Membe adaiwa kusaidia kampuni ya wanandugu (MEIS) kuchota bilioni 54

sijui kama ni mimi tu ndio siewlewi, hivi hizo hela zinazogombewa chanzo chake ni nini?
cautions Dar over $20m debt cash

Monday, 31 January 2011 07:41

By The Citizen Reporter
Dar es Salaam. The Libyan government has told the government of Tanzania it will consider unlawful any move to release $20 million (about Sh30 billion) from its account, meant to assist local investors, which is at the Tanzania Investment Bank (TIB).

The Libyan government issued notification to its Tanzanian counterpart in a November 2010 letter to the Ministry of Finance and Economic Affairs, copied to the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, after a local company, MEIS Industries Ltd, claimed it has won an investment agreement with the two governments, for the construction of a cement factory in Lindi Region.

The $20 million held at the TIB Account Number 004-200-0002216-01 is accrued from a settlement arrangement between the two governments on how to settle a debt that Tanzania owes Libya.

Under the arrangement, on July 20, 2005 the Libyan government agreed to cancel interest and penalty interest on the money it is owed by Tanzania to the tune of $101,687,077.50.

On March 4, 2009, the two governments reportedly agreed that the $20 million-plus interest, which is held at the TIB, shall be advanced to MEIS Industries Ltd for the construction of the cement factory in Lindi region.

According to the understanding between the two governments, the arrangement was rescheduled through a debt swap where $20 million was earmarked for investment in Tanzania in sectors to be mutually agreed .

However, in its letter to the Finance ministry, the Libyan government said it was agreed that MEIS Industries Ltd should repay the loan plus accrued interest to the TIB account within the terms to be agreed upon between the two governments and the company.

It said the investment agreement was prepared and signed by the government of Tanzania, the TIB and MEIS Industries, and was sent to Libyan authorities for perusal and clarification.

The letter said the Libya informed Tanzania that it was not happy with the terms and conditions of the investment agreement and it would not be in a position to endorse it.It added that there has been no agreement signed between the two countries to that effect.

The letter stated that there were two copies of the intended investment agreement, in which one provides for guarantee by the government of Tanzania and the other one showing that the government has not issued guarantee for the money to be borrowed by MEIS.

"The Tanzanian government knew the nature of the arrangement to the effect that no agreement has been signed but it has not taken serious steps to rectify the anomalies," the Libya says in the letter signed by its general director of Loans and Debts Department, Mr Abdulhakim M. Elmisurati.

"It is our view that necessary steps should be taken by the government of Tanzania in order to set the atmosphere free from this embarrassing situation," says letter, a copy of which was seen by The Citizen.

cautions Dar over $20m debt cash

The letter said the Libya informed Tanzania that it was not happy with the terms and conditions of the investment agreement and it would not be in a position to endorse it.It added that there has been no agreement signed between the two countries to that effect.

The letter stated that there were two copies of the intended investment agreement, in which one provides for guarantee by the government of Tanzania and the other one showing that the government has not issued guarantee for the money to be borrowed by MEIS.

“The Tanzanian government knew the nature of the arrangement to the effect that no agreement has been signed but it has not taken serious steps to rectify the anomalies,” the Libya says in the letter signed by its general director of Loans and Debts Department, Mr Abdulhakim M. Elmisurati.

“It is our view that necessary steps should be taken by the government of Tanzania in order to set the atmosphere free from this embarrassing situation,” says letter, a copy of which was seen by The Citizen.

mkuu akhsante sana unajua hawa waandishi wetu wanaitumia kalamu vibaya sana, kwa habari ya kwanza "mtanzania" imelenga personal attacks tu haikueleza nini chanzo kumbe kuna madudu ya serikali yamejificha na kama unavyojua tena RA na serikali yake
 
Kundi la JK linatumia style ileile waliyoitumia kumchafua Salim A.Salim 2005. Hizi ni harakati za kuwania urais 2015 na siasa za maji taka.
 
Hapa hakuna suala la siasa wala 2015, kinachogamba hapa ni maslahi ya kiuchumi na hoja zinazojengwa hazielezei ukweli wote kuhusu sakata hili. Ukweli ni kwamba,miaka ya nyuma Serikali ya Libya iliikopesha Serikali ya Tanzania mafuta . Deni hilo ni sehemu ya madeni ya nje ambayo serikali imekuwa ikidaiwa.

Kwakuwa deni hili ni moja ya yale madeni yaliyokaa muda mrefu bila mwenye fedha zake kudai, likaingizwa kwenye mpango wa DEBT SWAP- ambao Serikali au taasisi zisizo za kiserikali zimefanya mazungumzo na MDAI kuomba asamee deni kwa ahadi kwamba fedha hizo zitakazosamehewa zitatumika katika miradi ya maendeleo yenye kusaidia kuwaondoa wananchi kwenye umasikini.

Kwa kesi ya deni la Libya, METL ilikuwa ni moja ya makampuni kadhaa yaliyojitokeza kufanya mazungumzo na Serikali ya Libya kuomba deni hilo lisamehewe, ili sehemu ya fedha za msamaha wazitumie kuwekeza katika mradi wa maendeleo nchini.

Harakati za METL hazikuzaa matunda,kwani baadhi ya watendaji katika serikali ya Libya walifikiria badala fedha hizo kupewa kampuni ya Tanzania, bora ziwekezwe kwenye hoteli ya Bahari Beach ambayo inamilikiwa na Serikali ya Libya kupitia kampuni ya Libya Investment Authority (Sovereign Fund)
http://www.libyaninvestmentauthority.com/ .

Uamuzi huo ulichukua muda mrefu kuwa executed....kwasababu wanazojua wao walibya (pengine kwakuwa hawakuwa na interest ya uwekezaji kwenye miradi iliyopo sub-saharan Afria-kwani Sovereign Fund hii imejikita zaidi kwenye uwekezaji katika mafuta, na bishara nyingine za mabenki etc barani Ulaya.

METL (mohamed enterprises) baada ya kuona bado fedha hizo zipo nchini na hazijachukuliwa na Libyan Investment Authority kuwekezwa katika hotel ya bahari beach....wakaamua kufanya ‘uchakachuaji' kwa kushirikiana na AFISA WA UBALOZI WA LIBYA na baadhi ya watendaji wa Benki kuu, ili walipwe fedha hizo (kama deals za EPA zilivyokuwa zikifanyika). Mchakato wao wa kuchakachua ulifika mbali....lakini kwa bahati mbaya kwao, kuna mtu aliyeistua Serikali ya Libya kupitia BALOZI wao...wakazima jalibio hilo. Vile vile Afisa huyo wa Libya alisimamishwa kazi na kurejeshwa kwao Libya. Juhudi za Mohamed Enterprises kumshtaki afisa huyo hazikuzaa matunda kwakuwa alikuwa na kinga, na alishakuwa recalled kwao.

In the meantime, Balozi mpya wa Libya ambaye yupo well-connected na Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Libya na CEO wa Mfuko wa Libyan Investment Authority, aliwashawishi Serikali yake.....waruhusu fedha zao ziwekezwe nchini kwa kuipatia local company. Wazo la Balozi huyo lilikubalika kwao, na yeye akapewa jukumu la kutafuta local company ambapo yeye aliipendekeza kampuni ya MEISE (ya hao ndugu watatu wanaoongelewa). Balozi aliichagua kampuni hiyo kwasababu yeye alikuwa na mahusiano ya karibu na Mmoja wa wenye kampuni hiyo Bw. Islam ambaye ni Balozi wa Heshima wa Nchi ya Comoro hapa Tanzania. Mahusiano yao ya kibalozi ambayo baadaye yalikuwa cemented zaidi na ushirikiano wa Comoro na Libya katika harakati za Libya kuisaidia Serikali ya Comoro kukikomboa kisiwa cha Anjuan, yalipelekea AUTHORITIES kule LIBYA kuafiki moja kwa moja pendekezo la Balozi wao kwamba fedha zile ipewe kampuni ya BW Islam kwa ajili ya uwekezaji katika UJENZI wa kiwanda cha kutengeneza CEMENT kule LINDI. Kampuni ya MEISE iliamua kuwekeza kwenye kiwanda hicho Mkoani Lindi katika jimbo la Mchinga, kwakuwa eneo lile kuwa limestone kwa wingi sana, vile vile walikuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika kutoka SONGAS. Lengo lao lilikuwa ni kuuza cement hiyo nchini na nyingine ku export nchi za jirani hasa Zambia na Msumbiji ambako kuna mahitaji makubwa ya CEMENT.
Benard Membe, kama Mbunge wa kutoka Mkoa wa Lindi, amekuwa very supportive kwa mradi huo,kwani ungetoa ajira kwa wananchi wa mkoa wa Lindi na kuuinua mkoa wao kiuchumi. Si ajabu kama katika mikutano yake na Walibya ali express support ya mradi huo na kuwapa confidence Serikali ya Libya kwamba mradi huo unakwenda mahala salama na faida zake zi wazi.

Mpaka leo Mohamed Enterprises, hawajasema fedha hizo walitaka kuzifanyia nini? Na faida za mradi wao zingekuwa ni zipi? Lakini Pamoja na hayo, MWENYE FEDHA ZAKE, akiamua kumpatia mtu mwingine.....wao kwanini wawe na NONGWA....kwani waliwekeza mpaka waone ni haki yao? Katika historia ya DEPT SWAP nchini Mohamed Enterpirses wamekwishawahi kupewa pesa nyingi sana toka enzi za awamu ya pili....watueleze wamewekeza wapi? Matunda yake ni nini?
Kwa maoni yangu.....haya makampuni yanayopigana leo nani apewe fedha hizo....yanachelewesha maendeleo kwa wananchi...iwe wa Lindi au pengine ambao Mohamed Enterpirses alikuwa anafikiria kuwekeza.......Tuache kupigania maslahi binafsi...tufikirie wananchi wengi masikini wanaosubiria ajira....
NA kwa gazeti la Mtanzania hili linajulikana kwa siasa za majitaka dhidi ya watu wanaowadhania wanaingilia kati ndogo za mabosi wao za 2015....
Mkuu,
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti serikali ya Libya inapinga hizo pesa kupewa MEISI na pia lawyer anayewakilisha serikali ya Libya, Peter Swai anasema hakuna agreement yoyote kati ya MEISSI na Libya Gov?
 
Hizi pesa wanazogombania ni Mkopo?
Na kama ni Mkopo Serikali ya Tanzania inatoa guarantee?
 
Hapa hakuna suala la siasa wala 2015, kinachogamba hapa ni maslahi ya kiuchumi na hoja zinazojengwa hazielezei ukweli wote kuhusu sakata hili. Ukweli ni kwamba,miaka ya nyuma Serikali ya Libya iliikopesha Serikali ya Tanzania mafuta . Deni hilo ni sehemu ya madeni ya nje ambayo serikali imekuwa ikidaiwa.

Kwakuwa deni hili ni moja ya yale madeni yaliyokaa muda mrefu bila mwenye fedha zake kudai, likaingizwa kwenye mpango wa DEBT SWAP- ambao Serikali au taasisi zisizo za kiserikali zimefanya mazungumzo na MDAI kuomba asamee deni kwa ahadi kwamba fedha hizo zitakazosamehewa zitatumika katika miradi ya maendeleo yenye kusaidia kuwaondoa wananchi kwenye umasikini.

In the meantime, Balozi mpya wa Libya ambaye yupo well-connected na Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Libya na CEO wa Mfuko wa Libyan Investment Authority, aliwashawishi Serikali yake.....waruhusu fedha zao ziwekezwe nchini kwa kuipatia local company. Wazo la Balozi huyo lilikubalika kwao, na yeye akapewa jukumu la kutafuta local company ambapo yeye aliipendekeza kampuni ya MEISE (ya hao ndugu watatu wanaoongelewa). Balozi aliichagua kampuni hiyo kwasababu yeye alikuwa na mahusiano ya karibu na Mmoja wa wenye kampuni hiyo Bw. Islam ambaye ni Balozi wa Heshima wa Nchi ya Comoro hapa Tanzania. Mahusiano yao ya kibalozi ambayo baadaye yalikuwa cemented zaidi na ushirikiano wa Comoro na Libya katika harakati za Libya kuisaidia Serikali ya Comoro kukikomboa kisiwa cha Anjuan, yalipelekea AUTHORITIES kule LIBYA kuafiki moja kwa moja pendekezo la Balozi wao kwamba fedha zile ipewe kampuni ya BW Islam kwa ajili ya uwekezaji katika UJENZI wa kiwanda cha kutengeneza CEMENT kule LINDI. Kampuni ya MEISE iliamua kuwekeza kwenye kiwanda hicho Mkoani Lindi katika jimbo la Mchinga, kwakuwa eneo lile kuwa limestone kwa wingi sana, vile vile walikuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika kutoka SONGAS. Lengo lao lilikuwa ni kuuza cement hiyo nchini na nyingine ku export nchi za jirani hasa Zambia na Msumbiji ambako kuna mahitaji makubwa ya CEMENT.

