Meli za kivita za Urusi kupitia bahari ya Uingereza

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Kundi kubwa la meli za kivita za Urusi litapitia katika mlango wa bahari wa Uingereza.

Meli hizo zinaelekea Syria ambapo Urusi imekuwa ikisaidia wanajeshi wa Rais Bashar al-Assad kukabiliana na waasi.

Uingereza imetuma meli mbili zake za kivita kufuatilia kundi hilo la meli.

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema zitafuatiliwa "hatua kwa hatua" zikiwa karibu na maeneo ya bahari ya Uingereza.

Meli moja ya kubwa, ambayo inaaminika kuwa sehemu ya msafara huo wa meli, iliingia kwenye mlango huo wa bahari wa Uingereza (English Channel) kupitia karibu na eneo la Ramsgate.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameshutumu vikali hatua ya Urusi kuendelea kushambulia maeneo ya mji wa Aleppo kwa mabomu.

Maeneo ambayo meli hizo za Urusi zinapitia baharini ni ya kimataifa, na hayamilikiwi na Uingereza, lakini waziri wa ulinzi wa Uingereza Michael Fallon amesema ni lazima wazifuatilie meli hizo "kama sehemu ya kujitolea kwao kuilinda Uingereza."

Meli hizo za Uingereza HMS Duncan na HMS Richmond ziliondoka bandarini Portsmouth Jumanne kufuatilia meli hizo za Urusi ambazo zilikuwa zikielekea kusini kutoka Bahari ya Norway.

Meli kubwa katika msafara huo wa Urusi ni meli kwa jina Admiral Kuznetsov ambayo ndiyo pekee ya Urusi yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita. Meli hiyo inaweza kubeba ndege 50 na ina silaha hatari zikiwemo makombora ya kushambulia meli.

Mwandishi wa BBC aliyeko Moscow Steve Rosenberg anasema meli hizo zinakusudiwa kuimarisha uwezo wa Urusi kutekeleza shughuli za kijeshi Syria.

Hata hivyo, pia ni kama juhudi za kutuma ujumbe kwa nchi za Magharibi kwamba Urusi pia ina uwezo mkubwa kijeshi.
Image caption Admiral Kuznetsov inaweza kubeba ndege zaidi ya 50

Urusi tayari ina meli 10 karibu na pwani ya Syria ambazo zimekuwa zikitumiwa kushambulia waasi nchini humo.

Ingawa EU iliiwekea vikwazo Urusi kutokana na mzozo wa kivita mashariki mwa Ukraine na hata ya Urusi kuchukua umiliki wa Crimea, mataifa ya EU hayajaweza kuzuia Urusi kuingilia kijeshi Syria.

CHANZO: BBC Swahili
 
dah Si Uingereza ya Winston Churchill tena....I dedicate ''Pisha njia by TMK Wanaume'' to all Britons..:D:D
_92002160_russian_flotilla_map624_v2.png
 
Kuna umuhimu wa Urusi kweli kupeleka Meli iyo Syria Au kuna lingne la ziada??

Sipati picha iyo meli ndo ikaguswa kidogo tu na Kombora la Muingereza...

Tunataka dunia salama.
Yani hiyo siku akijaribu kutupia kombora kwenye hiyo Meli ya Urusi, hakuna siku watakayo jutia Mkuu.

Yani hiyo meli wataisindikiza kwa macho tuu. Na hawato igusa wala kuisimamisha.
 
Kuna umuhimu wa Urusi kweli kupeleka Meli iyo Syria Au kuna lingne la ziada??

Sipati picha iyo meli ndo ikaguswa kidogo tu na Kombora la Muingereza...

Tunataka dunia salama.
sijui kama umuhimu huo upo ila naona kuna haja ya urusi kuisaidia syria ipate utulivu na wasyria waishi kwa amani. america na ulaya wameshindwa jukumu hilo na nadhani hawakuwa na lengo la kurestore amani ya syria walipo amua kupeleka majeshi huko.
 
sijui kama umuhimu huo upo ila naona kuna haja ya urusi kuisaidia syria ipate utulivu na wasyria waishi kwa amani. america na ulaya wameshindwa jukumu hilo na nadhani hawakuwa na lengo la kurestore amani ya syria walipo amua kupeleka majeshi huko.
Na ile vita ya kuwakimbiza Iss Mosul njia ya kuingilia Syria ndo iko wazi naona Mrusi anajipanga kuwadhibiti kila kona.
 
Back
Top Bottom