Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Dr anaendelea kutoa ufafanuzi wa suala la rasilimali ambalo pia kitakuwa sehemu ya mabadiliko. Hapa kuna rasilimali:
watu
ardhi
maji na vilivyomo kama samaki,
madini
mifugo
mabonde yafaayo kwa kilimo ili hali taifa lina agiza chakula.
Rasilimali za tz lazima zimnufaishe mtz kwanza. Win win situation mtz anufaike na mwekezaji anufaike, lakini mtz zaidi
 
Swala la Rasilimali. Tanzania ina Rasilimali nyingi. Watu, Ardhi, Maji, Maziwa, mito, bahari, samaki, madini, mabonde ya kilimo. Rasilimali hizi hazitumiki vizuri kumnufaisha mwananchi. Hataki wawakazaji holela. win win situation.
 
Pia anasema hoja wa Raslimali kuwanufaisha watanzania haina maana kwamba wawekezaji hawatakiwim, la hasha, cha muhimu ni balance ili wawekezaji wanufaike pamoja na Watanzania, ila priority watanzania
 
Suala la rasilimali ni msingi mkubwa wa mabadiliko tunayotarajiwa kufanya , katika suala hili tanzania imebarikiwa na rasilimali nyingi kama watu , ardhi , maji na mengine mengi sana .

Rasilimali zilizopo lazima zimnufaishe mtanzania lakini haimaanishi wawekezaji wasiwepo , tunatafuta win win situation
 
hana mpya huyu labda tusubiri atazusha uzushi gani saa hii maana jamaaa kwa kuropokwa huyu

amesema hatachagua mawaziri kwa vigezo vya uswahiba au kufahamiana......na ataweka waziri mwenye vigezo kwenye wizara husika.....sio mhandisi anawekwa wizara ya afya n.k
 
Nami pia namsikiliza. Maswali anayouliza Dada Rose Mwakitwange yana mantiki sana na Rais Mtarajiwa anayajibu vizuri sana.
 
anazungumzia rasimali zetu na zinamnufaisha mtz .chadema ilani yake inasema rasimali zilizopo lazima zimnufaishe mtanzania na kuingia win win situatin.waku wanapiga makofi. dr kweli ametulia. sasa suala la makazi /ardhi .tatizo kubwa ni rushwa na kutokawa waamuzi na ufisadi. mgogoro wa wakulima na wafugaji ni kutokana na serikali isiyo makini.
 
Ameulizwa swali
Atasaidiaje kutokana na migogoro ya Aridhi mingi iliyopo,

Anasema, matatizo mengi ni kutokana na watendaji ambao wanaendekeza Rushwa, kwa mfano ufisadi ni mwingi sana na unasababisha migogoro,
Mfano , mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ni migogoro inayotokana na uzembe wa serkali, mfano wafugaji wa ‘barbari ' waliondolewa na serikali kwenye maeneo yao. Wakaachia, lakini serikali haikuwapatia mahali pa kwenda, serikali makini ni ile ambayo inamuondoa mfugaji alipo na kumepeleka mahala pengine pazuri.

Tatizo ni serikali kukosa umakini, wamelalamika sana hakuna anayewasilikiza, amesema pia wafugaji Wasukuma wanamatatizo yahoo hayo, na serikali haiwasaidii
 
Ameulizwa swali
Atasaidiaje kutokana na migogoro ya Aridhi mingi iliyopo,

Anasema, matatizo mengi ni kutokana na watendaji ambao wanaendekeza Rushwa, kwa mfano ufisadi ni mwingi sana na unasababisha migogoro,
Mfano , mgogoro kati ya wakulima na wafugaji ni migogoro inayotokana na uzembe wa serkali, mfano wafugaji wa ‘barbari ‘ waliondolewa na serikali kwenye maeneo yao. Wakaachia, lakini serikali haikuwapatia mahali pa kwenda, serikali makini ni ile ambayo inamuondoa mfugaji alipo na kumepeleka mahala pengine pazuri.

Tatizo ni serikali kukosa umakini, wamelalamika sana hakuna anayewasilikiza, amesema pia wafugaji Wasukuma wanamatatizo yahoo hayo, na serikali haiwasaidii
 
watu wanatoa machözi kwa hamasa wanazipata .anakatishwa na makofi.ukumbi umetulia kama wananyolewa. anataka kurekebisha utendaji wa watendaji wa serikali.
 
Anaongea matatizo ya ardhi. Wafugaji wanaondolewa lakini hawapatiwi eneo lingine.Hili ni jukumu la serikali, lakini serikali imejaa rushwa na haisimamii jukumu lake. Wafugaji lazima wapatiwe huduma muhimu na watendaji hawana maadili, wana ubinafsi sana.
 
Serikali ya chadema therefore, itasimamia kwa makini haki za watanzania wote na kuwasaidia kwa kile wanachohitaji. Na kwa kufanya hivyo migogoro haitakuwawepo, hii itaendana na kuwasimamia watendaji.
Anasema , usukumani amekuta kitu cha ajabu, watendaji wanawaambia wafugaji usiponi pa ngombe dume nitakubambikizia kesi ya mauaji…
 
matatizo ya nyumba za wafanyakazi,watanzania hawaijui nchi yao vizuri,umaskini umwigubika tanzania haswahaswa vijijini na wengine wanalala kwenye ngozi ya ng'ombe duh hapa dk slaa amenena kweli
 
Back
Top Bottom