Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Kaanza kwa kushukuru jinsi watanzania walivyompokea ktk mikutano ya kampeni kote alikotembela.
 
Kaanza kumwaga sera, mwenyekiti ni Rose Mwakitwange.

Anasema imebaki mikoa mitatu kumalizia kampeni.

Katika hotuba zake amesema anakwenda kufanya mabadiliko makubwa tofauti na mazoea.

Anaanza na msingi wa uendeshaji wa nchi ambao ni mabadiliko ya katiba
 
Wakuu tukutane kwenye jukwaa la dr. slaa live naamini sisi tusio na umeme tutahabarishwa kinachojiri kule.

Huku kwetu hamna umeme umeshakatwa dk 30 zilizopita
 
Sasa mtu wetu tupo mbali na nchi uku asia na redio ambayo ipo online ni redio maria na hawarushi hewani na hakuna tv za bongo on line kama vipi tuhabalishe kil baada ya mda nini chaendelea
 
Ameanza kuongea Dr. slaa na amewashukuru watanzania na anasema kuhusu mabadiliko makubwa na msingi wa uendeshji wa nchi na mambo ya katiba na pia wananchi wanaburuzwa na madaraka mikoani na halmashauri.
 
dr wa ukweli anashusha nondo .ametulia na ukumbi uko kimya .ameanza na mabadiliko ya katiba hasa madaraka ya rais.
 
hana mpya huyu labda tusubiri atazusha uzushi gani saa hii maana jamaaa kwa kuropokwa huyu
 
Nimechelewa kidogo, ila pia nitasaidiana na wanaoleta updates, stay tuned here at JF

Dr ndio anaongea,

Sasa anaongelea jinsi mamlaka za serkali bunge na mahakama vinavyoingiliana na anasema yeye atayaweka wazi zaidi kupitia mabadiliko ya katiba
 
Namfuatilia kwa makini mh. Dr. Slaa. Hakika huyu ndiye Rais wetu ajaye. Naanza kuamini kuwa kumbe tuna watu ambao ni zaidi ya almas. Watanzania tumtunze, tulikuwa tumepotea tumpe kura zetu aturudishe kanani.
 
Mabadiliko muhimu yanayotakiwa kufanywa
- mamlaka ya mkuu wa nchi ( kupunguza madaraka kwa mkuu wa nchi ili kuongeza uwajibikaji ) kuweka mamlaka yaliyo wazi , kugawanya mamlaka kwenye serikali , bunge na mahakama
 
Mabadiliko ya katiba kwa kupunguza madaraka ya rais, na kupunguza matumizi ya serikali. hapa ndio watu wengi wanalia hasa rais anapokuwa na madaraka makubwa na hakuna wa kumuadabisha.
 
Back
Top Bottom