Mdahalo Shirikishi: Watanzania Waarab au Wahindi wako wapi kwenye uongozi wa taifa letu?

Kuna kundi la watu ambao miongoni mwao hakuna aliyefanya dhambi?

Waarabu? Wazungu? Wabantu?

hehehe!! naam .... as long as teacher upo kwenye hii thread! wakijibu maswali yako tutajifunza mengi sana!!
 
Kuna kundi la watu ambao miongoni mwao hakuna aliyefanya dhambi?

Waarabu? Wazungu? Wabantu?
Dhambi ya ubaguzi, sisi wabantu kihistoria hatujafanya.

Mhindi na Mwarabu amefanya dhambi ya kumbagua Mtanzania, kihistoria?
 
Dhambi ya ubaguzi, sisi wabantu kihistoria hatujafanya.

Mhindi na Mwarabu amefanya dhambi ya kumbagua Mtanzania, kihistoria?

Mkuu mbona unataka nikujibie swali kwa premises ulizoziweka mwenyewe!

Wabantu hawakufanya ubaguzi, walikuwa wakivamiana tu Kabila moja na jengine kuonyesha mapenzi eee
 
Mwanakijiji, nadhani kawalenga Watanzania kama hawa Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othaman, Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Mtwara mjini Hasnein Murji.

Hawa ni baadhi ya Watanzania waliochanganya rangi, lakini Mwanakijiji kashindwa kuwataja kwa majina yao ingawa anawajua kahofia kukutana na maswali magumu.
 
Kwa namna ipi?Kwa namna ipi?

Mie nimeomba definition tu ya Mtanzania Muarabu na Mtanzania Mhindi na hadi sasa hapa tulipofika nimepata kutoka kwa mtu mmoja tu - Anheusier. Na hiyo definition aliyoitoa sina hata uhakika kama ndio definition inayotumiwa na watu wote humu ndani

Kwani kuna tatizo kwenye kutaka kueleweshwa?

Hakuna tatizo katika kueleweshana. Hata hivyo namna unavyoweka arguments zako inaonesha wazi kuwa umekerwa na mjadala kwa ujumla hivyo unaanza kuutikisa kwa kutafuta namna ya kuuzima. Ni sawa mtu aje akwambie "Gaijin naomba shilingi mia" halafu wewe uanze kumuuliza "Shilingi mia ya Kenya, Uganda au Tanzania?" au umuulize "Mia moja ni baada ya 99 au kabla ya 101?"

Nadhani ulitakiwa kuangalia mazingira ya "Kitanzania" juu ya Wahindi na Waarabu jambo ambalo kila siku linasemwa unless wewe "mwenzetu" si "mwenzetu"! (Usianze tena kuniuliza mwenzetu maana yake nini na scope yake ni ipi?). Kitendo cha wewe kusema MMJ amesema "Waarab" badala ya "Waarabu" kinaonesha kuwa una dhamira iliyojificha ama maslahi binafsi juu ya mjadala huu, ungeweza tu kusahihisha kwa kutafsiri Waarabu. Angalia usije ukani-challange kwa makosa ya spelling!! (Nimekosea spelling ya neno Challenge kwa makusudi).

Otherwise, kwa ninavyoufahamu weledi wako (Hapa JF) najua kabisa (Siyo kwamba naamini) kuwa umeelewa kinachosemwa hapa. Nice day to you Gaijin.
 
I have written about this topic before and I feel like I need to revisit it. It seems that our country is becoming more and more homogenous when it comes to racial make up of the top echelon of our country's leadership. ALL high positions of the country are being held by the racial majority - blacks. I'm more concerned about the Union Government:

Have a Look ( I don't mind kusahihishwa kama sitakuwa sahihi katika observation yangu):

Ikulu: Rais, Makamu - wote weusi
Waziri Mkuu - Mweusi
Mawaziri wote - weusi
Manaibu Wote - weusi

Mahakama
- Majaji wote wa Mahakama ya rufani (nadhani wapo watatu ambao wamechangia damu -sasa sijui tunatumia kipimo cha damu kidogo ya mwarabu we ni mwarabu au cha Wamarekani damu kidogo ya mweusi we ni mweusi!)!
- Majaji wote wa Mahakama Kuu ni weusi (sina uhakika waliochangia)
- Mahakimu sijui (lakini predominantly ni weusi bado - nakumbuka aliwahi kuwepo hakimu mmoja Mhindi sijui kama yupo)

Bungeni
Spika na Naibu Spika - weusi
Wenyeviti wote wa Kamati za KUdumu (ziko 17) - weusi

Jeshi la Polisi
IGP - Mweusi
Makamisha 4 wa juu - weusi
Makamanda wote wa Mikoa (nadhani ukiondoa mmoja - sikumbuki) ni weusi
(zamani walikuwepo polisi wa kigoa na singasinga)

Jeshi la Wananchi
Uongozi wake wote ni weusi!
Of course baada ya uhuru walikuwepo wazungu wachache waliobakia na wengine kupigana vita ya Kagera.

Naweza kwenda mbele na mbele; Hili linaniacha na maswali fulani ya kuchokoza:

a. Yawezekana tumekuwa ni taifa la wabaguzi wa rangi kuliko tunavyoweza kukubali?
b. Ukiondoa taasisi ambazo zinapandisha vyeo kwa merit ya ndani kwa ndani (polisi na jeshi); taasisi nyingine zinapata watendaji wake kwa kuteuliwa; hivi hakuna Mtanzania yeyote ambaye ni minority ambaye anafaa kuwa jaji? Yaani, kati ya wanasheria wote (na wapo wengi tu minority) hakuna anayeweza kupewa ujaji baada ya rekodi yake kuonesha kuwa anafaa?
c. Je serikali yawezekana haina mpango wowote wa kujaribu kurecruit minorities kwenye serikali yetu? Sijawahi kuona polisi au jeshi wakijaribu kuvutia watu wa minority - kwanini wakati baada ya uhuru tulikuwepo na vijana walioingia kwenye taasisi hizo na wakapanda vyeo taratibu? Ni kweli wahindi hawawezi kazi za polisi au jeshi (huko India nani anazifanya au Pakistani)?
d. Ni kwanini racially minority hawaonekani kwenye uongozi wa juu wa taifa letu kwenye maeneo YOTE? IS THERE ARE SYSTEMATIC DISCRIMINATION GOING ON?

Ikumbukwe kuwa Tanzania ilipozaliwa ilizaliwa ikiwa na tofauti moja kubwa - rangi haikutakiwa kuwa kigezo cha mtu yeyote kupewa au kunyimwa kazi katika Tanzania kama yeye ni Mtanzania. Tulikataa kabisa ubaguzi wa rangi na Nyerere alionesha hilo kwenye Jamhuri ya Kwanza na hata baada ya Muungano. What went wrong?

What is going On? Should we care? au watu weusi wamejiaminisha kuwa wao ndio "Watanzania zaidi" ndio "wazawa" hivyo "wanastahili zaidi"? Au wapo watu wanaamini kuwa "wahindi na waarabu" walishatutawala n.k n.k n.k hivyo hawastahili? Inawezekana kuna watu ambao akichaguliwa Waziri au kiongozi wa juu mahali fulani watawakuwa kama yule aliyelia baada ya Richa Adhia kuvaa taji la Miss Tanzania?

Je kuna umuhimu wowote wa Tanzania kuhakikisha kuwa hakuna systematic discrimination au kuwaacha minority pembeni? Fikiria US kwa mfano weusi wanamake up about 12-13 percent ya population lakini leo wanaye hadi Rais mweusi! Au Wamarekani wako mbali sana katika haya mambo ya rangi?

Mungu akubariki M.M

Hii thread yako imenigusa sana, ina ukweli mtupu, tatizo mijitu hawataki ukweli
 
Mkuu mimi naona hii ni mada nzuri sana. Ni vizuri kufanya tathmini/utafiti isije ikawa kuna "systematic discrimination of racially minority groups". We should not just take it for granted that it happened naturally. Sometimes some minority groups are systematically discriminated and many people wont realize because they think that it happened naturally.

