MDAHALO: Elimu ya Msingi iwe miaka 5 halafu Middle School then Secondary na High School...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Miaka ile 5 ya kwanza ya elimu ya msingi iwe ni kwa ajili ya:

Kusoma (Kiswahili na Kiingereza)
Kuandika na Uelewa (comprehension)
Kuhesabu (arithmetic)
Michezo na Sanaa

(Mwaka wa kwanza uwe katika kujifunza kusoma na kuandika - exclusively).

Middle School miaka 2 iwe kwa ajili ya:

Kuzama katika hesabu na lugha
Sayansi, Siasa (Civics) na Sanaa
Character development (kupitia michezo na extra curricular activities)

secondary (secondary education) miaka 2
Miaka 2 ya pure liberal arts (introductory courses)

High School - kuzama katika liberal education na semi specialization. (unafuta combination zilivyo sasa). Mwaka wa mwisho mtoto atakiwe kujua anataka kusomea nini Chuo Kikuu au onother tertiary institution.

Au mfumo gani mzuri zaidi wa kujaribu kudeal na hili tatizo la wanafunzi kufeli sana kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo?
 
kwa hizi IQ zetu wabongo sidhani kama hiyo ni good idea.just imagine katika hiyo miaka saba tu kuna watoto wanamaliza hawajui kusoma wala kuandika,sasa itakuwaje kwa miaka mitano? mi ningeshauri iwe miaka nane kabisa.
 
Miaka saba ni mingi sana kufundisha na kukomaza akili ya mtoto...!

Darasa la pili ni marudio ya Darasa la kwanza (hapa ndiyo huwa stage ya kwanza kufundisha watoto "kukariri"...!)

Darasa la tano ni marudio ya Darasa la nne (hapa ndiyo huwa stage ya pili kufundisha watoto "kukariri"...!)

Tunawapoteza watoto wengi ki-elimu kwa sababu ya kuwafundisha yaleyale kwa miaka minne...!
 
Miaka ile 5 ya kwanza ya elimu ya msingi iwe ni kwa ajili ya:

Kusoma (Kiswahili na Kiingereza)
Kuandika na Uelewa (comprehension)
Kuhesabu (arithmetic)
Michezo na Sanaa

(Mwaka wa kwanza uwe katika kujifunza kusoma na kuandika - exclusively).

Middle School miaka 2 iwe kwa ajili ya:

Kuzama katika hesabu na lugha
Sayansi, Siasa (Civics) na Sanaa
Character development (kupitia michezo na extra curricular activities)

secondary (secondary education) miaka 2
Miaka 2 ya pure liberal arts (introductory courses)

High School - kuzama katika liberal education na semi specialization. (unafuta combination zilivyo sasa). Mwaka wa mwisho mtoto atakiwe kujua anataka kusomea nini Chuo Kikuu au onother tertiary institution.


MM, hata kama utafanya yote hayo swali ya msingi kubwa ni je una walimu wa kutosha wanaoimudu fani yao? Je walimu hawa unawajali kwa kiasi gani?

Mawazo yako hayana tofauti na sera mbalimbali za nchi hii, ni nzuri kimaudhui lakini zinasahau changamoto halisi za utekelezaji wake.
 
Mwanakijiji,

Combination yako iko stagewise oriented than quality of education, kinachotakiwa kuangaliwa labda ni curriculum na syllabus je zina ubora gani. Mimi nafikiri tukazanie kuboresha elimu si kwa kubadili stage (system) bali kuangalia vitu vya msingi kwanza kama walimu, vitabu, madarasa, labs,na facilities zingine, tukifanikiwa hilo kwanza, kubadili stage ni kitu rahisi sana ni kama tunavyobadili mitihani ya form 2 na std 4, maana unaweza kuamuka kesho ukasikia mtihani fulani umefutwa mwingine umeongezwa. Kama curriculum/syllabus ni mbovu combination yeyote ya stage mfano ya sasa 7-4-2 au proposed 8-2-2 au yako 5-2-2+ wont work.
 
mfumo uliopo bado ni mzuri tatizo lipo kwa wasimamizi wa mfumo huu,wazazi na mwanafunzi mwenyewe.
Serikali imechakachua elimu kwa kufanya mabadiliko makubwa ya mitaala yasiokuwa na basis,yaani waziri anaibuka na kusema futa masomo flani lakini msingi wa kuyafuta au kuyaongeza haupo.vitabu vimekuwa vikibadilishwa kila kukicha halafu inaavyoonekana kitabu anachosoma mwanafunzi wa dar ni tofauti na kile anachotumia mwanafunzi wa newala.yawezekana kumeruhusiwa vyuo vingi sana vya kufundisha walimu na kwa bahati mbaya inaelekea vyuo hivi havina mtaala inayofanana hivyo mwalimu akihitimu anafundisha jinsi anavyojua kwa ufupi uwepo wa utitiri wa vyuo vya walimu umesababisha aina na viwango vya ufundishaji kuwa utofauti mkubwa sana.

Kudharauliwa kwa fani ya ualimu ni mojawapo ya chanzo cha mfumo wa elimu kuharibika.leo hii mtu akipata daraja la chini form 4 au form 6 anaona kimbilio la kupata ajira ni ualimu, hakuna anayefaulu vizuri na kuchagua ualimu.
Mishahara na maslahi finyu kwa walimu yameshusha tija ya walimu.hakuna mwalimu wa kumalizia topic jumapili au wakati wa likizo,walimu hawana hamu ya kufundisha!

Utitiri wa shule za english media,hii ni biashara kutoka kenya iliyokuja kuangamiza elimu yetu.vishule hivi uchwara vinatumia walimu kutoka kenya ambao hawajajua mitaala ya kitanzania au mara nyingine vinatumia mitaala ya cambridge wakati tupo tz.

Serikali kwa makusudi au kwa kutokujua imeua kabisa shule za serikali na sasa inaelekea kuua vyuo vya serikali.kuvuruga shule kama mzumbe,ilboru,msalato,pugu na jamii yake imetufikisha sehemu tumekosa shule ambazo ni standard,hapa nitolee mfano wa hospitali kwamba mgonjwa aliyeshindikana hupelekwa muhimbili..
Yuko rafiki yangu wa uganda aliniambia wanafunzi kutoka tanzania ndio wanaojaza shule zao za english media kwani waganda wanaprefer shule za serikali kwa elimu bora.
Kiufupi serikali imeshindwa kudhibiti madhara ya utandawazi.leo hii ukikatiza kwenye vituo vya daladala jaribu kuhesabu matangazo ya '''elimu ya sekondari kwa miaka miwili''' yalivyo mengi na hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kuelezea suala hili.

Walimu ni sehemu ya tatizo kwa sababu wanafundisha wasichokipenda na wasichokijua.

Wazazi wa siku hizi hawafuatilii maendeleo ya mtoto shuleni.wazazi hawana muda wa kufundisha watoto wao.wazazi hawashawishi watoto wao wasomee au wapende fani fulani fulani.

Wanafunzi wa sasa wana nyenzo nyingi za kusomea lakini kutwa atakuwa kwenye facebook,video game,kukariri mashairi ya hussen machozi na tamthilia za amerca kusini.hata hivyo vyote hivi sio tatizo iwapo kuna ratiba inayompatia muda wa kujisomea.

Mwisho napenda kupinga hoja ya mwanakijiji kwa sababu bado hatujajua kiukamilifu ni nini hasa chanzo cha kuanguka kwa wanafunzi wetu.
Nashauri ufanyike utafiti katika maeneo yote yanayohusu elimu ili tujue tatizo liko wapi hii ndio njia pekee ambayo ni sahihi na salama ya kubadilisha mfumo wa elimu nchini,hakuna haja ya kudesa kwa wakenya.
 
Nadhani watu wanamiss point iliyofichika; suala la quality ya elimu linaenda na structure ya elimu hiyo.... mfumo ambao ninaudokeza unapresume kuwa mambo mengine nayo yatabadilika kuenda sambasamba nayo.. Kwangu mimi issue ya quality sasa hivi inakuwa ngumu vile vile kutokana na structure yenyewe ya elimu...
 
Nadhani watu wanamiss point iliyofichika; suala la quality ya elimu linaenda na structure ya elimu hiyo.... mfumo ambao ninaudokeza unapresume kuwa mambo mengine nayo yatabadilika kuenda sambasamba nayo.. Kwangu mimi issue ya quality sasa hivi inakuwa ngumu vile vile kutokana na structure yenyewe ya elimu...

mkuu tunakupata sana.kwangu mimi quality ndio ina matter!!hiyo structure unayosema haikidhi imetumika kwa miaka kadhaa mpaka mwishoni mwa miaka ya tisini ambapo watu wakaanza kupoteza muelekeo.
 
meningitis

Umeongea misingi ya tatizo la elimu yetu, mitaala tofauti, siku hizi kila shule ina mitaala yake syllabus, utakuta leo shule hii inafanya National exam ukivuka barabara tu the next school unakuta nayo inafanya National exam lakini mitihani tofauti what is the meaning of a National exam, i think should be uniform otherwise dont call it national exam.

Tatizo ni pale tulipoanza kubinafsisha elimu tukashindwa kuzi control shule binafsi zilizokuwa zinaleta syllabus zao kwa kisingizio cha English medium schools, walikuwa wanasema mitihani yao wanafanya kwa kiingereza kumbe hata content yake ni tofauti na mitaala yetu.

Tuangalie kwa undani syllabus yetu is it compatible?, tunaposema kwa mfano O' level wanafundishwa Basic Mathematics is it real basic? mwanafunzi anapofundishwa Integration na differentiation (calculus) is this what basic mean in mathematics? Kwa mfano huu, nafikiri nayo inasababisha wanafunzi wengi labda kuchukia Maths, mwanafunzi anategemea kufundishwa Algebra anakutana calculus lazima aogope.

Upande wa serikali as a major education provider inachangia sana kuyumbisha elimu, kuna kipindi Kapuya alifuta masomo ya Biashara na Kilimo (O leve) na michezo mashuleni ni kwa kukurupuka tu without any consultation na stakeholders kama walimu, wenye shule, wanafunzi n.k sijui kama alijua madhara yake.

Kama tunataka kuboresha elimu yetu mimi nafikiri haya ndiyo masuala ya kuangalia zaidi ya stage anazozisema MKJJ.
 
Mwanakijiji
Yote wataongea lakini ukweli elimu ya Tanzania itaendelea kudidimia kama serikali haitachukua hatua za makusudi kuboresha sekta ya elimu, kwanza kabisa ni lazima tuwe na walimu wenye sifa wapewe vitendea kazi vyote muhimu na ni lazima wapewe motisha ili wawe na ari na kazi yao; na wazazi wajihusishe na maendeleo ya watoto wao; sisi tuliosomeshwa na walimu waliokuwa na moyo ndio DIV 4 na 0 zilikuwa ni aghalabu, hapa inabidi siasa ziwekwe pembeni.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Miaka na stage zibaki ka zilivyo, ila wabadilishe mitaala na kupunguza idadi ya masomo ambayo yanakuwa ni mzigo kwa wanafunzi. Wanafunzi waanze ku specialize toka O'level. Kwa mfano kwa system ya sasa mtu anayesoma Sayansi O'level inabidi asome masomo yasiyopungua 'tisa' ikiwapo na somo la history ambalo halitamsaidia, na mwanafunzi anayesoma Arts analazimika kusoma biology.
Mapendekezo yangu kuwe na masomo manne au matano kwa O'level, kwa wanasoma Science wasome Physics, Chemistry, Biology, Math na Geography (ila changamoto itakuja kwenye swala la lugha maana huko primary wanasoma masomo kwa kiswahili) na kwa wanaosoma Art wasome History, Geography, Engl, Kiswahili na Civics
 
Nadhani watu wanamiss point iliyofichika; suala la quality ya elimu linaenda na structure ya elimu hiyo.... mfumo ambao ninaudokeza unapresume kuwa mambo mengine nayo yatabadilika kuenda sambasamba nayo.. Kwangu mimi issue ya quality sasa hivi inakuwa ngumu vile vile kutokana na structure yenyewe ya elimu...
Mzee MKJJ unachofikiria samahani kwa kuingia kwenye mawazo yako ni sawa na kocha wa mpira kubadili formation ya 4-4-2 na kuwa 5-4-1 ili timu ishinde, kitu ambacho hakitasaidia kama wachezaji hawana kiwango kinachotakiwa. Tuboreshe kwanza walimu wetu miundombinu ya elimu sio hawa walimu wa voda fasta mwalimu anakuwa trained kwa mwezi mmoja (manufacturing teachers) ataweza nini hata kama utambadilishia structure.
 
Nadhani watu wanamiss point iliyofichika; suala la quality ya elimu linaenda na structure ya elimu hiyo.... mfumo ambao ninaudokeza unapresume kuwa mambo mengine nayo yatabadilika kuenda sambasamba nayo.. Kwangu mimi issue ya quality sasa hivi inakuwa ngumu vile vile kutokana na structure yenyewe ya elimu...

Heshima yako mkubwa!.Structure hii iliyopo imetumika muda mrefu na kwa miaka kadhaa ilikidhi viwango.Lakini kwa miaka ya karibuni kuna mambo ya msingi hayatekelezwi tofauti na zamani.Tatizo kubwa ni utitiri wa shule za sekondari nchini.Hii inapelekea wanafunzi wanaoenda kusoma shule hizi kukosa uwezo wa kumudu masomo ya sekondari.Dhumuni la shule za sekondari za serikali ilikuwa ni kuwaendeleza wale wanafunzi walioonekana wana uwezo na hatimaye wafike elimu ya juu na kusomea utaalamu wa fani mbalimbali.Lakini siku hizi sekondari imekuwa ni kwa wote kitu kinachopelekea wengi wa wanafunzi kuwa wabovu.Zamani ukipata nafasi sekondari ya serikali unamringia yule ambaye amelazimika kwenda private lakini siku hizi ni kinyume.

Pia ubora wa walimu nalo ni tatizo.Kupeleka watu waliopata alama za chini(eg IV 27/28 Kwa shule za msingi) kunafanya walimu kukosa uwezo zaidi wa kuwaendeleza na kuwafundisha wanafunzi.Elimu ya ualimu pekee haiwezi kutupatia walimu bora unless huyo mwalimu mwenyewe alikuwa ni mwanafunzi bora akiwa shuleni.Hata kwa upande wa sekondari ni form six wasiofit sehemu zingine ndio ambao hukimbilia ualimu(si wote).Serikali ipandishe hadhi ya ualimu kwa kuchagua best students kwenda teaching huku ikiboresha maslahi ya walimu na hatimaye kufanya fani ya ualimu iwe na ushindani kwa wote wanaofanya vizuri mitihani kushindania nafasi za ualimu.Tukiwa na walimu bora na wanafunzi bora level ya sekondari tutapata wataalam bora wa fani mbalimbali na hivyo kuiinua elimu yetu.


Shule zote za kata ambazo zipo urban zigeuzwe kuwa vocational training centres na zile za rural ziwe vyuo vya kilimo.Shule za sekondari zibakie angalau mbili kwa tarafa na zichukue wanafunzi waliofaulu kama zamani.Waalimu waliopo mashuleni wapewe mafunzo zaidi ili kufiti kuwa walimu wa shule hizi chache za sekondari.Wazalishwe walimu wengi zaidi kwa vituo hivi vya ufundi na kilimo ili kuimprove handcrafty na agriculture kuimarisha uchumi wa nchi kwa kupata wahitimu wanaoweza kujitegemea.Tatizo sio structure ila ni investment kwenye elimu.
 
Mwanakijiji, Kilimo kinafiti wapi kwenye hiyo structure yako? Kumbuka hii ni secta ya msingi sana katika nchi yetu.
Pili naomba uipanue hiyo structure inanibana sana kuchangia. sababu, kama nilivyoshindwa kuelewa kilimo kitafit wapi hapo juu, pia sielewi computer itafiti wapi, nadhani ile knowledge wanayopewa watu kwenye secretarial courses inatakiwa ikamilike kwenye advanced level.

Nadhani katika kosa ambalo mimi naona nilamsingi zaidi ni hapo kwenye kuweka kiswahili na kiingereza kundi moja. Katika dunia ya sasa Kiingereza ni cha muhimu kuliko kiswahili, Kutokukipa kiingereza first priority ikiwezekana kuachana kabisa na kiswahili, kiswahili kibadilishwe kuwa technical subject kama mathemetics na masomo mengine ya sayansi. Asije mtu akanibeza katika hili, sababu mambo ya kufundisha kiswahili kwa misingi ya kudumisha mira na desturi zetu ni potofu sababu kiswahili sio sehemu pekee ya mira na desturi zetu mbona hayo mambo mengine ya mira na desturi zetu yanakandamizwa why not kiswahili. Zitenganishe pls.

Mada nzuri sana hii panua structure
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom