Mdogo wa Rostam Aziz aachiliwa huru

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Na Happiness Katabazi

Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imemwachilia huru mdogo wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga (CCM), Rostam Aziz, Assad Aziz Abdulrasul, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kula njama na kuingiza dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 92. 2 ambazo zina thamani ya sh bilioni 2.4 baada ya kumuona hana kesi ya kujibu.

Abdulrasul katika kesi namba 19B ya mwaka 2011 alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ya kula njama na kusafirisha kiasi hicho cha dawa za kulevya aina ya heroine na alikuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza.

Washtakiwa wengine ni Kileo Bakari Kileo, Yahaya Zumo Makame, Mohammadal Gholamghader Pourdad na Saidi Ibrahim Hamis.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Kipenka Mussa, aliyesema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, ushahidi ulitolewa na mashahidi 200 na vielelezo 25 vya upande wa jamhuri, mahakama hiyo imeona ushahidi na vielelezo hivyo havithibitishi mshtakiwa wa saba (Abdulrasul) kuwa alitenda makosa hayo mawili aliyoshtakiwa nayo.

Jaji Kipenka alisema ushahidi na vielelezo vyote umeweza kuishawishi mahakama iwaone washtakiwa waliosalia kuwa wana kesi ya kujibu.

"Kwa sababu hiyo mahakama hii inamuachilia huru mshtakiwa wa saba (Abdulrasul) kwa sababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yake ila kwa washtakiwa wengine waliobakia katika mahakama hii imewaona wana kesi ya kujibu hivyo watatakiwa wapande kizimbani wajitetee katika tarehe itakayopangwa na mahakama hii," alisema Jaji Kipenka.

Mapema 2011 ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikula njama kusafirisha dawa za kulevya kinyume na kifungu cha 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 22(a) and 25 cha Sheria ya Dawa za Kulevya.

Kuwa washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Aprili Mosi na Machi 8 mwaka 2009 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, Tanga na Jamhuri ya Iran ,washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama kusafirisha dawa hizo na kosa la pili ni ni la kukutwa na dawa hizo Machi 8, 2010 huko kijiji cha Kabuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 16(1)(b)(1) cha Sheria ya Dawa za Kulevya.

Polisi yakamata wawili Dar, Polisi wakishirikiana na watumishi wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wamewakamata watu wawili akiwemo raia wa Ghana, Emanuella Adom (51), wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam jana.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ambaye ni mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya Tanzania Godfrey Nzowa alisema Adom alikamatwa jana saa kumi usiku akitaka kuelekea Accra Ghana kwa kutumia ndege aina ya KQ akiwa na hati ya kusafiria namba G0084666 iliyotolewa February 8, 2011.

Nzowa alisema walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kumfuatilia na kumkuta na paketi 2 zenye uzito wa kilo 3 za heroin ambazo alikuwa amezihifadhi katika mabegi yake mawili ya kuhifadhia nguo.

Nzowa alisema kuwa Mei 2, mwaka huu, polisi walimkamata mtuhumiwa mwanamke Mary Mvula, raia wa Zambia akiwa na dawa za kulevya aina ya heroin akitokea Pakistan kupitia Dubai, Addis Ababa na hatimaye kukamatwa uwanja wa ndege wa hapa nchini.

Alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa amemeza dawa hizo na kujisingizia kuwa ana ujauzito, lakini baada ya uchunguzi ilibainika kuwa ni dawa na kufanikiwa kutoa kete 49 za dawa hizo.

Nzowa alisema jeshi la polisi limejipanga vyema katika mipaka yote, bandarini pamoja na viwanja vyote vya ndege kuhakikisha wanadhibiti uingizwaji na utoaji wa dawa hizi haramu.

Hata hivyo jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa vituo vyote vya polisi vilivyopo karibu nao kama wanafahamu viongozi, watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara haramu ili waweze kuchukuliwa hatua.


SOURCE: Tanzania Daima
 
Kila aina ya Kesi hapa nchini basi inasamehewa,inakera sana.
 
nimeiona hii habari kwenye website ya Tanzania Daima nikadhani labda sio kweli na walikuwa hawaja-update.
ama kweli nchi hii ina wenyewe na kibaya zaidi hawa wenzetu sio wakaaji hapa na wala hawataathirika na matatizo wanayotusababishia.

yaani wanatutumia tu kama zile bidhaa zinazotangazwa na PSI kwa ajili ya kupammabana na gonjwa hatari la UKIMWI! Hapa wakuu bila kufanya utaratibu wa vetting ya majaji/mahakinu (wafanyakazi wa umma) kama inavyoendelea Kenya sasa, sijui nini kitatokea.
 
China angenyongwa.. ILe kesi ya Mtoto wa Liyumba na Kontena la madawa ya kulevya Mbona Kimyaa??
 
angekuwa mdogo wake na slaa,mbowe au lema sheria ingepindishwa na angehukumiwa kunyongwa mpaka kufa
 
kilicho cha kushangaza kila siku tunapata taarifa za waliokamatwa na dawa za kupunguza akili/hekima lakini ni nadra na tena sijasikia nani kafungwa jela.Si ajabu walioonwa na hatia ni porters tu maskini yarabi na wataishia maisha yao yote jela:That is the LAW,too strong for the WEAK and too weak for the STRONG
 
Majajaji wa Bongo siwaamini kabisa!!
Kushindwa au kushinda kesi itategemea unafahamiana vipi na jaji
 
FEDHA NA SHERIA KIPI KIKO JUUU?????
WANAOTUNGA SHERIA WANATAKA FEDHA
NA WANAOVUNJA SHERIA WANATAKA FEDHA!!:hat::hat::hat:

NA WANAOSIMAMIA SHERA WANATAKA FEDHA!!!:israel::israel::israel:
 
Wale waliokamatwa kiwanda cha madawa na aliyekua pm sumaye maeneo kunduchi iliishia wapi?
 
Jamani, jamani jamani.... tumekwisha. Huyu jamaa alikutwa kwenye gari lililokuwa na mzigo, Kipenka alihitaji ushahidi gani mwingine wa kumhusisha na mzigo huo? Ingekuwa ameombe lift tungesema kuwa hakujua gari lilikuwa linasafirisha nini, lakini.... Oh! we acha tu.
Hivi baada ya mambo kama haya serikali bado inaweza kuwa na guts za kuwataka wananchi washiriki kwenye vita dhidi ya dawa za kuilevya na wakaielewa?
 
Majajaji wa Bongo siwaamini kabisa!!
Kushindwa au kushinda kesi itategemea unafahamiana vipi na jaji

Mara nyingine (na mara nyingi) sio ma-jaji. Waendesha mashtaka wa serikali (ambao wana mshahara kiduchu) wanaweza kuendesha mashtaka kwa namna ambayo wanajua kabisa hakimu au jaji atakuona huna hatia. Hili watu wengi sana, kutia ndani na Takukuru, hawajaliangalia kwa makini.

Kama walishikwa red handed basi inaonekana Rostam alitumia akili akacheza tu na waendesha mashtaka wa serikali wayakoroge mashtaka.
 
Na wewe miongoni mwa hizo sehemu? Uwa inasemwa/inasemekana mawakili wa Serikali siku hizi wanalipwa mishahara mizuri sasa unaposema wanalipwa kiduchu kwahiyo ni kichocheo cha kuharibu kesi sijui kama ni kweli.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom