Membe: Gaddafi amefikia mwisho lakini hatuwatambui waasi!

Membe amesema Tanzania inajua kwamba hatima ya Kanali Muammar Gaddafi kuongoza Libya imekwishafikia, lakini haiwezi kuwatambua waasi wakati bado hawajaunda serikali. “Serikali ni pamoja na kuwa na viongozi walioapishwa, tutawatambua kama watakuwa na mihimili mitatu ya serikali, bunge na mahakama,” alisema Membe.

Hadi sasa nchi za Afrika ziizoitambua serikali ya waasi wa Libya ni pamoja na Kenya, Botswana, Ethiopia, Djibut, Rwanda na Tunisia. Nyingine ni Senegal, Gabon, Gambia, Bokina Faso, Benin na Nigeria. Zingine ni Morocco, Chad, Ivory Coast, na Ghana.

Source: Mwananchi

Hapo pekundu.......Gadaffi alikuwa navyo hivyo vitu? Mbona mlimtambua

BTW: Membe=Nyoka wa mdimu....said Mudhihir
 
Maskini Tanzania, yaani sisi leo tunafuata? Hawa wangekuwa wakati wa harakati za ukombozi PLO, POLISARIO, ANC, FRELIMO n.k wasingepata nafasi Tanzania. je wanaitambua serikali ya Misri au ya Tunisia? Na hiki kipimo cha "Kuapishwa kwanza" kimeanza lini. Si waseme tu kuwa urafiki ulikuwa na Gaddafi lakini siyo wananchi wa Libya? Hii ni aibu kwa Tanzania.

Hivi unajua hata hao walibya majority hawajui kinachoendele? Masikini wewe usiejua kuwa vita ile ni ya NATO kumng'oa Gadaffi na sio ya wananchi wa Libya na ndio maana waasi ambao wamewekwa kwa ajili ya maslahi ya wenye NATO walikuwa wanasaidiwa kudhoofisha miundombinu ya mawasiliano ya jeshi la Gadaffi na huku wakinufaika na silaha na mafunzo yake yaliyotolewa na makomandoo wa NATO. Anyway najua hujui futilia utajua ushiriki wa nato na ujiulize kwa manufaa ya nani?Kwanini Libya?kuna nini hasa? mbona Zimbabwe hawaendi kuwaokoa kwa kutawaliwa na diktekta kwa miongo mingi na nchi kuingia kwenye njaa isiyoisha? Jiulize matatizo ya Somalia NATO haiyawezi? wao wanahuruma na binaadamu si wangesaidia Somalia ikatawalika kama wanavyotaka Libya itawalike? Lazima ujiulize maswali kama mia hivi ili ujue maslahi ya nchi za umoja wa kujihami na usiwaingize hesabuni Walibya (waliopangwa kumtumikia kafiri wapate mradi wao)
 
Hii inawezekana ni baada ya serikali ya waasi kutangaza dau la $2,000,000 kwa yeyote atakayemuua Gadaffi au kuwezeshwa kukamatwa. Inatupapicha yawezekana Dictator Gadaffi amehifadhiwa na serikali ya utawala legelege.
 
Ghadafi Kama Nyerere alijua sana kujenga nje kuliko ndani, viongozi wengi wa Africa Nyerere aliwafanyia mema ndio maana wanataka hata kumfanya mtakatifu, Membe hawezi kumsaliti Ghadafi ni sawa na kumsaliti nyerere
u can't compare the two,.the former is the moneymonger and dictator,the latter was a true pan africanist,..oil and water don't get along buddy!!
 
Nilimuona Membe akiongea ITV. Nina wasiwasi huyu waziri kama anajua diplomacy. Kuna njia nyingine angeweza kuongea kuhusu suala la Libya bila kuweka bayana msimamo wa Tanzania kwa sasa, na zaidi hisia zake binafsi.
 
Membe na jk bwana,
ngoja tuone na ngonjera zao hizi kama hawaja salimu amri
uwezo wa kupishana na usa, uk , france, rusia na china tumeutoa wapi?
 
