Bernard Membe awataka vijana kutetea Taifa kwa nguvu zote

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Kauli ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Bernard Membe, kuwataka vijana wapiganie haki kwa nguvu zote na kulitetea taifa kwa gharama yoyote.

Inaashiria wapo viongozi ndani ya serikali na chama tawala CCM waliochoshwa na kukerwa na hali ya mambo ilivyo sasa hapa nchini.

Membe aliyasema haya jana katika tamasha la Campus Night lililoandaliwa na kanisa la VCC Victory Christian Centre.

Kanisa linaloongozwa na Mchungaji Huruma Nkone. Membe alisema Tamasha linapaswa kutumiwa na vijana kuitetea nchi kwa gharama yoyote pasipo hofu ya kuogopa jambo lolote. Alisema pia, vijana wengi hawana ajira.

Kauli hiyo aliisindikiza na takwimu ambayo inaonyesha ni 10% ya vijana kati ya vijana laki moja ndio wamepata ajira.

Tamasha hilo lilikusanya idadi kubwa ya vijana wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam. Kwa kauli ya Membe nashawishika moja kwa moja kuwaunga mkono CHADEMA katika harakati zao za kupigania haki ya wanyonge.

Membe ameonyesha kupingana na misimamo ya viongozi wenzie kuwa harakati za CHADEMA hazina tija kwa taifa.
 
Ukitaka kuwajua wanasiasa wenye malengo ya "kisiasa" shika hii kauli halafu subiri nyingine kwenye tukio jingine then linganisha

Mark these words, then after few weeks ataalikwa pengine ataongea mengine....kama kawaida yao
 
anauchu na uprezidaa huyu? mpaka anajikuta anaropoka hovyo hovyo. Mpaka 2015 atakuwa chizi kabisa
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    7.2 KB · Views: 23

Similar Discussions

Back
Top Bottom