Meli ya Bakhresa inaungua moto!

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu,

Napata taarifa sasa hivi kuwa kuna meli ya mafuta ya Bakhresa inaungua moto karibu na Posta ya zamani, naambiwa imeshaungua zaidi ya nusu...

Kama kuna wenye kuwa karibu na eneo hilo pls tunaomba updates zaidi
 
Wasiwasi wangu ni kuwa ikitokea ikalipuka basi watu walio maeneo ya jirani na eneo hilo wanaweza kuathirika vibaya sana...
 
Watu naambiwa wanasogea karibu na bahari kuangalia tukio kitu ambacho ni hatari hasa kwa meli za mafuta!
 
Ni maeneo ya karibia na Azania Front... Nimefanya kuwaarifu na polisi tayari wamepeleka msaada. Kuna boti inajaribu kuzima sasa
 
mkulu mie nilikuwa sijui kama bakhresa anamiliki meli za mafuta??...au ni meli iliyobeba mafuta kwa ajili ya magari ya bakhresa?
 
Watanzania kazi tunayo,watu wanasongelea eneo la hatari kiasi hicho? mh! tena meli yeyewe ni ya mafuta ni hatari sana endapo italipuka.
 
mkulu mie nilikuwa sijui kama bakhresa anamiliki meli za mafuta??...au ni meli iliyobeba mafuta kwa ajili ya magari ya bakhresa?
Ina rangi ya blue na haijakamilika kupakwa rangi... Ni ya mizigo kama ile iliyopinduka kule Zanzibar na ilikuwa imepaki jirani na parking ya boti ziendazo Zanzibar. Kwa maelezo niliyopata kwa wadau ni kuwa ile ni meli yake kabisa Bakhresa
 
Mungu atuepushe na haya mabalaa.sijujua ni kwa nini hasa waswahili huwa hatupendi kupitwa na kitu.maana hao watu wanaokwenda eneo la tukio wanataka waone kinacho endelea hapo,pasipo kujua kufanya hivyo wana hatarisha maisha yao.
 
JAMANI HAPA BAHARINI USAWA (JIRani) WA STAND YA POSTA YA ZAMANI KUNA BOAT INAUNGUA KICHEKESHO NI UZIMAJI WAKE.

GARI LA ZIMA MOTO LIMELETWA NA PANTON, KASHESHE NI KULIWEKA KWENYE USAWA UNAOTAKIWA ILI KUWEZA KUZIMA. HALAFU PEMBENI KUNA BOAT INAMWAGA MAJI MBALI KABISA NA PANTON.
........MI CJUI NICHEKE AU NISHANGILIE TU.
 
Tatizo tanzania hakuna fire za boti kuja kuzima mara moja. Kila la kheir, tutashukuru kama kutakuwa hakuna mtu aliyefariki katika moto huo
 
Wakuu,

Napata taarifa sasa hivi kuwa kuna meli ya mafuta ya Bakhresa inaungua moto karibu na Posta ya zamani, naambiwa imeshaungua zaidi ya nusu...

Kama kuna wenye kuwa karibu na eneo hilo pls tunaomba updates zaidi
mwezangu hapa ofisini kwetu tumeona moshi mkubwa but we donknow whats happening tumemuuliza mlinzi naye hajui, heee kumbe masikini pole yake.
thanks kwa info.
 
Jamini hii meli ina muda mrefu hapa ilikuwa ikipakwa rangi, ipo usawa wa stand ya posta mpya si kwenye meli za Zanzibar, si dhani kama ni ya mafuta kwa jinsi inavyoonekana.
Halafu si meli hii ni Boat tu.
 
Hayo mafuta yalikuwa yanapelekwa wapi? isije ikawa majamaa yameuza (kwa wizi) mafuta yote kisha yakailipua ili kuzima soo????!!!!,
 
Back
Top Bottom