Elections 2010 Media Watch: Mrema hajajiuzulu kugombea!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nimetoka kuzungumza sasa hivi na Mgombea wa Ubunge jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP Bw. Augustine Mrema ambaye amepinga vikali uvumi ulionezwa tangu jana jioni kuwa ameamua kuachia ngazi kwenye kinyang'anyiro hicho. Amesema kauli hizo ni mchezo mchafu tu wa kisiasa.

Kwa hiyo habari za kuwa Mrema amejiuzulu hazina ukweli wowote. Anawataka mashabiki wake na wapenzi kuendelea kumuunga mkono kwani bado hajasalimu amri na hana mpango huo.
 
Naona kama kuna fuka Moshi huko Vunjo. Ila huyu 'mzee', misimamo yake tata sana, historia inaonyesha hivyo!
 
Hata kama amekanusha lakini haweze kupata ubunge kule tena. Hana mvuto kisiasa kabisa kule vunjo na popote Tanzania. Arudi tu CCM aendelee na pension yake tiss na chama.
 
Kwanini hawa watu wanaotangaza kwenye majukwaa au kutumia magari ya matangazo kwamba mtu fulani kajitoa wasichukuliwe hatua Kali? nadhani next time Tume ya uchaguzi ipige marufuku huu mchezo na badala yake yenyewe pekee iwe na mamlka ya kutangaza kwamba mgombea fulani kajitoa.
 
Hata kama amekanusha lakini haweze kupata ubunge kule tena. Hana mvuto kisiasa kabisa kule vunjo na popote Tanzania. Arudi tu CCM aendelee na pension yake tiss na chama.

Bado anapendwa sana na kina mama wengi kule kiraracha, atatoa ushindani mkali kwa yeyote atakayeshinda i.e. CCM au CHADEMA
 
CHADEMA acheni uzushi kila sehemu. Mara karatasi za kura, mara kule Arusha yule mama sijui kaenda kujifungua USA. Hivi kwanini mnataka kuwadanganya Watanzania?

Mwacheni Mrema achukue jimbo la Vunjo kwani ana uwezo wa utendaji kuliko hao wagombea wengine.
 
Mwacheni Mrema achukue jimbo la Vunjo kwani ana uwezo wa utendaji kuliko hao wagombea wengine.

Acha Mrema aonyeshwe kazi na CCM maana ni kiherehere chake kimemfikisha huko..........Yeye kweli angelikuwa mwanamageuzi kamwe asingelimpigia debe Jk na kumwacha mgombea wake wa TLP mkiwa..............Mgombea CCM wa Vunjo wa Ubunge ndiyo amemzulia hili janga. Sasa apime uhusiano wake na Chama hiki cha Mafisadi
 
CHADEMA acheni uzushi kila sehemu. Mara karatasi za kura, mara kule Arusha yule mama sijui kaenda kujifungua USA. Hivi kwanini mnataka kuwadanganya Watanzania?

Mwacheni Mrema achukue jimbo la Vunjo kwani ana uwezo wa utendaji kuliko hao wagombea wengine.

Kweli nimeamini hakuna dini isiyo na mfuasi, yaani bado kuna watu mnasema Mrema ni kiongozi bora kiutendaji! Baada ya huyu mzee kupitia misukosuko (NCCR &TLP) mingi nadhani tabia, mienendo na utendaji wake wa ukweli umeonekana wazi. kama ni kiongozi bora, kama ni mwanademokrasia au Ditkteta truth is naked
 
CHADEMA acheni uzushi kila sehemu. Mara karatasi za kura, mara kule Arusha yule mama sijui kaenda kujifungua USA. Hivi kwanini mnataka kuwadanganya Watanzania?

Mwacheni Mrema achukue jimbo la Vunjo kwani ana uwezo wa utendaji kuliko hao wagombea wengine.
The problem si Chadema wanazusha ila ni upumbavu wa wale mnaoukubali uzushi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom