Meli vita hatari zaidi ulimwenguni kwa sasa

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Dec 20, 2012
195
537
Jana wakati nimetoa makala fupi kuhusu melivita ya NIMITZ kuna mdau mmoja aliibuka na kuipinga kwa kusifia Melivita ya urusi ijulikanayo kwa Jina la Admiral Kuznetsov naomba nikamwambia alete data za KUZNESTOV hiyo aache kutulisha maneno yenyewe , mimi ni muumini wa data na ushahidi, yaani facts. Jamaa akatokomea mitini. Naomba ifahamike kuwa lengo langu katika makala hizi siyo kushindanisha Ukuu baina ya mafahari hawa wawili katika medani za vita (USA &Russia) bali ni kueleza ukweli juu ya mambo yalivyo.

Leo naomba niizungumzie kidogo hii Admiral KUZNESTOV Melivita daraja la Keria kama ilivyo NIMITZ ya Marekani.

Kwanza kabisa melivita hii inamilikiwa na Jeshi la wanamaji la Urusi, na ilitengenezwa na Shipyard sea watengenezaji wakuu wa Melivita za Urusi , melivita hii ilijengwa katika nchi ya Ukraine kipindi hicho kabla haijameguka kutoka Umoja wa Kisoviet (USSR), kwa sasa ndio melivita ya pili kwa uhatari duniani kwenye daraja la melivita aina ya keria baada ya NIMITZ ya jeshi la wanamaji la Marekani.

Melivita hii ilijengwa ili kuzuia makombora ya masafa marefu kutoka Majeshi ya NATO kuifikia Urusi, na inao mfumo maalumu wa kujilinda dhidi ya mashambulizi ya adui kwa maana ya kwamba inao uwezo wa kuzuia makmbora yanayoweza rushwa kutoka kwenye Nyambizi, ndege na mabomu. Ina mfumo wa kurushia maroketi.

KUZNESTOV ina uwezo wa kubeba tani 67,500 za mizigo ya kivita tofauti na NIMITZ ambayo inabeba hadi tani 100,000 (U can see the difference). Ina urefu wa mita 305 sawa na futi 1001 huku NIMITZ ina urefu wa Mita 333, inakimbia kwa spidi ya Km 54 kwa saa sawa na NIMITZ ya Marekani, pia inabeba ndege za kivita 40 na helkopta 24 za kivita huku NIMITZ ikibeba ndege hizo zaidi ya 85.

Ina uwezo wa kurusha makombora kwa umbali wa Km 15700 ikiwa katika mwendo wa taratibu huku NIMITZ ina uwezo wa kurusha makombora kwa kilomita 19,200 katika mwendo huo huo wa taratibu.

Jeshi la Urusi linazo melivita hizi 2 tu , kwa sababu baada ya kuvunjika kwa muungano wa Kisovieti na kiwanda cha kuzitengeneza hizi kilikuwa nchi Ukraine hivyo Ukraine ilizipiga baadhi yake tanji na baadae kuiuza moja kwa Wakala wa usafiri wa majini wa China mwaka 2002 kwa masharti ya kutoifanya Meli ya Kivita, Wakala huyo alikubaliana na masharti hayo na kusema China walitaka kumalizia utengenezaji wake na kuifanya kuwa meli ya kifahari kwa ajili ya hoteli na Casino ila ilipofika kwao waliigeuza matumizi na kumalizia Utengenaji wake na kuifanya kuwa melivita yao ya kwanza kabisa daraja la aircraft carrier..

Hivyo Urusi ilishindwa kuaanza utengenezaji upya wa meli hizi ndio maana imebakia kuwa nazo 2 tu, huku adui wake Marekani akiwa na NIMITZ 10.

KUZNESTOV imekuwa ikitumika katika oparesheni mbalimbali za Jeshi la Urusi na kwa sasa melivita moja ya KUZNESTOV ilitegemewa kuwa katika Bahari ya Mediterannia ikiyasaidia majeshi ya Anga ya nchi hiyo kufanya mashambulizi dhidi ya waasi nchini Syria. Ilitarajiwa kuwepo kuanzia mwezi July ila tarehe 19 Mwezi uliopita Jeshi la wanamaji la Urusi lilitoa taarifa kuwa KUZNESTOV haitoweza kufika katika mda uliopangwa kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao.

Wachunguzi wa masuala ya kiusalama walisema kuwa Oparesheni hiyo ya kuwasili kwa KUZNESTOV katika bahari ya Mediterannia kumecheleweshwa kwa kuwa Urusi inakabiliwa na uhaba wa marubani wa ndege vita MIG 29KR ambazo zinaruka kutoka melivita hii kwa ajili ya kumshambulia adui, ila juzi tarehe 17 Melivita hii ikiwa imeongozana na baadhi ya melivita zenye uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia zilionekana zikielekea bahari ya mediterannia kwa ajili ya Oparesheni ya kuwamaliza waasi nchini Syria.

Yote kwa yote KUZNESTOV ni daraja kubwa la Melivita aina ya keria ila bado kwa sifa chache nilizozieleza hapo juu haijaifikia NIMITZ niliyoielezea kwa uchache pia jana.

Ulinganifu wa zana hizi unajikita kwenye uwezo wa kubeba mizigo kwa tani, uwezo wa kubeba ndege vita na helkopta, pia uwezo wa kubeba makombora na silaha zingine za kujilinda dhidi ya adui. NIMITZ ina uwezo wa kurusha makombora ya masafa marefu ya Nyuklia ila hii haina uwezi huo.

Pia NIMITZ inaendeshwa kwa nguvu za Nyuklia (Nuclear power) hivyo kuifanya kuwa na uwezo wa kujiendesha miaka 20 mfululizo bila kuhitaji kujazwa mafuta ila hii KUZNESTOV inaendeshwa kwa mitambo ya gesi hivyo haiwezi kuhudumu miaka 20 mfululizo bila kujazwa nguvu kama NIMITZ.

Pia tunapokuwa tunalinganisha uwezo wa dhana hizi adimu za kijeshi tunajikita kwenye ukubwa wake. Pia lazima tuangalie na idadi yake kwa nchi husika. Hawa wanazo 2 wale wanazo 10 .

KUZNESTOV inategemewa kubaki kwenye huduma za kijeshi hadi mwaka 2030 itakapobadilishwa na Melivita nyingine ya kisasa na yenye uwezo zaidi yake. Kwa sasa KUZNESTOV ndio inatajwa kuwa melivita daraja la Keria ya pili kwa uhatari zaidi duniani baada ya NIMITZ ya Marekani. Kadri siku zinavyoenda teknolojia inabadilika na hawa mafahari wawili wanabadilika pia hivyo siyo ajabu kuona Melivita nyingine kali zaidi kutoka Urusi ikichukua nafasi huko miaka ya 2030 huku Marekani nao wakija na FORD kama mbadala wa NIMITZ.

I stand to be corrected.

Josephat Keraryo Nyambeya .

Wasiliana nami kupitia nyambeya@yahoo.com ili tuweze kubadilishana mawazo zaidi.
 
Mmmmmmmh hatari sana sana, hawa Jamaa kuna siku watakuja kuiangamiza Dunia kabisa. Lakini,mshangao eti unakuta Korea anaitunishia misuri Marekani. Marekani wanachofanya siku hizi ni kunyamaza tu na kuendelea na mambo yao. Lakini hawa watu ni hatari zaidi KIVITA,KIUCHUMI NA KISIASA.
 
Good article ila utakuwa umebase kwenye US media kama chanzo cha habari zako.... Leo hii kama vyombo vya habari kama vingekuwa na nguvu + kutumia lugha ya kiingereza kwenye mambo yao tungekuwa tunaujua ukweli Wa mambo...

Naaomba uingie hapa, hii ni website ya warusi utapata habari kemkem kuhusu majeshi ya warusi moja kwa moja kutoka kwao na sio propaganda za wamarekani

Russia Insider: True News, not just Headlines!
 
Una hakika kama vyombo vya habari vya Urus havifanya propaganda?!
 
Alafu mkuu nataka nikurekebishe kitu kimoja; Air craft Carrier ni tofauti na Destroyer. Popote ilipo Aircraft Carrier jua kuna destroyer tatu hadi nne na submarine moja zinazoisindikiza aircraft carrier. Hii ni kwasababu ya kuhakikisha usalama na ulinzi wa kutosha wa Nyambizi( Aircraft Carrier) ingawa yenyewe pia ina makombola ya kujilinda kutoshambuliwa na adui.
 
1477139521549.jpg
1477139534449.jpg
1477139534449.jpg
 
Back
Top Bottom