Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
TAASISI ya Vox Media Centre Tanzania na East Africa Business and Media Training Institute (EABMTI) kwa ushirikiano na kituo cha Star TV kesho wataendesha mdahalo wa kibunge, mada ni Bunge la 10 na Tanzania tunayoitaka. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyopatikana Dar es Salaam jana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vox Media, Ansbert Ngurumo, inaeleza kuwa mdahalo huo utafanyika kwenye ukumbi wa Mtakatifu Gaspar mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa Ngurumo katika taarifa hiyo, wazungumzaji wakuu kwenye mdahalo huo ni Naibu Spika Job Ndugai na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, huku wananchi 200 wakipata nafasi ya kuwauliza maswali; mdahalo huo utarushwa hewani kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 1:50 usiku. Inaelezwa kwenye taarifa hiyo kuwa ni fursa nyingine kwa wananchi kujadili masuala nyeti yanayohusu uhai wa taifa kwa kumulika, kuhoji na kutafakari namna Bunge linavyowawakilisha.
Ni fursa yetu kupima utendaji wa wabunge na kuhoji kama wanakoelekea ndiko tunakopaswa ni fursa pia kwa wazungumzaji wetu kusisitiza yanayopaswa na kukosoa yanayopotoshwa au kukosewa kuhusu Bunge, ni fursa kwa wabunge kujipima kwa maoni ya wananchi, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Katika mdahalo huo Mkurugenzi Mtendaji wa EABMTI, Rosemary Mwakitwange, ataongoza mdahalo huo kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa taasisi hizo. Mwaka jana taasisi hizo ziliaandaa midahalo kadhaa wakati wa kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu iliyohusu wagombea urais wa Tanzania.
Tanzania Daima