In our situation, though, I think most of these racially minority groups, namely arabs and indians have opted to stay out of some circles especially public service. Most of them indulge themselves in trade rather than being employed by someone. I think they inherit certain practices from their parents, whom, I believe you will agree with me, are mostly wealthy businessmen. I once read in a book titled "Rich Dad Poor Dad" where the author says that the rich teach their children how to make money work for them as opposed to the poor who send their children to schools and colleges so they can be employed in reputable organisations.

One friend of mine once asked me a question, "have you ever seen a white Tanzanian (a hind or an arab) in a job interview?" Surely I have attended a few interviews but I do not remember seeing them in job interviews despite the fact that I had several colleague at the college who were not blacks. He then told me that they send their children to gain the necessary knowledge to enable them to establish their own businesses not to be employed.

However, the question remains, why dont we find any of them in certain trades such as the army, police force, the judicial system, etc. I think we need to do a research before we come to a conclusion.
 
Hakuna tatizo katika kueleweshana. Hata hivyo namna unavyoweka arguments zako inaonesha wazi kuwa umekerwa na mjadala kwa ujumla hivyo unaanza kuutikisa kwa kutafuta namna ya kuuzima. Ni sawa mtu aje akwambie "Gaijin naomba shilingi mia" halafu wewe uanze kumuuliza "Shilingi mia ya Kenya, Uganda au Tanzania?" au umuulize "Mia moja ni baada ya 99 au kabla ya 101?"

Nadhani ulitakiwa kuangalia mazingira ya "Kitanzania" juu ya Wahindi na Waarabu jambo ambalo kila siku linasemwa unless wewe "mwenzetu" si "mwenzetu"! (Usianze tena kuniuliza mwenzetu maana yake nini na scope yake ni ipi?). Kitendo cha wewe kusema MMJ amesema "Waarab" badala ya "Waarabu" kinaonesha kuwa una dhamira iliyojificha ama maslahi binafsi juu ya mjadala huu, ungeweza tu kusahihisha kwa kutafsiri Waarabu. Angalia usije ukani-challange kwa makosa ya spelling!! (Nimekosea spelling ya neno Challenge kwa makusudi).

Otherwise, kwa ninavyoufahamu weledi wako (Hapa JF) najua kabisa (Siyo kwamba naamini) kuwa umeelewa kinachosemwa hapa. Nice day to you Gaijin.

Hakuna mazowea kwenye haki za watu wala kwenye elimu. Kama tungekuwa tunakwenda kimazowea tu hadi leo wanawake wangekuwa hawapigi kura na tungesema jua linaizunguka dunia. Kwa hiyo kuuliza kwangu hakunifanyi kutaka kuitikisa wala kuibeza thread, bali ni katika kutaka tuelewe vizuri kile tunachochangia.


Tunapomzungumzia Mtanzania Mhindi na Mtanzania Muarabu kwenye uongozi wa nchi lazima tuwe na definition ili tujue tunamzungumzia nani. Kuna Wahindi walikuja tangu enzi za Mjerumani kujenga reli na kuna Waarabu waliokuja kufanya biashara na kuselelea karni nyingi sana nyuma. Hao vizazi vyao vilivyopo hapa leo, lazima tujue tunawaweka kundi gani.


Othman Chande ni Mtanzania Muarabu? Salim Salim jee? Zungu nae?



Bila ya kujua scope ya hao Watanzania Wahindi na Waarabu, sijui tutawezaje kupata mawazo na fikra za maana


Mwanakijiji Kama muandishi mahiri anaelewa fika kwa nini amekosolewa neno lile alokosolewa. Ni suala la kuwa makini kwenye details tu

Have a good day :]
 
M/kijiji mada hii ni nzuri lakini,inayoitaji uelewa mpana sana,kati ya majoriy na minority nani anambagua mwenzie.Kwa picha ya haraka ambayo wewe umeitengeneza ni kuonyesha majority wamewabagua minority [Wahindi na Waarabu,japo pia kuna Wazungu na Half-caste] ambao hapa wewe umewataja ni wahindi na waarabu.Je ni kweli majority ambao ni wabantu kwa maana ya watanzania weusi kwa rangi ya ngozi yao wamewabugua watanzania wahindi na waarabu nyeupe kwa rangi ya ngzoi yao?

Historia ni mwalimu mwema daima,kabla ya uhuru Tanzanganyika ilikuwa na raia katika madaraja kama ifuatavyo
1: Wazungu-hawa walikuwa dalaja la kwanza na makazi yao kwenye miji yetu Tanzania yalijulikana kama Uzunguni
2: Wahindi na Waarabu-daraja la pili ambalo makazi yao yalijulikana kama Uhindini
3: Wamatumbi-Watanganyika sasa watanzania-darja la tatu makazi yao Uswahilini na vijijini kote Tanzania.

Hivyo kwa picha hiyo,unaona tayari ndani ya kila mmoja kuliundwa tabaka ambalo lilijengeka vichwani mwa kila mmoja.Ila ujio wa uhuru ulifungua tabaka la tatu ambalo ndio lenye watu wengi [Majority] kubeba dhamana ya kimadaraka Taifa.

Malimu Julius Kambarage Nyerere,alikuwa na dhamila njema sana yeye kama yeye binafsi.Na ndio maana hata marafiki zake wa karibu kwenye ushauri kisheria walikuwa Wahindi.Mwalimu alijenga mfumo ambao hakika,aliwapa fulsa wahindi na waarabu kuendesha biashara pasipo kutengeneza mfumo wa kuwabilidilisha nao kimtazamo wao kutoka kwenye daraja la PILI baada ya Mzungu.Mwalimu akaangaika kuliondoa daraja la kwanza yani wazungu waliokuwa wafanyakazi kwenye ofisi za Serikali na makampuni ya Serikali na yasiyo ya Serikali kwa kuwapandishia kodi wakashindwa kumudu kuishi Nchini katika daraja lile la kwanza hivyo wengi kujikuta wanaondoka kuludi zao Ulaya,wakiwaacha wahindi na daraja la la pili Nchini wakipeta.

Lakini wakati Mwalimu anabomoa daraja la Kwanza alisahau kubomoa daraja la pili,akaluka akaja kuangaika na kulipandisha daraja la tatu kutoka mwisho kuja juu akifikilia daraja la tatu nao wote wanawaza kama yeye anavyowaza.Matokeo yake daraja la la tatu walivyofika juu nao wakabadilika na kwa kushirikiana na baadhi ya wa daraja la pili ambao nao walishapanda kuwa daraja la kwanza kwenye sura isiyo ya kimadaraja lakini mioyoni mwao na dhamira zao wako kwenye dalaja la kwanza ndio hao baadae walikuja kupewa majina ya Baba Benzi.

Kwa ujumla Mwalimu alifanya mazuri sana lakini swala la kudeal na minority Mwalimu alichemka sana,kwa kuwa Mwalimu aliwaamini sana minority na kuwaona kama watu wasiostahili kutiliwa shaka,na daraja hili la pili wahindi na waarabu walilijua hilo na walikuwa wajanja sana,hata katika kumshauri mwalimu walijionyesha kama watu walio royal sana kwa kiongozi na mpaka leo ndio wanavyocheza na baadhi ya viongzoi wetu.

Ujio wa azimio la Arusha,ambao uliwanyanganya Mali wale wote waliokuwa wamejilimbikizia iwe kwa njia halali au haramu mali ambazo ziliamishwa kutoka kuwa za watu binafsi na kuwa za umma ilikuwa pigo sana hasa kwa wahindi na baadhi ya waarabu.Kwa kuwa baadhi yao waliona ni heri Taifa lingeendelea kuwa chini ya Mkoloni kuliko kuwa huru.Lakini tofauti ya kimapato ya kimaisha ambayo Mwalimu aliiona ikijijenga ilikuwa ni madaraja ambayo leo tunayo ya baadhi ya wachache kuwa matajiri wa kukufulu huku wengi wakiwa hawana uwezo wa mlo mmoja kwa siku, na lengo la Mwalimu halikuwa kuunda madaraja bali juenga Taifa la watu sawa wenye hadhi sawa pasipo kujali nasaba ya mtu.

Kutokufutwa kwa asili ya madaraja ambayo yalijengwa toka zama za mkoloni kuwa huyu ni muasia na huyu mmatumbi,na kuwa hadhi ya kimakazi, mfumo ulikosea sana kuangalia dhana nzima hiyo ambayo ilijikita vichwani mwa wahindi na waarabu tena wakiwa na dhamila wachukue daraja ilo la kwanza,na ndio maana Mwalimu alipokuja kuzinduka akapitisha fyagio la utaifishaji wa mali kuwa za umma.Nasikia Mwalimu alikuwa na ugomvi sana na watu kama Bokhe Munanka aliyetaka mfumo wa kuishi na wahindi na waarabu uangaliwe kwa jicho la karibu sana.

Kibiashara
Wahindi na Waarabu baada ya Privatization ,walijitoa katika shughuri za Serikali na kuamua kujituma kwenye shughuri binafsi zikiwa ni hasira na kuanza mikakati ya kuishi mguu ndani na mguu nje huku wakijifanya kuwa ni waaminifu kwa Serikali ya Mwalimu.Mbaya zaidi wale wamatumbi weusi waliopata nafasi ya kuwa viongozi kwenye Serikali walilubuniwa na baadhi ya Wahindi na Waarabu kuanza kuunda mfumo wa kuiba mali za umma na uchotaji katika migongo ya wafanya biashara,ambao walipata tiketi ya kumpumbaza Mwalimu kwa wao kuonekana ni waaminifu kwa Mwalimu kumbe nyuma yake wanamtafuna kupitia wasaidizi wake ambao si waaminifu kwake na kwa Taifa.

Sekta ya biashara Tanzania toka enzi ya ukoloni na hata baadae Mwalimu ilikuwa mikononi mwa hao wanaoitwa minority,na Mwalimu alipoingia madarakani na kuona jinsi gani wachache wanaweza kugeuka wazungu ndani ya rangi tofauti ndio maana akaja na azimio la Arusha.Lakini bado akutengeneza kada ya majorirty nao washiriki kama wafanya biashara kwa kuwa empower bali nguvu akaamisha kwa kuunda mashrika ya umma.Japo lilikuwa wazo zuri lakini ubaya halikuwa wazo shirikishi kama lilivyokuja wazo la Ubinafsishaji wakati wa BMW pasipo kuwashirikisha umma bali vikundi vya watu wachache.

Kwa uhalisia wananchi walipaswa kushirikishwa nini kifanyike kwao katika sekta ya biashara.Mwalimu akaweka nguvu kwenye kilimo huku wachache wakimuhujumu kwenye viwanda na mali za umma.Mfano mzuri wa kutokushirikishwa wananchi juu ya jibu la ajali za barabarani ni daraja la Manzese,matumizi ya daraja la manzese sio wazo shrikishi kutatua tatizo la ajari za barabarani maeneo hayo,matokeo yake ajali zinaendelea kama kawaida.

Kielimu
Aingii kichwani kuwa mpaka sasa bado kuna shule ambazo bado watoto wa kihindi na kiarabu wanasoma pekee yao.Je mfumo [SYSTEM] ilikuwa wapi na iko wapi kufuta aina hiyo ya kuwa na aina moja ya tabaka kusomesha watoto wao ndani ya Taifa lenye aina kubwa ya mchanganyiko wa makabila.Leo hii mtoto wa kihindi anasoma chekechekea mpaka form six Tanzania lakini ajui kiswahili,chuo kikuu anaenda Canada au USA ama Uingereza.Tanzania inabakia kwake ni sehemu ya kuchuma yeye na familia yake lakini makazi lasmi yakiwa ugahibuni aliko pata elimu na kununu makazi ya kuishi maslahi ya kuendeshea maisha duniani yanatoka Tanzania.

Kimakazi
Ni Tanzania pekee watu bado wanatambua mji kupiti utaifa,japo wengine ulazimisha kusema mbona USA, wanayo majina hayo kama CHENESE TOWN,!!Jamani ni upumbavu kuwa watumwa wa kuiga mambo tusiyo na uwezo nayo,wale ni wamarekani sisi ni watanzania.Leo unafika sehemu unasikia hapa ni UHINDINI !!! ama hapa NI UDOSINI!!...Hii ni aibu na wao wahindi waliotutenga chini ya mgongo wa support ya Serikali wanaishi na kufurahi hali hiyo kwa kuwa na makazi yao,Madhehebu yao,Shule zao,Kila kitu chao.

Leo hii Serikali haina mpango wa kuwatawanya wahindi kutoka NHC walizokaa miaka nenda ludi wapewe viwanja waamie Mbagala, Kijitonyama,Tandika au kwingineko kwa nia ya kuwa minority nao waishi na Watanzania wenzao majority katika mitaa na makazi kama wengine.Sasa hivi baadhi yao wamekuwa Maland Lord walioamua kujenga majumba mitaa ya Upanga na Oysterbay mkakati ni kuakikisha kuwa wahindi hawatoki maaeneo mbali na jumuhiya zao,tizama magholofa binafsi yanayomilikiwa na matajili wa kihindi na kiaarabu kaangalie wapangaji ama wenye nyumba [Appartment] kama kuna mswahili kwenye compound za majengo hayo,walio humo ni wahindi na waarbu na Serikali inajua na kukaa kimya ikiona ni kawaida.Haiwezkeani Appartment sitini zote wakae wahindi pekee yao Serikali pasipo kutia mkono kuwa ni lazima ziishi familia tofauti tofauti.Watanzania wakisema unaambiwa soko huru,eeeh soko huru au uria lisilo na kanuni ni uhuni.Matokeo yake eneo zima unakuta ni aina maoja ya Taifa.

Kimahusiano [Ndoa]
Ubaguzi mkubwa upo kwenye swala la ndoa na mahusiano,hapa kwa mfumo ulivyojengwa na kuendelea kuaminika kwa majority wanaamini kuwa ni lahisi mtoto wa kiume wa kibantu -mmatumbi kumuoa binti wa kizungu toa ulaya kuliko kuwa na urafiki potelea mbali wazo la kumuoa binti wa kihindi ama kiaarabu.Kuna kijana wa kibantu alienda masomoni India akapata rafiki wa kike wa kihindi akaludi nae home Tanzania, akaishi nae wahindi wakajua wakaengineer mambo binti akaludishwa India kwa style waliyomchezea mbantu.

Lengo lao nini ni mweusi kuonekana ana mahusino na Mhindi au Mwarabu kwao wao hawa minority ni taboo.Ili liko wazi kwa wanaojua Wahindi wa India na baadhi ya mataifa ya Uarabuni uwa wanaishi kwa matabaka,yani daima wanatambuana na kuoana kwa kutumia madaraja na hiyo ndio assimilation waliyo nayo wahindi na Waarabu kwa kuwa mwenye asili aachi asili yake.

Waarabu nao kama wahindi wao wamejaribu kuoa mabinti wa kiswahili lakini si mabinti wa kiarabu kuolea na vijana wa kibantu yani majorirty.Nao hawa waarabu wanasura ile ile ya ubaguzi ambao umejijenga wa kuzalau kada ya mmbantu na kumuona kama maskini asie na uwezo wa kuishi na binti wa kiaarabu.Na ikitokea hivyo basi familia umtenga na kumfanya binti yao ajisikie ndani ya dhambi ya radhi ya familia na wazazi.

Uraia wa Wahindi na Waarabu

Hakika inaumiza sana kusikia mfumo umehalalisha Taifa kuwa na Mataifa ndani ya Taifa.Hakika inapaswa kujulikani kuna watu wanaitwa watanzania,hakuna Mtanzania-Muasia,Mgogo Mtanzania,au Mkurya Mtanzania.Hivi inakuwaje mpaka Taifa linakubali wahindi hawa kujibatiza kuwa ni Watanzania-wenye asilia ya asia.

Kwanini tusiwe na jina moja linalotambulika kwa mhindi-hata kama ni kuwaambia watafute term itakayowatambulisha kwa ujumla wao kuwa Watanzani kama tunavyosema wachaga lakini sio waasia,waasia wako bara asia,hiki ndio chanzo cha hawa jamaa kuwalea na kuwakuza watoto wao wakiwa mguu ndani na mguu mwingine nje, na upeleka wake zao kujifungua Canada,UK na USA ili kupata uraia huko.Matokeo yake uleta watoto uku wakachukua uraia wa Tanzania na USA [Michezo ya Dual-Pass] lengo ni kwa faida za kiuchumi na si za kitaifa kama ambavyo ingekuwa ni kwa mbantu.

Kosa letu Nini?
Kosa la baguzi hizi ni matokeo ya inferiority na superioity kutoka pande mbili moja ikiwa dominant dhidi ya nyingine kiuchumi na kihaiba. Chanzo chake ni mapungufu ya KIMFUMO [SYSTEM]. Hatuna mifumo ambayo ilipaswa kutengeneza mazingira ambayo yatalenga kuondoa Superiorty na inferiority ambayo yatafanya kundi moja Superior ambao ni Minority lisijione kuwa lina uwezo na kuwa linastahiki privellege zote kuu na kuwa lina akili sana kuzidi minority na mbaya zaidi linajijenga kinasaba kuwa limeteuliwa kutumikiwa,ndio maana hakuna familia ya kihindi au kiarabu isiyo na wafanyakazi wa ndani ambao wana maendeleo kulinganisha na walio kwenye familia za kibantu na kizungu,hiki ni kipimo kidogo sana cha chini kwenye swala la ustawi.

Pia swala la wabantu [majority] kuwa inferiority haswa kwa watu wazima kizazi cha waliokuwa watoto na vijana kabla ya Tanzania kuwa huru, kizazi hicho niwaoga sana kila wanapokutana na kada hi ya Waarabu na Wahindi.Nimeshashuhudia baadhi hata ya watu wazima ambao mimi nawaheshimu wakimuona Mzungu, Muhindi au Mwarabu wana kuwa na hofu mpaka katika kujieleza.Kama ni mazungumzo unaona dhahiri mmatumbi anavyobuluzwa kwenye mazungumzo kwa mmoja kuonekana kama anae report kwa bosi hata kama ni mazungumzo ya kawaida.

Fikra hizo walizolithi watu wazima Wamatumbi [Majority] ambao wengi wao ni viongozi ndio hizo zilizotumika kuwapa fursa za kiuchumi wahindi na waarabu na kuingia nao mahusiano ya kibiashara yenye sura za kificho wakiwa madarakani, hatimae wakitoka madarakani udhulumiwa Mali zao na kuwaacha wakiangaika na mashinikizo ya moyo na hatimae vifo huku wahindi wakipeta na maisha ya kulea na kusomesha watoto wao kwenye majumba waliyo nunua Canada,Uk na USA.

NI kweli kuna Ubaguzi uliojengwa chini ya kivuli cha mfumo [system] ambayo mpaka sasa wahindi na waarabu [ambao imewapa jina Watanzania wenye asilia ya Kiasia],na kwa ubaguzi huo ni matokeo ya mivutano ya migandamizo [Conflict of Interest] ya kitabaka na kiuchumia, ambao mfumo [system] bado haujaupa jicho la ndani,na watawala kutumia hawa minority kufichia madhambi yao kwa kujua wana uwezo wa kuhifadhiwa madhambi yao na kada hiyo yenye sura ya upole na unyenyekevu kwa watawala [ROYAL] kufaidika na wizi na upofu wa majority kuishi kwa kuamini historia, na ulibukeni wa kiafrika dhidi ya Mtu mwenye ngozi nyeupe.

Wanasiasa na watawala kwa kujua mchezo mchafu ambao ufaidika nao kutoka na mnyukano huo wa kitabaka na kiuchumi ambao asilimia 83%ya uchumi wa Watanzania, huko mikononi mwa hao wanaoitwa Watanzania wenye asilia ya kiasia.Wamefumbia jicho ambalo lilionwa na Marehemu Bhoke Munanka miaka ya sitini mpaka leo,walichofanya ni kukubaliana kuwaweka pembeni kwenye maswali ya utawala na utendaji wa kiserikali bali kuwapa baadhi ruksa wachache kuja kwenye siasa ili waweze kufanya lobbing za ujenzi na utungaji wa sheria za uendeshaji wa Serikali na Nchi zitakazowagusa kwenye sekta yao ya kibiashara ambayo sasa imefanikiwa na uimarika chini ya Sera za Ubainafsishaji ambako wao wameshika mpini na majority wameshika makali.Minority ndio walio wengi wenye kuhodhi njia kuu zote za uchumi wao wakiwa ndio wamilki na wabia wao baadhi ya viongozi wetu kutoka katika kada ya majority.

Wahindi na Waarabu wamekosa nafasi kwenye madaraka ya kunyenyekewa na kusimamia sheria kwenye utekelezaji lakini wamefanikiwa kwenye kumilki sekta kuu zote kuu za uchumi,na Taifa kama Taifa tuko mamilioni ya majority na minority ni wachche sana.Hivyo majority wanamilki Serikali waliyokasmisha kwa wanamajorty wenzao ambao wanahusiano na minority ambao wao wanamilki njia zote za uchumi na Ndani na Nje ya Nchi.
 
Mkuu, Mbunge wa Mwanza mji Ezekiel Wenje, hana asili ya Kenya na yeye tutamuitaje?

aitwe Mtanzania Mkenya ikisha kila anapokwenda anyooshewe kidole hivyo. Baada ya hapo aanzishe jumuiya ya Watanzania Wakenya wagombanie haki zao.

Wakimaliza Watanzania Wakenya, Watanzania Wahindi na Watanzania Waarabu wafanye vivyo
 
Kwa upande wa wahindi tuna tatizo kubwa, ni wahindi kwa maana ya foreigners kwanza halafu -wasafiri walioko Tanzania kwa muda second. Ni wahindi wachache mno wanajihesabu kama watanzania. Wengine wote utafikiri wako safarini kuelekea somewhere else.

Hapa nakubaliana na wewe, wengi wao (wahindi) wana uraia wa nchi zaidi ya moja na wengi wao ndoto zao huwa ni kutafuta pesa hapa kisha wanaenda zao Canada, Uingereza au Marekani. Hapa ni wapita njia tu.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu swala lako linatazama upande ambao hao wahindi na waarabu hawautazami kabisa kwa sababu asili yao watu wa Middle East sii kukamata UONGOZI bali wanachoamini ni MONEY and POWER ya kushika uchumi wa nchi husika. Wayahudi, Wahindi, Wabulushi, na Waarabu kila wanapokwenda dunia hii hutumia mfumo Al Pacino ktk sinema ya Scarface - MONEY bring power, once you have power the world is yours!..

Hivyo ndivyo wamezikamata serikali zote za Ulaya na Marekani pasipo kushika madaraka ya juu ktk nchi hizo. UK leo wanalia na wahindi, ukimwona Mhindi kajiingiza katika siasa basi ujue huyo ni mtoto wa mlalahoi na mzaliwa ktk mazingira na malezi ya nchi hiyo. Kwa sababu mara zote kutokana na greed yao ya mali (utajiri) kujishehena madhahabu na vito (hadithi na historia) wakiingia ktk uongozi ni mara moja wataharibu. Mifano ipo kibao ya kina Rostam Aziz ni wengi tu wametokea nchi mbali mbali. Hawa watu hawahitaji kuwa madarakani ila penmye kutengeneza fedha. Ukimuona Mwarabu au Mhindi kijijini kwako basi jua kuna Utajiri..na wala sii asili yao kuongoza bali kutawala kwa nguvu ya fedha.
 
..AFRICANIZATION.

..ARUSHA DECLARATION.

..hayo ni moja ya mambo ambayo yaliwaathiri hawa wenzetu.

NB:

..hivi mmewahi kujiuliza kwanini WAAFRIKA wako kwa uchache sana ktk biashara kubwa-kubwa nchi hii?

..pia kwanini biashara haramu ya pembe za NDOVU, FARU, na NYARA ZA TAIFA, wahusika wakuu ni wa-Tanzania wa asili fulani tu?

..pia ile niliwahi kuleta picha ya wafanyabiashara waagizaji MAFUFA na majority walionekana kuwa wa-Tanzania wa asili fulani?

..WHY DO WE HAVE SUCH TRENDS IN OUR SOCIETY????
 
Back
Top Bottom