Membe akalia 200bn za Zanzibar

kama amezuia nampongeza kwani hizo pesa badala ya kufanyia mambo ya maana zingeenda kwa uamsho mbona mnasajili meli za nje lakini ni sumatra ndio inalipa kimataifa na hamtoi hata senti tano,umeme mmeshindwa kulipa ingawa mnautumia hakuna aliyewazui hata sasa jiondoeni tutaishi kwa raha huku bara
 
Si nchi maana hakuna nchi isiyo na vyombo vya dola! hakuna nchi isiyo na kiti UN.

Hawa watu ni waajabu sana, wamesahau kuwa mishahara ya Rais wa ZNZ hadi mfagiaji inatoka hazina Dar.
Wamesahau kuwa gharama za wabunge 50 zinatoka hazina.
Wamesahau kuwa si Ikulu wa maskani wanalipa umeme
Wameshau kuwa Spika na BWL wote ni wafaidika wa mishahara na mafao ya Tanganyika
Wamesahau kuwa Gharibu Bilal amepewa Bilioni 32 kwa ajili ya ZNZ
Wamesahau kuwa hawana bajeti ya jeshi wala polisi
Wamesahau kuwa viongozi wao wote wastaafu wanalipwa na Tanganyika


LET ZNZ GO! Hawa watu uwezo wao wa kufikiri unatisha! uchoyo na umimi umewajaa sana!
Sidhani kuwa wanahitaji ZNZ huru, wanachohitaji ni elimu kumwekea kila mznz huru.


Kaka umenena. Hawa jamaa wamefikia hatua mbaya sana ya kuudhi na nadhani uvumilivu unafika kikomo si muda mrefu. Ndiyo hawa hawa walikurupuka na kuanza kulia lia kwamba Zanzibar haijashauriwa wakatai serikali, kupitia kwa Prof. Tibaijuka walipowasioisha ombi UN la Tanzania kuongezewa ukubwa wa bahari kina. Kwa akili yao walidhani inachotwa bahari ya zanzibar wakati kimataifa hiyo tayari inahesabiwa kama sehemu ya Tanzania. Baada ya kuambiwa kwamba timu ya wataalam ilikuwa na wazanzibari wakaaibika na kutahayari.
 
Mbopo,

Naomba utuweke sawa kuwa:
[h=2][/h]
Hivi ni kweli ZNZ walipewa 200 billion?

na je ni kweli Membe hajatia signature?

kwani hizi pesa za bilateral zinatakiwa kutiwa sign na Membe au waziri wa Fedha?

Protocol inasemaje?

Kama ni za development projects kwa nini serikali ya UAE isiingize direct kwenye miradi ya maendeleo huko ZNZ kama wanavyofanya waChina?
 
mi napata tabu kweli na uwezo wa hawa watu (wazanzibari) kufikiri na kungamua mambo wao matatizo yao wanalia muungano kabla ya serikali yao ya kitaifa walikua wakilia tatizo ni ccm, sasa wamegeukia Muungano nadhani tukishatengana wataanza ooh tatizo tanganyika ipo mno karibu ndo maana hatufanyi biashara.
membe anahusika nini na kusign pesa za msaada? juzi jumuia ya ulaya ilitoa pesa kwa Tanzania membe alikuwepo?
zanziba iwe nchi au si nchi wakipewa msaada wa zanzibar basi direct unaenda kwao nothing to do with Tanzania mliwahi kuona tende zikishushwa kariakoo? ni za zanzibar zinapelekwa zanziba....wakale.
propaganda kama hizi hazisaidii tatueni matatizo yenu kistaarabu.
 
It only takes a fool to believe in this asinine and wild allegation. Hivi kama hali ingekuwa hivi na Zanzibar wakawa wana haki na hicho kinachozungumzwa hali ingekuwa shwari hivi? Hakuna hata wakati mmoja ambao misaada imewahi kutolewa kwa jina la zanzibar ikapitia kwa serikali ya muungano. Watu wamejiunga na kukutanishwa na matatizo yao na sasa wanaamua kutaka kusingizia matatizo yao kwa Membe. Ndiyo wale wale wanaotuhumiwa kuwa na kampuni iliyosajili meli za Iran na sasa wanatunga uongo ambao hata mtoto wa chekechekea hawezi kuuamini.

Sasa wanawashambulia wale ambao ni voice of reason na walioonyesha objectivity kuhusu muungano kwa kuwaita wasaliti. Wakitaka kuondoka waondoke salama badala ya kutafuta visingizio vya kijinga!

Na baadaye wanaanzisha platform kwa ajili ya kuchonganisha na kuzusha
 
wacheni wizi nadhulma kaboresheni mikoa yenu ya bara natuachiwe pesa zetu zisije bara zinatutosha mbona hamna aibu.
 
nakwanini watanganyika walio wachache mnakataa kuwa sio muunga au kwa porojo za vyombo vya khabar tu shida ni muungano tu zanzibar huru kwanza
 
Zanzibar hairuhisiwi ku sign foreing aid kwasababu ZANZIBAR SI NCHI!

Jamani hili si ndiyo alisema Pinda miaka miwili iliyopita kuwa Zanzibar si nchi likaleta HULLABALOO huko Zanzibar?!

Je imekuwaje kwa hao mabwana kuwambia nyinyi SIO NCHI mbona humkuwashikia bango?

Membe anaweza kukataa ku-sign kama mkopo wenyewe unaona una masharti magumu ambayo TANZANIA repeat again TANZANIA haiwezi kulipa NOT ZANZIBAR ambayo haiwezi hata kulipa bills za umeme wake kwa TANESCO.
 
Mbopo,

Naomba utuweke sawa kuwa:
Hivi ni kweli ZNZ walipewa 200 billion?

na je ni kweli Membe hajatia signature?

kwani hizi pesa za bilateral zinatakiwa kutiwa sign na Membe au waziri wa Fedha?

Protocol inasemaje?

Kama ni za development projects kwa nini serikali ya UAE isiingize direct kwenye miradi ya maendeleo huko ZNZ kama wanavyofanya waChina?

Maswali magumu
majibu mepesi

lakini hatuna atakayekupa majibu JF

kwa sababu habari yenyewe ni uzushi
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

kwenye hili naona Membe kazushiwa

wazanzibari walivyo walalamishi tungekuwa tushawasikia wakilalamika na hasa toka kwa mawaziri wao ambao wako very outspoken
 
Balahau mbona lalamika na haya basi! Michele mnayochukua kyla, nyanya mpaka masalo kariakoo, vichwa vya ng'ombe hadi hasua vingunguti, rubi kilombelo, umeme wa bule, mavz kwa wazenj mawaziri wabunge madiwani...., hamjui cha mwenzio mavi kula uliwe!
 
Kwa kweli umejitahidi kiba maada ambayo hakika ina muguso mkubwa sana si kwa wazanzibari tu bali hata kwa wabara. Lakini imefikia mahali nachelea kukubaliana nawe asilimia mia kwa mia kwa sababu hii moja: Unaposema kunyimwa visa hao maofisa waliotakiwa kuhudhuria mkutano wa wa maendeleo ni kuhujumiwa kwa kuwa wabara hawaendi nadhani si kweli kabisa kwaani unapotaka kwenda nchi furani sio nchi yako inaayotoa visa bali ni nchi uendayo, mathalani ukitaka kwenda India lazima uende Ubalozi wa India Uliopo hapa nchini ili wakupe visa ya kukurusu kuingia nchini kwao na si vinginevyo. Aidha, Serikali ya Tanzania haina nafasi ya kuhoji kwa nini raia wake amenyimwa visa au kapewa. Hivyo kwa hili ambalo ninalifahamu vema na kwa jinsi ulivyotumia usitadi kulifanya lionekane la kweli inanifanya nisite kidogo kuamini unayoyasema. Ni vema tukajitahidi kulijua ipasavyo suala tunalotaka kulitoa handharani kuliko kutoa tuhuma nzito kama hizi wakati huna uhakika nazo. Mwisho sisemi yote uliyoyaandika ni uongo kwaani siyafahamu ila najitenga nawe kwa hili moja ninalolifahamu vizuri na inaonyesha dhahiri kuwa si kweli.
 
Back
Top Bottom