Membe asaini mkataba bila kuusoma nchini China, mwakilishi aja juu, rais Kikwete amtetea!

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Malalamiko ya watanzania kwamba viongozi wanasaini mikataba bila kusoma sasa yamethibitishwa wazi na mwakilishi wa Dimbani zanzibar Bw.Mwinyi Haji Makame(CCM) kwa Bw. Bernad Membe ktk kile kuonyesha kuwa careless kwa kufikia kusaini mkataba ambao hakutakiwa kusaini ambapo mwakilishi anadai kwenye video hiyo iliyoko ndani ya youtube.

Mwakilishi huyo alipokuja juu mbele ya JK kwamba kwanini waziri wake amesaini Mkataba ambao si wake? JK kama kawaida yake ya kutetea uzembe alimuombea amsamehe kwamba hayo ni makosa ya kibinadamu tu.

Kwahiyo watanzania kilio chenu cha miaka mingi cha kulalamikia mikataba kusainiwa bila kusomwa sasa kimedhibitishwa wazi na Bw. Mwinyi kuwa viongozi ni watu wasio na huruma na nchi hii tunakupandisha ndege hadi China tunakulipa Posho za kukatana na shoka halafu still hufanyi kazi yako tunayokulipa nafikiri baada ya kuangalia video wale wote mliokuwa mnawaza labda Bw. Membe anafaa kuwa rais wa nchi hii mtabadili mawazo yenu. waandishi tusaidieni kumuuliza ilikuwaje asaini mkataba bila kusoma kwanza anachosaini??

Angalia video hii:

 
Last edited by a moderator:
cc tunaotumia opera mbona hatuwezi kuiangalia? Tunaomba tuwezeshe kwa njia nyingine, au ukiingia youtube inaitwa video gani?
 
Mh, kwa hali hii ya viongozi maslahi hatufiki kokote, halafu eti anataka tumpe nchi,
si atatuuza kwa mikataba kama ile ya kina chifu Magungo!...
 
cc tunaotumia opera mbona hatuwezi kuiangalia? Tunaomba tuwezeshe kwa njia nyingine, au ukiingia youtube inaitwa video gani?
kamati ya maridhiano six: maoni ya wawakilishi kwa tume ya marekebisho ya katiba; part8
 
Japo Mie siyo Fan wa Membe (Mbopo), suala hili linakilemba cha siasa za kuelekea 2015 na mlalamikaji anajaribu kujisogeza karibu na Kambi ya Lowassa toka upande wa pili wa Muungano. I like Lowassa……..kapanga vema kete zake katika majukwaa na matukio mbalimbali. Ni bandika bandua!

Nauliza tu kwa kutaka kujua; nje ya Nchi Mawaziri huwa wanasaini Miswada (Bills) au Mikataba (Contracts) na Makubaliano (MoU)?
 
Mungu wangu! halafu huyu ndie anataka tumkabidhi nchi yetu nzuri Tanzania tuliyopewa na Mungu
kwa upendeleo!!!!!! Si atatuuza na watoto wetu na wajukuu."Ee Mungu tuepushe na balaa la watu wa
aina hii,hata wakitangulia mbele ya haki ni mapenzi yako yatimizwe"
 
Tatizo lile lile kuzungumzia watu badala ya mfumo.....unadhani asingekuwa Membe au huyo dada angefanya tofauti? kwanini utegemee utashi wa mtu na sio mfumo?. Badala ya kukomaa na mtu (Membe) pigania mfumo mzuri ambao by virtue of your position ulitakiwe ndio wewe usaini, na kwamba akisaini mtu mwingine muswada/mkataba unakuwa void.
 
Tanzania imekuwa ni nchi ya kitu kidogo.Jamaa ana 10% kwenye huo mkataba,kwa hiyo hana haja ya kuusoma.Ndo maana tunaomba MUNGU CHADEMA ikichukua nchi 2015,ivunje mikataba hii,kwa sababu ni batili.Haina maslahi kwa nchi zaidi ya kunufaisha mtu au kikundi cha watu fulani.
 
Ni kweli bro na waziri makame alipomuuliza membe mbona umesign mkataba sio wako. Membe akamjibu wewe huna tools. Mpaka hapo wazanzibari wakisema hawautaki tena muungano jee wanakosea?
 
Back
Top Bottom