Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

anazungumzid madaraka makubwa ya rais na matumizi mabaya anatoa mfano wa baraza la mawaziri 60 kwamba ilikula pesa ya walipa kodi
 
Nipo hapa kando ya TV kwa kweli naomba umeme usikatike.

mnafaidi peke yenu tu, tupeni link nasi tujionee au hata sauti tupate yanayojiri jamani. Hyuy Dr ni mtu muhimu sana hivyo tunahitaji kujua kila kinachoendelea live kama nyie huko.
 
Dr. anaongelea habari ya uendeshaji wa serkali

Kwamba kuna watu wako serkalini lakini hawaelewi vizuri majukumu yao,

Mfano manaibu waziri kazi zao ni kujibu tu maswali Bungeni, nje ya hapo hawana kazi kubwa ya kufanya, sasa anasema hawahitajiki ili kuokoa pesa hizo zitumike kwenye maswala mengine ya kijamii

kwamba, serikali ya chadema itakuwa na baraza dogo lenye matumizi madogo kwa maslahi ya taifa

anapata makofi mengi sana
 
Hakuna uwajibikaji na madhara ya nchi. katiba yetu haiko wazi na antaka kuweka mambo vizuri . Rais ndia anateua mawaziri. Rasilimali zintumika ovyo. kodi inatumika katika utawala. mawaziri 60. mishahara ya maposho. mawaziri kazi yao kujibu bunge tuu badala ya hizo pesa kuendeleza. atafanya serikali ndogo na yenye kuwajibika.
 
dr wa ukweli anashusha nondo .ametulia na ukumbi uko kimya .ameanza na mabadiliko ya katiba hasa madaraka ya rais.
<br />
<br /:Hakika huyu bw ni kichwa kweli kweli, nina katiba mkononi anatoa vifungu kama jinsi vilivyo ndani ya katiba.
 
Tutakuwa na serikali ndogo yenye tija na uwajibikaji , ni fedha nyingi zitaokelewa kupelekwa kwenye huduma za maendeleo ya wananchi - kwa maslahi ya taifa , tutaacha ubinafsi na kueleza zaidi maslahi ya taifa

Kwa hatua ya awali mawaziri watapatikana kutokana na wabunge lakini baada ya kubadilisha katiba mawaziri watatoka kutoka nje ya bunge ili kuleta uwajibikaji na tija kwa taifa
 
Swali la jinsi atakavyo pata mawaziri,

Dokta anaelezea kuwa baada ya mabadiliko ya katiba, mawaziri hawatatokana na Wabunge, watu watachaguliwa kulingana na profession zao

kwamba hakuna tija kama waziri anatokana na uteuzi wa kiurafiki, hilo atabadilisha kabisa kupata viongozi wenye ubunifu, wenye tija n.k
 
Mawaziri watatoka nje ya bunge. Hili litaondoa uteuzi kwa uswahiba na kufahamiana. Hakuna tija. Tunakosa viongozi waadilifu.
 
mnafaidi peke yenu tu, tupeni link nasi tujionee au hata sauti tupate yanayojiri jamani. Hyuy Dr ni mtu muhimu sana hivyo tunahitaji kujua kila kinachoendelea live kama nyie huko.

Jaribu TV4Africa ila utalipishwa kiasi kidogo ambacho ni chini ya euro 6.
 
Tayar ameweza kuchambua ki2 kikubwa. utawala au muundo wa serikali. ebu niambie ww umeona nini mpaka sasa
 
Masuala yatakayo jadiliwa leo ni kama yafuatayo

- Makazi
- rasilimali
- mfumo wa kodi
- maslahi ya wafanyakazi
- suala la uwajibikaji
- jumuiya ya afrika mashariki
Mkuu endelea kutuhabarisha
kuna dalili pia watu wa network wanaweza kukata mawasiliano ya internet au kupunguza nguvu za coverage.
Dalili nimeanza kuziona. CCm wamejazana kila kona
 
Swali sijalipata vizuri kwa kuwa TV ilileta tatizo la kelele kidogo

Ila majibu ni kuwa,

Tanzania ina raslimali nyingi sana, Maji, samaki, .... anatoa mfano kuwa Watanzania wanakula mapanki wakati kuna samaki kibao,

pia anaongelea raslimali madini na mabonde mengi ambayo tanzania inayo, wakati huo huo inaagiza chakula nje, kitu ambacho si sahihi na hatakivumilia hata kidogo,

Raslimali za Tanzania lazima ziwanufaishe watanzania
 
ilani ya chadema ktumia rasilimali za nchi kumfaidisha mwananchi
 
Back
Top Bottom