Imebainika kuwa, wakati kesi ya MeTL ikiwa inaendelea siku chache badaye MEIS Industries ilifungua kesi namba 124/2010 dhidi ya Serikali ya Libya ikitaka ilipwe dola milioni 20 za Marekani na gharama za usumbufu za dola milioni 14.

Salaama umejitahifdi kutufafanulia ila kuna mambo kadhaa bado yanaleta mkanganyo hapa:
1. Umesema deni lenyewe ni kati ya madeni yaliyokaa muda mrefu bila mwenye deni kudai..! Hapa inachanganya kama mwenye deni hadai basi kimsingi deni linakwisha au hakuna deni tena, tofauti na EPA wenye madeni walidai lakini hawakulipwa kwakuwa nchi ilikuwa haina pesa za kuwalipa na ndipo sasa kukawa na "Debt Conversion/Swap" za kitapeli/kijanja (EPA).

2. Hujagusia juu ya kesi iliyofunguliwa na kampuni ya MEIS na kuidai serikali ya Libya kiasi cha USD 34mil ambapo USD 20mil ni Dai kamili na USD 14mil ni fidia. Sasa kama wao walipendekezwa na serikali ya Libya kupewa hizo pesa bure?? ili wawekeze iweje leo waidai serikali ya Libya na madai yao yana na usumbufu?

Sijui labda ni uelewa wangu mdogo wa haya maswala lakini hakika yanachanganya tena hasa ulipoweka maelezo yako, nina imani utafafanua zaidi ili wana jamvi wenye kuchanganyikiwa kama mimi waweze kuelewa kwa kina zaidi.

Hata hivyo pamoja na yote swala la 2015 ndio source ya habari hii, RA na kundi lake wanatumia habari hii kumchafua Bw. Membe ili kama kweli yupo kwenye mbio za urais wampunguze speed au ajitoe kabisa. Inawezekana yeye anafanya ufuatiliaji huu kwa manufaa ya wananchi lakini kwa kuwa kuna loophole ya kumchafua ndio maana inafanyika hivyo.
 
kazi kweli kweli nyoka anazidi kukamaa na gamba lake na kuzalisha magamba mengine zaidi.wanajaribu kuyavua magamba lakini hayavuliki.siasa ya ccm ni mchezo mtamu kweli

Hatimaye MEMBE amekiri kuwa ana uhusiano wa karibu na ile kampuni ya MEISS ambayo anataka iende jimbon kwake ikajenge kiwanda cha saruji......membe amesema kua kampuni hiyo ana uhusiano nayo kwa kua ni rafiki zake.....
My take:sakata hili liliibuka last weekend ambapo gazet la mtanzania liliripoti na inaendelea hukohuko kwenye gazeti la mwanamagamba(mtanzania)
 
[/COLOR]Mkuu,
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti serikali ya Libya inapinga hizo pesa kupewa MEISI na pia lawyer anayewakilisha serikali ya Libya, Peter Swai anasema hakuna agreement yoyote kati ya MEISSI na Libya Gov?
[/FONT][/COLOR][/SIZE]

Katika kuchambua suala hili, kuna mambo mawili ya msingi ambayo ni muhimu kuyafahamu.....katika masuala ya uwekezaji nje ya nchi, Serikali ya Libya ina more than one CENTRE OF POWER (or rather the place where decisions are made). Centre hizo ni WIZARA YA MAMBO YA NJE; WIZARA YA FEDHA (kwa maana ya Libyan Investment Authority) na OFISI YA WAZIRI MKUU.

Kwa bahati mbaya, Centres hizo haziko coordinated na mara nyingi maamuzi yake yanategemea wakubwa wa centre hizo wana maslahi gani.

Mara nyingi Interest za Foreign ni ku advance maslahi ya kidiplomasia kwa kutumia uchumi, wakati wale wa Libyan INvestment authority wao wanaangalia ilipo faida. KWa issue hii ya TZ, foreign Libya walikuwa wana support mradi wa MEISE na HAZINA (investment authority) walitumiwa na METL ku spoil deal ya MEISE. Ndio maana ukifuatilia utagundua KESI ya Serikali ya Libya inasimamiwa na Upande wa Investment Authority (Sio ajabu legal fees inalipwa na METL) kwani kwa mkanganyiko uliopo Libya hivi sasa, sioni mtu mwenye interest kule ya kuendesha kesi ya kufuatilia uwekezaji wao hapa nchini-hasa kwa kipindi hiki ambacho Libyan Investment authority yenyenye inakabiliwa na assets freeze sehemu nyingi duniani kutokana na shinikizo la WAZUNGU dhidi ya Ghadafi.

Rekodi ya utendaji ya HAZINA ya LIBYA kupitia Libyan INvestment Authority sio NZURI. Wana sifa kubwa ya kuwa corrupt na inefficient. Kawaida yao ni kutumia fedha nyingi kununua miradi (ili wapate commission binafsi) then wanai neglect...mfano mzuri ni ile transaction ya ununuzi wa GRAND REGENCY HOTEL (angalia Kenya's Finance Minister Resigns over Controversial Sale of Nairobi Hotel to Libyan Investment Company. - Free Online Library
Mfano mwingine wa kuneglect miradi yao ni hotel ya Bahari BEach ambayo imewachukua miaka mingi kuanza kuitengeneza toka walipoichukua under Debt Swap Arrangement.

Tetesi, zilizopo ni kwamba METL walipata connection kule Wizara ya Fedha ya Libya na kuitumia connection hiyo ku spoil deal ya MEISE.....
Ni kutokana na hali hiyo......MEISE wakaamua kushtaki....

KWa hali ilivyo sasa, yule mtu wa Foreign Affairs wa Libya ni miongoni mwa viongozi waliokimbia nchi mara baada ya matatizo ya Libya kuanza.....hivyo kuondoka kwake kunatoa fursa ya wale wenye links za HAZINA ya Libya kupush for agenda ya ku reverse maamuzi yaliyokuwa in favour of MEISE wakisimamiwa kikamilifuna METL (interested party).
 
NASHUKURU FREDMLAY kwa kutaka ufafanuzi.....nijibie hoja zako kama ulivyoziweka...

Salaama umejitahifdi kutufafanulia ila kuna mambo kadhaa bado yanaleta mkanganyo hapa:
1. Umesema deni lenyewe ni kati ya madeni yaliyokaa muda mrefu bila mwenye deni kudai..! Hapa inachanganya kama mwenye deni hadai basi kimsingi deni linakwisha au hakuna deni tena, tofauti na EPA wenye madeni walidai lakini hawakulipwa kwakuwa nchi ilikuwa haina pesa za kuwalipa na ndipo sasa kukawa na "Debt Conversion/Swap" za kitapeli/kijanja (EPA).

One thing that is undisputed, ni kwamba deni hili ni la muda mrefu.... pengine nimekosea kusema deni lililokaa muda mrefu bila kudai- I should have instead say...deni lililokaa muda mrefu bila serikali kulipa japo linatambuliwa na kuorodheshwa katika external debt. Madeni ya aina hii mengi hasa ya nchi kwa nchi yalifutwa chini ya utaratibu wa HIPIC na kwa upande wa wadai ambao ni non Paris Club creditors....mazungumzo ya nchi kwa nchi yamekuwa yakifanyika...Libya ikiwa ni moja wapo.

2. Hujagusia juu ya kesi iliyofunguliwa na kampuni ya MEIS na kuidai serikali ya Libya kiasi cha USD 34mil ambapo USD 20mil ni Dai kamili na USD 14mil ni fidia. Sasa kama wao walipendekezwa na serikali ya Libya kupewa hizo pesa bure?? ili wawekeze iweje leo waidai serikali ya Libya na madai yao yana na usumbufu? Sijui labda ni uelewa wangu mdogo wa haya maswala lakini hakika yanachanganya tena hasa ulipoweka maelezo yako, nina imani utafafanua zaidi ili wana jamvi wenye kuchanganyikiwa kama mimi waweze kuelewa kwa kina zaidi.

Swali hili nadhani nimelijibia kwa kina kwenye thread ya juu..... Katika masuala ya uwekezaji, Kule Libya kuna centres of Power 3, kila moja ina operate kivyake. Watu wa MEISE walideal na Foreign ya Libya wakapata commitment ya Serikali ya Libya kupewa mkopo. Sasa baada ya spoilers (METL Mohamed Enterprises)- kutia mchanga transaction hiyo kwa kutumia connection/contacts zao na baadhi ya Corrupt Officials wa Libyan Investment Authority- ndipo MEISE wakaona wamegeukwa wakafungua kesi kudai makubaliano yao yaheshimiwe na walipwe fidia. Sooo unaposema SERIKALI YA LIBYA- lazima ufahamu unaongelea MAMLAKA IPI? YA HAZINA, ya FOREIGN au OFISI YA WAZIRI MKUU..

Hata hivyo pamoja na yote swala la 2015 ndio source ya habari hii, RA na kundi lake wanatumia habari hii kumchafua Bw. Membe ili kama kweli yupo kwenye mbio za urais wampunguze speed au ajitoe kabisa. Inawezekana yeye anafanya ufuatiliaji huu kwa manufaa ya wananchi lakini kwa kuwa kuna loophole ya kumchafua ndio maana inafanyika hivyo.
Mwisho wa siku hapa........la muhimu la kujiuliza who is the looser katika siasa za aina hii......sidhani kama ni MEMBE au wapinzani wake wa kisiasa....wanao loose ni mama zetu, baba zetu, ndugu zetu waliokuwa na matarajio makubwa ya kupata riziki zao kutokana na kufanikiwa kwa mradi huu wa kiwanda cha CEMENT..Hivi Urais huu unatafutwa kwa faida ipi? Kama lengo la kutafuta urais ni kuwatumikia wananchi ambao wengi wao ni masikini SANA.....basi hatua ya kwanza ya kuchukua ni kuachana na mbinu, hila na ushabiki wenye athari kwa matarajio ya wananchi wenyewe kujikwamua katika umasikini!
 
Hatimaye MEMBE amekiri kuwa ana uhusiano wa karibu na ile kampuni ya MEISS ambayo anataka iende jimbon kwake ikajenge kiwanda cha saruji......membe amesema kua kampuni hiyo ana uhusiano nayo kwa kua ni rafiki zake.....
My take:sakata hili liliibuka last weekend ambapo gazet la mtanzania liliripoti na inaendelea hukohuko kwenye gazeti la mwanamagamba(mtanzania)

- Wapi evidence mkuu? Na hili gazeti la Mtanzania ni la nani hasa?

Willie @ NYC, USA.
 
Salaama,

Asante kwa maelezo yako. Sasa, wewe huoni kuna conflict of interest kwa Membe kutumia uswahiba wake na MEISE kuvutia uwekezaji katika jimbo lake kwa upande mmoja, na kwa upande wa pili kutumia nafasi yake Wizarani kukwamisha shauri la kisheria ambalo Mohd Enterprises wanalitafuta kulipitisha hapo? Kwanini Wizara ya Mambo ya Nje inakwamisha jitihada za kisheria za MeTL (hata kama inaonekana wewe umeshaonyesha bias dhidi yao), kwanini Mahakama isiwe ndiyo ya kuamua kwamba wakose dili badala ya Wizara kukwamisha samasi kwa faida ya Membe na wadau wake? Wewe huoni tatizo hapo?
 
Acheni. Membe ni mmoja wa viongozi safi

Usafi wake upi huo? Wa kutumia nafasi yake kukusanya pesa kutoka maofisa wa ngazi za juu wa mataifa ya nje kujenga kitita chake cha kugombea uraisi 2015? Membe hawezi kulalamika eti gazeti la MTANZANIA lina mchafua wakati na yeye yupo bize kuchafua wenzake kupitia magazeti kama RAIA MWEMA.
 
haishangazi kuona wanatunga hadithi kama hizi kwani wanapigana sana kumchafua yoyote wamuonae kama ni threat kwao kuelekea 2015.
 
- Wapi evidence mkuu? Na hili gazeti la Mtanzania ni la nani hasa?

Willie @ NYC, USA.

A splendid question! Nani hajui wanachosimamia wenye gazeti hili? Halafu hiyo conflict of interest hapa inatoka wapi maana kiwanda kinajengwa nje ya jimbo la Membe na hawa waliifuatilia issue hii wao wenyewe na hakuna ushahidi kwamba MeTL waliomba kupelekewa summons na waziri akakataa. Hivi watu wanafahamu kesi mbili za MeTL zinahusu nini? Nafikiri watu wafuatilie hizo kesi ndipo watagundua utapeli ulipojificha.
 
haishangazi kuona wanatunga hadithi kama hizi kwani wanapigana sana kumchafua yoyote wamuonae kama ni threat kwao kuelekea 2015.

Hoja zenyewe za kuchafua hazina mashiko. Ni muendelezo wa nahau za yule bwana aliyeita wenzake nyoka wa mdimu na baadae akawa job less kwa roho mbaya yake.
 
Salaama,Asante kwa maelezo yako. Sasa, wewe huoni kuna conflict of interest kwa Membe kutumia uswahiba wake na MEISE kuvutia uwekezaji katika jimbo lake kwa upande mmoja, na kwa upande wa pili kutumia nafasi yake Wizarani kukwamisha shauri la kisheria ambalo Mohd Enterprises wanalitafuta kulipitisha hapo? Kwanini Wizara ya Mambo ya Nje inakwamisha jitihada za kisheria za MeTL (hata kama inaonekana wewe umeshaonyesha bias dhidi yao), kwanini Mahakama isiwe ndiyo ya kuamua kwamba wakose dili badala ya Wizara kukwamisha samasi kwa faida ya Membe na wadau wake? Wewe huoni tatizo hapo?
Wewe ndio huko neutral?
 
Usafi wake upi huo? Wa kutumia nafasi yake kukusanya pesa kutoka maofisa wa ngazi za juu wa mataifa ya nje kujenga kitita chake cha kugombea uraisi 2015? Membe hawezi kulalamika eti gazeti la MTANZANIA lina mchafua wakati na yeye yupo bize kuchafua wenzake kupitia magazeti kama RAIA MWEMA.

una hakika na hili uliloliandika hapa???
 
Hoja zenyewe za kuchafua hazina mashiko. Ni muendelezo wa nahau za yule bwana aliyeita wenzake nyoka wa mdimu na baadae akawa job less kwa roho mbaya yake.

kwa kuwa wapo kwenye operation maalum ya kuchafua naamini mengi ya uzushi yatakuja ila maji na mafuta vitajitenga siku zote
 
Usafi wake upi huo? Wa kutumia nafasi yake kukusanya pesa kutoka maofisa wa ngazi za juu wa mataifa ya nje kujenga kitita chake cha kugombea uraisi 2015? Membe hawezi kulalamika eti gazeti la MTANZANIA lina mchafua wakati na yeye yupo bize kuchafua wenzake kupitia magazeti kama RAIA MWEMA.
Kwahiyo mmekubali mnajaribu kimchavua MEMBE kupitia gazeti lenu la MTANZANIA kisa kujistukia kwamba, au kwa hisia zakinyume na maumbile umlizonazo ,eti yeye MEMBE anawachafua kupitia RAIA MWEMA? Je kama yeye MEMBE ausiki na vijishutma vyenu thidi yake kipitia RAIA MWEMA, umtajikaza kiume angalau sekunde kazaa na kumtaka radhi,na we JUHA tu kwamba unajidhalilisha bure
 
Back
Top Bottom