Meli iliyobeba malori 600 ya kiwanda cha Dangote yatia nanga Bandari ya Mtwara

mtotomtamuu

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
602
1,454
Hii ni fursa mpya kwa madereva
1481395206157.jpg
1481395213369.jpg
1481395221114.jpg

[Kazi kwenu madereva ajira hizoo!!q



View attachment 444946
View attachment 444947
View attachment 444948
View attachment 444965
View attachment 444966


Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote jana alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini.

Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini.

Aliongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.

Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.

Hapa chini ni picha ya meli hiyo ikiwa bandarini Mtwara.
 
Milion 150*600=??

Hesabu za fasta fasta!

HOWO?

Angechukua SCANIA/VOLVO!
Unangalia kitu kitakacho kupa faida na sio kitu kitakacho kupa heshima mtaani. Bei ya scania ni kubwa kulinganisha na howo na wakati gari zote zitafanya kazi ile ile. Spare za howo ni cheap ukilinganisha na scania. Kumbuk Dangote ni mfanya biashara



Jiulize kwanini wafanyabiashara wa mabasi wameacha kunua scan is kila mtu anakimbila youtong za kichina
 
Huyu jmaa anatisha cna hv mm ht bjji cna yy ananunua malor 600 hz kufuru cna
Hapa ndipo unaona tofauti katika matumizi ya akili.

- Nishauri vijana wenzangu wapunguze kidogo malumbano ya siasa humu, wakasome hata VETA ili wapate chochote maana tusijekujikuta kazi zotre zimeishia kwa wahindi na wakenya.Maana sisi kila siku humu ni kutukanana masuala ya siasa.
 
Back
Top Bottom