Mdahalo: Ndugai vs Lissu - Jumamosi Julai 30

Status
Not open for further replies.
hofu yangu ndugai asije akajisahau akataka kumpiga redcad Tundulisu kama kwenye bunge,kumbe yumo ktk ukumbi mwengine kabisa
 
Anaonekana kama anatakakuleta mambo ya mzaha jinsi anavyo ongea hapo bungeni kuhusu mambo ya mdahalo,kwenye huo mdahalo ajue tupo serious nao ndio tatizo la magamba mamabo ya msingi wanaleta mambo ya ushoga na mizaha kibao tunasema mwisho wao waja.
 
Je, Ndugai ana ubavu wa kushindana hoja na Tundu Lissu? Hapa naona mlima na kichuguu.
Hapo ndipo penye tatizo. Hivi magamba wote wameshindwa kupata mtu anayeweza walau kujenga hoja za kiwango cha Lissu? Sitashangaa Ndugai akiingia mitini siku hiyo.
 
Hapa hoja sio umahiri wa Tindu Lissu au Ndugai. Mimi ninachokiona utakuwa ni mpambano kati ya ukweli na uongo. Chama cha magamba sasa hivi kinajikongoja kwa kuwaambia wananchi uongo. Kuanzia M/kiti wao ni mwongo, W/mkuu ni mwongo pamoja na mawaziri na mtiririko wote. Kwa hiyo kitakachompa shida sana Ndugai ni kukanusha ukweli. Chama chake cha magamba kitampa wakati mgumu sana kwa sababu serikali yake imeshavurunda mengi na bado inaendelea kuvurunda siku hadi siku.
 
Kumpanisha ndungai na Lissu ni sawa na kuipambanisha Yanga na Manchester United!!!! Mshindi ameishajulikana hata kabla mechi haijaanza!!!!

Tiba
 
Hee! Ndugai alimzuia Pinda kujibu maswali magumu bungeni jana, sasa Rosemary itabidi naye amzuie Ndugai kujibu maswali magumu ukumbini, maana kwa kweli yeye alichofanya jana ni kutekeleza amri ya chama chake kuhakikisha wapinzani hawawi tishio nchini. Hata ungekuwa wewe ungeweza LABDA kulinda kitumbua chako kisiingie mchanga. Akikumbuka kilichompata 6 kwa kuwaachilia wapinzani watese bungeni na madhara yaliyopatikana kwa chama ni lazima ndugai angepaswa kutetea chama chake kilichompa ulaji. Huo ndio ubinadamu wa kawaida tuache utani.
 
Mimi kwa upatu wangu naona utakuwa mdahalo mzuri sana kama Lissu atapunguza jazba na kuzungumza vizuri kwani Ndugani ni mwanasheria mahiri sana na mtulivu sana katika kupambana na hoja.

Nazidi kusisitiza kuwa LISSU apunguze jazba ili mjadala uwe mzuri kwa faida ya wachangiaji na watanzania wote kijumla .

nawatakia mafaniio mema.
 
kwa sheria za bunge Tundu ataumbuka, hazijui, ama sheria za nje ya bunge Tundu anazifahamu sema tatizo lake hajui kujenga hoja kwa lugha ya kawaida huwa anajenga hoja kwa lugha ya jaziba sana. kitu ambacho mimi siamini kama mtu kujenga hoja mpaka utumie jaziba

Kwa taarifa yako, pamoja na kuwa mtaalamu wa sheria za mazingira, pia ni GURU aliyebobea sheria za mabunge na kanuni zake katika Common wealth countries.. Ndugai lazima achape lapa mapema...utaniambia hiyo kesho..uzuri kwanye mdahalo hakuna askari wa bunge...atachapa lapa mwenyewe... You got me
 
Kumbe mdahalo umeshapita Juni 30, mod iondoe hii thread.

Sorry, kidole kiliteleza kidogo kwenye key board, isomeke July 30, 2011

Na jaribu kusoma habari yote ili mapungufu ya headline yasikuumize kichwa

 
Mh Naibu Speaker kajitangazia ushindi mnono wa hiyoo kesho! alijitangazia ushindi huo leo asbh wakati wa kutoa matangazo ndani ya mjengo.
Ilivyoonekana alikuwa na hofu khs mdahalo huo.
aliwaomba walipukaji wenzie wawepo kesho ndani ya mdahalo kumpa support kiaina wakati akitangaza mjengoni!, alionyesha hofu kubwaaa..!!!

huyo Bibie Mwendesha mdahalo inavyoonyesha ana usongo na walipukaji....., habari za chini ya jamvi nackia alikuwa ameajiriwa na Habari Corporations ya Rostam Aziz.
Baadae Mh Rostam akampiga chini kiaina! so still ana usongo na walipukaji mjengoni!

Muhimu 2waombe TANESCO chini ya Mh Ngeleja wasijeficha aibu kwao kwa kuuchukua Umeme wao!
 
..namshauri Tundu Lissu ajiandae vyema kwa ajili ya mdahalo huo.

..Ndugai si mtu wa kumdharau ukizingatia kwamba alimdhibiti Freeman Mbowe ktk mahojiano waliyofanya pamoja.

..katika mdahalo wake na Mbowe, Job Ndugai alifanikiwa kujenga taswira kwamba wabunge wa CDM ni watu wasiojua sheria na taratibu za bunge, pamoja wajibu wao kama wawakilishi wa wananchi. The sad thing ni kwamba Mbowe alishindwa kujibu mashumbulizi hayo.

..tusimdharau Ndugai, he can do some damage to CDM's image and reputation. tusisahau kwamba he comes across as an innocenct, calm, and collected individual.
 
Naondoka sasa hivi naenda morogoro,lazima niushuhudie mdahalo huu live,najua tanesco kesho watachukua umeme wao hapa dsm.
 
Ninasumbuliwa na mda,kwa nini wasifanye kama inavyokuwa nkrumah walau watu hupata mda wa kutosha saa4-8 kuliko haka ka1.30hrs,huu ni upuuzi,imagine mwongozaji mwenyewe huyo,utangulizi 15min,kufunga15min,sasa60min zitatosha maswali gani na mangapi na kwa ufafanuzi gani?ama ndo funika kombe?

hata kwenye mtihani unaweza ukafeli si kwa vile ww ni kiraza bali mda ni mfinyu sana,kama wanataka walau waweke 120min vinginevyo it's kidding us!

hapa ishu sio mdahalo namaanisha mda ndo ishu ya msingi,let us be serious tunapodebate hot issues tuweke mda wa kutosha kwa maana hatufanyi maigizo hapa,hii sio bongo movie we need appropriate time,iweje kipindi cha kipimajoto ITV chenye wageni4 kipewe 2hrs alafu hii ishu ina watu 200+ ipewe 1:30?
 
imekaa vizuri hiyo ila inabidi lissu awe makini asije akatolewa nje ya ukumbi na job ndugai.
 
Makamba angekuwepo angemkataza kama alivyomkataza jk kufanya mdahalo na dr slaa, kwani anajua baada ya hapo ni aibu.
 
Status
Not open for further replies.
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom