Mdahalo wa katiba balaa, ITV kufungiwa?

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
Habari za kutoka ndani ya Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) nilikokua leo, zinasema kwamba tume hiyo imeitaka ITV kujitetea kwanini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kuonyesha LIVE mdahalo wa katiba uliohusisha wanaharakati na wanasheria wa Jukwaa la Katiba.
 
Wapuuzi hawa!!

Sheria zao zinakataza mijadala ya katiba isionyeshwe live? au isionyeshwe? au isiwafikie wananchi?

Makenge hawa!!!!
 
Kwa nini wajitetee sasa kwani ni mara ya kwanza walianza kuonyesha midahalo ya Rosemary mwakitwange na Tanzania tunayoitaka
Wanaonyesha midahalo ya waalimu wa chuo kikuu,wana kipindi cha Marumbano ya hoja sema usikike nakadhalika.

wapuuzi hao TCRA warudishe fedha bilioni 5 walizoiba kusomesha watu wawili kwanza, ITV ni kati ya major power house hapa nchini kuigusa lazima ujiandae sana wanaweza kufungia magazeti kama walivyofungia alasiri, kasheshe lakini sio ITV na wakatoka salama
 
Pumbavu kabisa hawa tisiiaraei.
Tumepandishiwa gharama za simu kinyemela karibu mara 3 zaidi wao wamekaa kimya.
Makampuni ya simu, hasa tigo yanatuibia pesa zetu hata kama hatujatumia huduma yoyote wao wamekaa kimya.

Hilo la mdahalo wa katiba lina ubaya gani.
 
tunavyoendelea kuchokonoa ndivyo ubaya na unafiki wa ccm unajidhihilisha kwa mwamvuli wa utawala bora na uhuru wa vyombo vya habari.
 
Hawa si ndo walitumia zaidi ya 700mil kusomesha mtu mmoja
Nyambafu kabsaa badala ya kudeal na mambo ya msingi kama voda wanavyomis use namba zetu.
Ila mtoa mada itabidi star tv nao wafungiwe walionesha pia
 
Hii ilianzia bungeni jana. Na TCRA hawajui hata wajibu wao kisheria. Hata kusimamia usajili wa simu wameshindwa!
 
mkwara tu mmiliki anamchango mkubwa sana ndani ya CCM,na hata hivyo nilishasema humu jukwaani ya kwamba Lusinde wote wa CCM walishapata laana kwa kudhulumu haki za watu,kukandamiza demokrasia na hata kwa kuitikia ndioooo ili mradi tu jambo fulani lipite kwa manufaa ya magamba,sasa kama wamekurupuka hao TCRA basi watazidi kujivua nguo juu ya suala la Katiba na kila mtu ataona uozo wao na jinsi wanavyo-force mswaada huu ili uje utengeneze katiba ya CCM na wala sio ya wa TZ
 
Taratiiibu tutakomboka wala msijali wadau na hawa wawe kwenye lile kundi mara tupatapo uhuru wetu
 
ni sawa na kuingilia uhuru wa habari
TCRA hawana mamlaka yaho, chombo cha habari kinapaswa kuwa huru ili mradi wasivunje sheria za nchi
sasa walitaka wananchi wasipate habari kwa kuwa wanajadili katiba? TCRA kama National Regulatory Authority kama wakithubutu kufanya hivo watakuwa wanafanya kazi kisasa badala ya kutekeleza majukumu yao.zipi sheria za kimataifa zinazohusu mawasiliano na tanzania ni signatory wake hapo watakuwa wamekwenda kinyume na ITV watakuwa na haki kuwaishtaki endapo watathubutu kufanya hivo
ITV msiogope wanasheria tupo
 
TCRA na yenyewe inajiingiza kwenye siasa?
Fuatilia uteuzi wa wakuu wa TCRA ndiyo utagundua kwanini tunataka katiba mpya. Usitegemee mimi nikuteue alafu usinikingie kifua kwa maswala yaliyo ndani ya uwezo wako, si nakupiga chini tuu?
 
TCRA HAIWEZI KUIFUNGIA ITV,KAMA WATAJARIBU WATAUONA MOTO SISI NDIO TULIOOMBA ITV NA TUMEILIPA KWA HIYO ITV ILIKUWA INAFANYA BIASHARA NA SIO SIASA

WAO WAENDELEE KUIBEBA TBC KWA KUIPA RUZUKU NA KUIRUHUSU ICHUKUE MATANGAZO YA ITV MWISHO WAO UNAKUJa
 
Back
Top Bottom