi kwa muda wa miaka arobaini na mbili aliyokuwa madarakani kutawala nchi yeye pamoja na watoto wake na kuelekea kulithishana utawala. Matumizi mabaya ya fedha, mauaji yasiyokuwa na kikomo na ukandamizi wa demokrasia

Akumbuke wakati anampindua mfalme wa Libya mwaka 1969 kwa ahadi ya kuleta mazuri kwa Walibya lakini aligeuka na kuwa yeye mfalme zaidi

ya wafalme wote duniani, hapo ccm fadhila ndio inawasumbuwa na madeni na uwekezaji wa kiufisadi aliowekeza nchini. ccm wapo katika kusikilia

wakisikia ameuwawa au kukamatwa ndio maamuzi yao yatatoka,

Kweli tupu

Back
Top Bottom