JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,442
- 54,993
nakubaliana na wewe!!ni lazima tuandae kundi dogo la 'wasomi' lakini tusisahau kutoa ujuzi kwa 'vilaza' waliobakia.
Meningitis,
..nilichopendekeza hapo ni a "TACTICAL RETREAT" ili tuweze kujipanga upya ktk kuboresha sekta ya elimu.
..kwa mtizamo wangu ni vema serikali ika-consolidate shule chache kati ya shule za kata, na kuhakikisha shule hizo zinapatiwa nyenzi zote, pamoja na waalimu, ili kuziwezesha kutoa wanafunzi waliofikia viwango.
..baada ya kufanya hivyo serikali sasa inaweza kujipanga upya na kuleta mpango makini zaidi wa UNIVERSAL SECONDARY EDUCATION.
NB:
..nakubaliana na wewe 100% kwamba tusisahau kutoa ujuzi kwa "vilaza" waliobaki.
..kuhusu suala la "vilaza" au "vipanga" mimi naamini every child is special, kinachotakiwa ni wazazi na waalimu kuhakikisha kwamba tunafanya kila tuwezalo kuvumbua kipaji cha kila mtoto/mwanafunzi. mimi nakumbuka shuleni kulikuwa na watoto hawafanyi vizuri darasani tukiwaita "vilaza" but they were very good in sports. Sasa wazazi na waalimu wangeviendeleza vipaji vile leo wangekuwa watu muhimu ktk jamii.