Kudadeki
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 859
- 52
Kwa waliofuatilia ule mjadala wa wagombea vijana hivi LIMBU LUKAS - CUF Hivi huyu Jamaa naye ni KIJANA? Maana nahisi anaweza kumzaa Mnyika,
Tafsiri yako ya kijana ni nini? :confused2:
Kwa waliofuatilia ule mjadala wa wagombea vijana hivi LIMBU LUKAS - CUF Hivi huyu Jamaa naye ni KIJANA? Maana nahisi anaweza kumzaa Mnyika,
Nilichopost mimi na ulichonijibu haviendani.Mimi nilikuwa nina mwambia Kudadeki achane na siasa za ukabila,wewe umenirukia na kuongelea kitu kingine.We sijui ndo Kudadeki, whoever the hell you, are jenga hoja! Myika ni mgombea ubunge kupitia CHADEMA aliyetokea kwa na kabila kama ulivyo wewe..
Wewe umejificha nyuma ya siasa za udini na ukabila,siasa za chuku. Zaidi ya hapo hauna hoja.Na wewe utabaki hivyo hivyo bila ya hoja. :smile-big:
Kwenye mkutano wa kampeni ndiyo una muda mwingi wa kupiga soga na kuifafanua sera ya chama chako. Kwenye mdahalo una restriction ya muda and you have to answer the question within the given time limit. Nitakupa mfano wa swali la elimu. Muongeaji wa CUF alienda straight to the point kuwa from chekechea to chuo kikuu, elimu itakuwa bure chini ya uongozi wa Prof. Lipumba. Yule muongeaji wa Chadema akaanza kutoa maelezo ya taaluma ya ualimu kuachwa nyuma na sijui kudharauliwa, matokeo yake muda ukaisha na kashindwa kujibu swali.
Tafsiri yako ya kijana ni nini? :confused2:
Acha uongo wako wa kujifanya wewe CCM. Ule ulikuwa mdahalo, unatakiwa kuonyesha uwezo wa kujibu maswali haraka na kwa muda uliowekewa. Ule ilikuwa siyo RTD ya Nyerere aliyekuwa anaongea masaa 3 mfululizo bila ya kuzingatia muda na kubaki kuchekacheka.
Wazungumzaji wa CHADEMA walibaki kujisifia kuwa wao ndiyo wamefanya hivi na wao ndiyo wamefanya vile kwenye bunge. Yaani watu 11 wanaweza kutufanya sisi tuamini kuwa ndiyo waliopitisha sheria mpya ya madini? Swali la vipi mtapiga vita na kuondoa kero ya ufisadi, jibu linaanza kuelezea historia ya bunge liliopita matokeo yake swali halijibiwi na muda unaisha. Ukiulizwa 1+1 ni ngapi na una muda mdogo wa kujibu na ukaanza kueleza kuna robo ngapi kwenye hiyo moja na kuna nusu ngapi kwenye kila moja ya hiyo moja, hayo ni matatizo ya wazungumzaji wenu. Wakulaumiwa siyo wazungumzaji wa CUF!
Utaendelea kujifunza huku roho ikikuuma. Ila ushauri wa bure usije ukajiua tu wakati wa matokeo ya uchaguzi yatakapoanza kutoka baada ya uchaguzi. :becky: