Mdau mwenzetu W. Malecela anapodhalilishwa na vyombo vya habari tumsaidiaje

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884

MTOTO.jpg

Na Sifael Paul
WILLIAM Malecela a.k.a Le Mutuz ambaye anatajwa kuwa ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe Bongo, John Malecela ambaye anadaiwa kuwa ni funga kazi kwa kupenda kupiga picha na wanawake wazuri kila anapokuwa, Amani limemfuatilia hatua kwa hatua na sasa linafunguka.
Kwa mujibu wa ‘mapicha' yake mazuri yaliyopo mitandaoni, asilimia 90 zinamuonesha Le Mutuz akiwa na wanawake wazuri wa kada mbalimbali.

WAMO MASTAA

Mbali na wanasiasa wenzake, Le Mutuz aliyegombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa leseni ya CCM hivi karibuni lakini kura hazikutosha, anaonekana kwenye picha nyingi zisizo na idadi akiwa na mastaa mbalimbali wakiwemo waigizaji na wanamuziki wenye majina makubwa Bongo.​

NI KILA MAHALI?

Katika picha hizo, Le Mutuz anaonekana akiwa sehemu mbalimbali hasa kwenye kumbi za starehe, baa, migahawani, viwanjani, nyumbani na ufukweni, vyote jijini Dar es Salaam.​

ETI NI MAMBO YA ‘KUTOKLEZEA'

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Le Mutuz, jamaa huyo mwenye ‘sivii' ya kuishi nchini Marekani kwa muda mrefu amekuwa akiwakaribisha warembo hao kwenye mtandao wake (jina tunalo) kwa kutundika picha hizo na kuwataka waingie humo kujiona ‘walivyotoklezea'.​

BAADHI YA MASTAA NI HAWA

Baadhi ya mastaa wanaoonekana na ‘mutu mukubwa' huyo na kusababisha minong'ono kwa kuwa zina mapozi tata ni pamoja na Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Masawe, Jokate Mwegelo, Miss Tanzania 2011, Salha Israel, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee' na warembo wengine ‘kibwena' wasiokuwa na majina.​

WAMO MARAFIKI WA FACEBOOK

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, inaelezwa kuwa, Le Mutuz huwa anawasiliana na warembo ambao ni marafiki zake katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo hukutana nao na kupiga picha ili kuziweka mtandaoni kwake.​

MSHANGAO!

Kwa mujibu wa maoni ya watu wanaotembelea mtandao wake wanashangazwa na ishu hiyo huku wakihoji mbona anafanya na mademu tu, tena wazuri?​

LENGO NI NINI?

Ili kupata undani wa kwa nini Le Mutuz anafanya hivyo, Amani lilifanya jitihada za kupata kupitia kilongalonga chake cha kiganjani lakini hakupatika, hata hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

Wadau wengi hapa JF tunamfahamu kutosha William Malecela kwa michango mizuri na kuleta mada za udadisi katika kujenga jamii yetu. Ni mdau mwenzetu na ni mmja kati ya wadau wa mwanzoni kabisa waliojitahidi kuchangia mada mbalimbali hapa Jamii forums.

Uvumilivu wake katika kujadili mada pamoja na kuonyesha ustahimilivu hata tunapomkosoa au kuwa kinyume cha itikadi anazoamini ambayo ni haki yake ya free speach ni funzo tosha wangu na kwa wengi.

Kilichonishtua ni Gazeti moja hilo pichani kuweka habari ambazo sidhani kama yeye binafsi zitamfurahisha pamoja na familia yake. Kwa walio karibu naye wajaribu kumpa moyo na subira kwani maisha ni safari na binadamu ni kinyonga, kwani akiwa na sikio sikivu ipo siku magazeti haya haya yataandika mazuri tu juu yake.

Tukumbuke ameshapata nafasi kadhaa katika Chama cha Mapinduzi kuwa mwakilishi na vyeo vingine na bado anatarajia kupanda taratibu, mambo kama haya nisingefurahia kutokea kwake kwani yanaweza kuwa kihuzi katika kupanda hatua nyingine zaidi kufikia matarajio yake. Papo kulinda heshima ya jna la Malecela John.
 
we agent wake nini? yeye mwenyewe anafurahia, angalia post zake za nyuma akijisifia kupiga picha na warembo na kula maisha.
 
MTOTO.jpg
Wadau wengi hapa JF tunamfahamu kutosha William Malecela kwa michango mizuri na kuleta mada za udadisi katika kujenga jamii yetu. Ni mdau mwenzetu na ni mmja kati ya wadau wa mwanzoni kabisa waliojitahidi kuchangia mada mbalimbali hapa Jamii forums.

Uvumilivu wake katika kujadili mada pamoja na kuonyesha ustahimilivu hata tunapomkosoa au kuwa kinyume cha itikadi anazoamini ambayo ni haki yake ya free speach ni funzo tosha wangu na kwa wengi.

Kilichonishtua ni Gazeti moja hilo pichani kuweka habari ambazo sidhani kama yeye binafsi zitamfurahisha pamoja na familia yake. Kwa walio karibu naye wajaribu kumpa moyo na subira kwani maisha ni safari na binadamu ni kinyonga, kwani akiwa na sikio sikivu ipo siku magazeti haya haya yataandika mazuri tu juu yake.

Tukumbuke ameshapata nafasi kadhaa katika Chama cha Mapinduzi kuwa mwakilishi na vyeo vingine na bado anatarajia kupanda taratibu, mambo kama haya nisingefurahia kutokea kwake kwani yanaweza kuwa kihuzi katika kupanda hatua nyingine zaidi kufikia matarajio yake. Papo kulinda heshima ya jna la Malecela John.

Una muonea huruma? Kayataka mwenyewe. Anapenda kuuza sura sana huyo.
 
Sijapenda jinsi wanavyojaribu kumuita 'mtoto wa Malecela'

wakati ni mtu mzima mwenye mambo yake

na ameshajitambulisha yeye mwenyewe kwa activities zake

sasa kum link na baba yake kwa kila analofanya ni kutowatendea haki wote wawili
 
Ni maisha aliyoamua kuishi, sasa hapo kuna tatizo gani??
Ila mimi kama mtanzania nisingependa awe kiongozi wangu wa ngazi yeyote.
Nisingependa awe shemeji yangu .... he seems to be irresponsible, like a lil teenage boy.
 
Samahani sijaelewa kidogo
Hapo kinacholalamikiwa ni nini?
Kwani hizo sio picha zake?
 
Kwani siyo mtoto wa Malecela? Yeye mwenyewe anajiita William John Samwel Malecela....hapo anatumia majina yote matatu ya baba'ake na lililokosekana ni Cigwiyemisi tu.

Ukimuita mtu 'William John Malecela'

sio sawa na kumuita 'mtoto wa Malecela'

kwa mfano umeenda hospitali kauliza dokta ni nani?
watakujibu dokta ni 'Wiliam John Malecela'

hawatakujibu dokta ni 'mtoto wa Malecela'

ina tofauti kubwa sana
 
Kwani siyo mtoto wa Malecela? Yeye mwenyewe anajiita William John Samwel Malecela....hapo anatumia majina yote matatu ya baba'ake na lililokosekana ni Cigwiyemisi tu.
Na kubwa zaidi anakaa kwa Baba yake Upanga Seaview, na mnaweza kushangaa akaibuka hapa na kufurahia hilo gazeti lilivyomtoa na anaweza kuanza kusema huo ndio Ubig Celeb.
 
Ukimuita mtu 'William John Malecela'

sio sawa na kumuita 'mtoto wa Malecela'

kwa mfano umeenda hospitali kauliza dokta ni nani?
watakujibu dokta ni 'Wiliam John Malecela'

hawatakujibu dokta ni 'mtoto wa Malecela'

ina tofauti kubwa sana

Context is everything!

Hospitalini huendi kutafuta information. Most likely unaenda kupata matibabu.

Gazeti, moja ya kazi zake ni kuprovide information. Ukiishia kuandika tu William Malecela watu watajiuliza...does he have any relation with John Malecela? Kwa kuandika ni mtoto wa Malecela tayari unakuwa umeshakidhi kiu ya watu ambao wangejiuliza hilo swali.

Hebu ona hiki kipande kuhusu Chelsea Clinton....

She's made headlines before as the daughter of a former U.S. president – and as a glowing newlywed.

But now Chelsea Clinton will sit on the other side of the news desk.

The daughter of Secretary of State Hillary Clinton and Bill Clinton will begin working as a fulltime special correspondent for NBC News on Monday, The New York Times reports. Source

Jenna Bush
NEW YORK - NBC's "Today" show has hired someone with White House experience as a new correspondent – former first daughter Jenna Hager.
The daughter of former President George W. Bush will contribute stories about once a month on issues like education to television's top-rated morning news show, said Jim Bell, its executive producer. Source
 
Sasa unatakaje?
1. Hizo picha kapiga mwenyewe, na mtandaoni kaweka mwenyewe
2. Yeye kama yeye anapenda picha zake, ndio maana kaziweka mtandaoni
3. Nani kakwambia kua anahisi kadhalilishwa? Au wewe umeongea nae?
4. Unafikiri tungemsaidiaje mfano? tususe kununua gazeti hilo? tuwashtaki?
5. Mwenyewe W. J. Malecela kasemaje? Mbona kachukulia poa tu?
 
Ingia kwenye link hii post # 156 mtayapa majibu ya William short & clear wala msipote muda wenu.
William Malecela na Ajali za Kisiasa
 
LE MUTUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUZ,LE BAHARIAAAAAAA ,BAHARINI HAMNA TOTOZIIII LAZIMA AKOLEE NA SURA HIZO CHEZEAAA BONGO WEWE

ILA HILI JMABO LIKO MAHAKAMANI MSIJADILI TAFADhALI
 
Yaani yeye ndo kafanya hayo afu mnavilaumu vyombo vya habari! JE WALIMKAMATA WAKAMLETEA HAO MABINTI WAKAMUWEKEA BASTOLA KICHWANI KISHA WKAMLAZIMISHA ATABASAMU WAKAMPIGA PICHA!!???????, AU HIZO PICHA ZAKE WAMEZIPATAJE????
 
Back
Top Bottom