Hivi ilani ya CCM kuhusu sera ya mambo ya nje inasemaje? Maana yawezekana wanatanguliza siasa na uswahiba badala ya uchumi,biashara na tekinolojia!
 
Suala sio uswahiba wote mnajua Ghadaff amepigwa na NATO na wala hakuna watu wa Libya pale wale wengine wote vibaraka hata hapa Tz wapo wamejaa sasa watu ooh Membe membe sasa mnataka aseme nini?!! yani nyie msione kichaka tayari uharo pwaaaa...kisa wazungu na misaada njaa yao!!! wale hawana rafiki wa kudumu na hizi tabia za kuombaomba zinasababisha watu hawaelewi ama wanajifanya hawaelewi its a shame!!!

Kwani kama NATO inapenda Afrika why wasizuie AL shabab?!! ama Boko Haram?!! nyie vipi bana!!! hawa wazungu washenzi tu tena sana....wanakwenda kwa maslahi and nothn else...Tunisia wala Egypt hakukua na Rebels hawa walianza na risasi, mlitaka Ghadaff awambie nini sasa kama wana risasi?!! mbona hapa Tz maandamano ya Arusha risasi zilitumika?!! uliwaona hao NATO?!! KULE Syria na Palestina mnawaona?!!

acheni colonial mind bana...am not supporting Ghadaff kuua ila siungi mkono ushenzi wa Wazungu kuja kuvamia nchi ya Afrika kwa kisingizio cha kulinda Raia na wakati huo huo wameua maelfu..watch out
 
Tatizo ndio linakuja hapo... Membe katoa hio kauli akisahau kua the so called waasi mpaka wa watengamae na waunde hio Serkali inayoeleweka inachukua kiji mda - Huku ikiwa wazi kua Gaddaffi sasa kashindwa na hana kabisa upenyo wa kuchomokea ili arudi katika Himaya yake (maeneo yake of interest) let alone uongozi... Hivo basi huyo huyo Membe (kama sio wawakilishi) watajikuta in the near future akianza mawasiliano na hao hao Waasi (ambao inevitably ndio watashika nchi moja kwa moja) katika maswala mengine nyeti - which surprisingly to a person ambae mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ni area yake of work inabidi awe aware.... Inasikitisha kua sometimes viongozi wetu hawajui when to just shut up!
Subiri naye Kikwete atatoa Tamko mda si mrefu, Ashadii mbona unakuwa kama hujui nchi inaendeshwaje kwasasa? Usije ukashangaa keshokutwa utaambiwa yale yalikuwa ni maoni tuu ya Membe
 
Ningeshauri wachangiaji wasome protokali za geneva, badala yakujikita kwenye ushabiki, ingekuwa vema mleta hoja au waunga hoja wamekuja na vipengele vya kimataifa ambavyo mhe waziri amevivunja kwa taarifa yake hili tuelimishane na tupunguze kupotoshana mchana kutwa na sijui FRELIMO mbona tuliwatambua n.k, nikama kung'ang'ania kumpeleka mwanao shuleni miguu peku kisa hata wewe ulisoma ukiwapeku( isitoshe ndio maana unafikra peku)
 
Huyu si ndiye aliyesikika akiongea kwa jazba kuwa hawatamruhusu rais wa Madagascar Andry Rajoelina kuendelea kwa sababu alikuwa ni DJ muhuni na aliingia kwa mapinduzi ya wanajeshi waasi? Inabidi atujulishe walifikia wapi na Rajoelina wa Madagascar kabla hajaanza kutueleza masuala ya waasi. Kwa ufupi genge la Madikteta wa AU wameshindwa kutetea maslahi ya wana wa Africa na wamebaki kulindana wenyewe tu. Matokeo yake kila mara wanakuwa wa mwisho kuingilia pale kunapokuwa na matatizo yanayowakabili wananchi wanyonge. Mfano mzuri ni Somalia mpaka sasa AU wamekaa kimya utadhani mabo ni shwari huko.

