Mkuu Tempolale, kumbe umegundua jinsi ninavyoichukia Chadema!.Huwa unanifurahisha kwa maoni yako lakini maoni yako mara nyingi sana lazima kuwe na statement inayotoa picha harisi ya namna unavyoichukia chadema. Hivi kwanini usiyaangalie yale magwanda ya Chadema kwa mtazamo wa kwamba chadema wameshona sare zao kwa kitambaa kigumu kwasababu hawana uwezo kama CCM hivyo wanataka zidumu zaidi?
..isije ukawa unatumia neno mapinduzi ili kuwatisha watu.
...najua nyinyi wana-CCM ni wajanja sana kutumia maneno na kuhadaa na kuwatisha wananchi.
Sio tu kwamba NAKUMBUKA, bali pia NAFAHAMU hilo na nilitegemea wewe pia ungekuwa na ufahamu wa hili, hasa the fact kwamba for the past 20 years or so, CCM is Facing A Crisis in its Political Hegemony, na ni moja ya sababu kubwa kwanini upinzani unazidi kushika kasi;..kumbuka kwamba CCM maana yake Chama Cha Mapinduzi.
..we just need a better Tanzania…
…sasa wewe ukiita mageuzi, mageuko, mapinduzi, hiyo ni juu yako.
Chadema wanapozungumzia (M4C) wana maanisha nini? M4C inasimama badala ya movement for Change ina maana kubwa.
Mabadiliko kama mabadiliko yana maana na dhana kubwa mno ambayo inahitaji umakini kujadili kwa kina.
Dhana ya M4C ya chadema sijaielewa kabisa. Ndio maana mimi naiita "movement for power" na hii M4C ni kivuli tu cha kufikia malengo yao ambayo kwa uhakika sio yenye malengo ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu.
Mimi siongelea kuhusu hisia hapa naongelea ''fact'' huo ndio ukweli.Wanachofanya ni kutaka kuondoa Regime tu lakini hakuna specific program ambazo watakuja ku implement ili ku transform jamii yetu.
.
.
Maadili pia ndani ya chama ni mabovu kama chama hakina order na discipline wakati hakiko madarakani kikiingia kitafanya nini? Chama chochote kitacho komboa Taifa hili ni kile viongozi wake wana maadili, kina Order na discipline ndani yake na viongozi wake wanaheshimiana na wanaongozwa na dira moja tu Utanzania.
Mtoa mada unasema kuwa M4C huielewi au unaielewa ??
Hapo juu kwenye blue, unasema huielewi !!
Halafu tena hapo kwenye red, unasema unaongelea fact !! Fact ya kitu usichokielewa ?? Au fact ya kitu gani ??
Rudi ukaeleweshwe vema kuhusu M4C. Ukishaielewa, uichambue, ndio uje na facts za M4C hapa JF.
Huwezi kusema unaleta facts za kitu ambacho wewe mwenyewe umesema hukielewi !!
Kwa kukusaidia tu, moja wapo za facts za M4C ni kuondoa utawala wa mafisadi na kuweka utawala adilifu wenye kuleta maendeleo ya Watanzania wote, sio maendeleo ya mafisadi. Hiyo ndio Change !!
Ideology ipi iliyopo?
Mkuu huna haja ya kuzunguka zunguka; Kwa ufupi M4C inalenga kuleta
mageuzi makubwa nchini katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa kupitia Mapinduzi ya kidemokrasia.
Nakubaliana na wachangiaji wenzangu. Kitu ambacho hatuelewi watanzania hasa viongozi na wasomi ni kuendelea kufikiri maendeleo yataletwa na hiyo mikakati inayotoka world bank na kwingineko i.e. Mkukuta, tasaf etc.
Haya mataifa yanayotoka eg china, korea, india hata iran kwa asilimia kubwa wamepiga hatua kwa kutumia bongo zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kununua au kuiba technology ambayo wanajua itawatoa!
Mapinduzi ninayofikiria mimi ni katika elimu, mtoa mada huenda wewe ni mhadhiri chuo fulani, tunahitaji mfumo utakaofanya watanzania wafikir kwa akili zao namna ya kutoka (to progress) kama wachaga wanavyoanza kwa kuuza karanga barabarani, kaduka, duka, retail, whole sale etc.
Kwa kweli wananchi tumechoka kiasi kwamba hayo mageuzi au mapinduzi yaje tu tuone the other side of the coin. Will be positive with positive thinking (which we lack), negative if we continue the way we think now!