Mchungaji zuzu

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
345
118
Baada ya Zuzu kumaliza kozi ya uchungaji na kufanya kazi kwa muda, siku moja akakutana na wachungaji wenzake 2 wakaamua wafanye toba wenyewe maana kila siku wanawafanyia toba waumini wao.

Basi ikawa hivi;
Mchungaji Zumbukuku:Jamani mie naomba mniombee niweze kuacha hii dhambi maana ninakula sadaka za waumini hapa nilipo natafutwa kuna hela hawazioni.

Mchungaji Zezeta :mhm afadhali wewe, mie mwenzio yangu ndo balaa naomba tu mniombee mwenzenu maana wale wanawake wote mnawaona mle kanisani kwangu nimeshatembea nao, yaani hivi ninavyowaambia waume zao washajua na wananitafuta.

Mc​hungaji Zuzu ilivyofikia zamu yake akawa anaondoka zake,

wenzake wakamwambia "vipi tena mwenzetu unaondoka wakati hatujamaliza"
akawajibu" mhmh mwenzenu mie ndo kabisaa naomba tu mniombee niweze kuacha hii dhambi maana mwenzenu mie ni mbea,yani hivi nilivyoinuka nilikuwa naenda kuwambia waumini wenu"​.
 
Dah u made ma day manake kuna m2 kaniboa kwa hl namsamehe.Thnx braza.
 
Ni kweli kabisa dhambi kubwa kuliko zote ni umbea.

hapo unanichanganya kwani viongozi wangu wa dini wamenifunza dhambi zote ni sawa afu leo unaniambia dhambikubwa kuliko zote ni umbea
 
Mh jock za kidini na imani za dini zingepungua humu jamvini ningefurahi sana
 
Tuwe wakweli,dhambia ya uzinzi na wizi haiwezi kuzidi dhambi ya umbea. Na haya madhehebu ya dini yanayochipuka kama uyoga tuwe makini nayo.
 
Back
Top Bottom