hata hiyo road map ya au anayo itetea huko ivory coast iliishia wapi? si mpaka wafaransa na waasi walipovamia ikulu ya gagbo ndio suluhu ikapatikana? sema wao wameshindwa kutekeleza sera zote zenye kuhusiana na demokrasia katika afrika ya kenya tuliyaona kama sio nchi za magharibi kumpa uwezo koffi annanh, mpaka leo hii serikali ya umoja wa kitaifa isingekuwepo kenya bali hiyo vita. kwa ufupi vita afrika inaletwa na viongozi lege lege wa afrika, wasio penda kufuata demokrasia, wanao weka mbele familia zao kuliko wananchi wa nchi zao
 
I personally heard the talks between our Minister (Membe) and the BBC this morning. He really showed the kind of diplomatic leaders we are currently having; very bad.

Nilijiuliza, hivi huyo Balozi wa Libya anapaswa kutii mamlaka ya nani? (Balozi) Anajua fika bosi wake wa zamani (Gaddafi) hayuko tena madarakani na order imetolewa na watawala wapya (waasi), japo hawajaapishwa, juu ya mambo mbalimbali yahusuyo taifa lao ikiwamo kwa balozi za nje kupeperusha bendera mpya; hivi ni mpumbavu gani angekuwa na ujasiri wa kukataa agizo kama hilo? Nani asiyependa maisha yake, potelea mbali kazi?

Kitendo alichofanya Membe ni kibaya mno kiasi kwamba kinahatarisha hata usalama wa raia wa Tanzania na waafrika wengine waishio Libya kwa sasa. Kuna taarifa kwamba waasi wanawalenga waafrika weusi kwa madai kwamba wanmuunga mkono adui wao Gadafi kama ilivyopostiwa hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/167969-libya-rebels-now-target-%91blacks%92.html

Hivi waasi wakisikia statement ya Membe unategemea watawafnyia nini watanzania wenzetu waishio huko? Busara zaidi zitumike kwenye suala hili badala ya kujuana na ubabe wa kijinga.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hii inawezekana ni baada ya serikali ya waasi kutangaza dau la $2,000,000 kwa yeyote atakayemuua Gadaffi au kuwezeshwa kukamatwa. Inatupapicha yawezekana Dictator Gadaffi amehifadhiwa na serikali ya utawala legelege.



Fikra mgando. Maamuzi ya kutotambua waasi yasingeweza kuchukuliwa kabla ya utawala wa Gaddafi kuanguka na hili limetokea siku chache tu zilizopita. Pili, uamuazi huu umezingatia pia kikao cha baraza la usalama la AU ambalo Tanzania nayo ilishiriki. Tatu, suala la waasi kuamua kubadilisha alama za nchi yao bila kufuata utaratibu na kama Vienna Convention inavyosema nalo si la kuliangalia kwa jicho jepesi. Hivi kuna ayaejua ni nani anaongoza Libya sasa hivi? Utatambuaje kikundi cha waasi ambao bado hawajashika hatamu za utawala zaidi tu ya kuteka miji na majengo?
 
Maskini Tanzania, yaani sisi leo tunafuata? Hawa wangekuwa wakati wa harakati za ukombozi PLO, POLISARIO, ANC, FRELIMO n.k wasingepata nafasi Tanzania. je wanaitambua serikali ya Misri au ya Tunisia? Na hiki kipimo cha "Kuapishwa kwanza" kimeanza lini. Si waseme tu kuwa urafiki ulikuwa na Gaddafi lakini siyo wananchi wa Libya? Hii ni aibu kwa Tanzania.

