Meja jenerali (mstaafu) mwakitosi afariki: Lau masha alikuwapo

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

MAOFISA wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakibeba jeneza lenye mwili wa Meja Jenerali Mstaafu, Jumanne Mwakitosi, wakati wa mazishi yaliyofanyika leo, kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam. Meja Meja Jenerali Mwakitosi alifariki juzi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Wanajeshi wakilifikisha jeneza lenye mwili kwenye eneo la kaburi

Kisha mazishi kwa mujibu wa dini yake ya Kiislamu yakafanywa. Hapa wahusika wameingia kaburini tayari kuzika.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Abdulrahman Shimbo (kushoto) akiungana na waombolezaji wengine kuomba dua baada ya mazishi hayo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Tanga, Meja Jenerali Mstaafu, Saidi Kalembo.

Kisha JWTZ wakatoa heshima ya Kijeshi kwenye kaburi

Askari wa JWTZ wakirindimisha mizinga 13 kwa heshima ya kijeshi ya mazishi hayo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi (kushoto), Waziri wa Ulinzi Dk. Huseein Mwinyi na Waziri wa mambo ya Ndani wa zamani, Lawrence Kego Masha (kulia) walikuwepo kwenye mazishi hayo, bila shaka hapa walikuwa wakiteta jinsi Marehemu alivyokuwa mtu muhimu katika jamii. (Picha zote na Chachandudaily.blogspot.com).
 
No hiyo picha hapo chini ninaonesha Masha bado analalamika kushindwa Ubunge. Bado haamini mpaka leo kwamba alishindwa ubunge.
 


Binaadamu kaumbwa kwa udongo na anarejea udongoni. Hii dunia tunapita tu - tupendane.
Mola Amuweke Pahala Pema > Amin
 
Back
Top Bottom