Akihojiwa na waandishi wa habari nyumbani kwake msasani, aliyekuwa msuruhishi wa mgogoro wa Burundi kipindi, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliulizwa kuhusu aliyekuwa rais wa Burundi, Pierre Buyoya kama ni rais halali au haramu. Alichojibu ni kuwa " Hakuna rais haramu pale, vinginevyo tusingekaa naye mizani ili kutafuta usuruhishi wa mgogoro" Hivyo kwa kuwa alikuwa ndiye Kiongozi wa pale na kitendo cha kukaa naye meza moja ni halali...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hivi Tanzania lini iliwatambua waasi wa Tunisia na Misri, mbona hatukusikia haya ya kusubiri kuapishwa kwanza, je kama serikali ya waasi itaamua kuahirisha uchaguzi wa bunge hadi mwaka kesho itakuwaje. Tuseme ukweli bila kumng'unya maneno Gaddafi alikuwa amewashika viongozi wengi wa afrika including wa kwetu ndio maana wanakuja na hadithi za ajabu ajabu, karibu 20% ya bajeti ya AU ilikuwa inatoka Libya(Gaddafi), alitumia utajiri wa Libya kujijenga mwenyewe badala ya kuwajenga wananchi wake, alifadhili nchi nyingi za afrika na cash kwa marafiki zake inasemekana msafara wake ulikuwa unatembea na cash money nyingi ajabu.



Tunisia na Misri hawakukamata SILAHA ... ni tofauti kabisa na kinachotokea LIBYA
 
Red: Hapo ndio tunapojidhihirisha jinsi waTZ tulivyo SLOW na MAFALA. Tunakaa tunasubiri waje wajipendekeze kwetu ndio tuwatambue, kwa lipi hasa? Hiyo ndio kazi ya usalama wa taifa ya kutafuta majibu ya maswali hayo na sio kusubiri uletewe majibu. Majibu ya maswali hayo yana umuhimu sana kwa mahusiano ya kibiashara baina ya Libya na Tanzania. Wenzetu waliowatambua the so called "waasi" wameshawatafuta, wamezungumza nao, wakajadiliana mahusiano ya baadaye kibiashara baina ya nchi zao ndio wakawatambua. Rusia, Germany and China ambao were opposing NATO mission in Libya sasa hivi their intelijensia daily wapo Bengazi wanalonga na NTC, sisi tunasubiri eti waapishwe, mwee.. poor sisi, aliyeturoga sijui alitupa recovery medics wapi!!!!! Tunajiona maBOSS kumbe masikini wa kutupwa

Kama kuna mtu slow hapa basi ni wewe, katika foreign policy -ambayo hatuna- kuna overt na covert mission.

Tanzania hatuna hata comprehensive Foreign policy, achilia mbali covert mission zaidi ya kupeleka wanajeshi wastaafu walevi balozini.

Kusema kwamba waacheni waasi waonyeshe wanasimamia wapi hakumaanishi tu forego covert mission, labda kama uko slow ndiyo unaweza ku interpret hivyo.

Moreover, kabla ya kutaka kujipasua msamba kugombea biashara kwenye vita za watu, ingefaa kwanza uwe na cha kufanyia biashara.Tanzania is mostly an importer, kuanzia biskuti, pini mpaka mitambo ya umeme.Hizo export chache tulizonazo mostly ni agri products na minerals ambazo hatuna economic justification ya kuingia katika a diplomatic brouhaha kwa ajili yazo. Angalia usiuze ng'ombe kwa sababu ya kushinda kesi ya kuku.Angalia jitihada za kufanya biashara ya vitu ambavyo huna isikuingize gharama ya mahusiano ambayo ni kubwa zaidi na inaweza kukuharibia biashara kesho ambapo unaweza kupata uwezo wa kufanya biashara.

Tunajua viongozi wetu wanachemka sana, na Membe mchemfu, na the romantic story hapa ni ku buy into the west's oversimplification ya "the tyrant Gaddafi vs freedom fighters". Lakini tuepuke foreign policy ya copy paste.

The west, and not only governments, even individuals, collective has a habit of aligning -really masking- it's own personal ambitions with some lofty altruistic public positions. If our interests do not match theirs, and there is no reason to jump on the bandwagon, let us not.
 
Back
Top Bottom