Wewe unahatari tena hatari ya kujaribu kuchota dhambi ambayo haina sababu. Haya mambo ya imani ni ya mtu binafsi na kamwe hakuna imani ya ujumla ndiyo maana nawashangaa sana watu wanaosema (sisi ni watu tuliookoka) Ni vigumu sana kuokoka kama kikundi anayeokoka ni mtu mmoja kwa binafsi yake anayeweza kuwaweka kwenye kundi ni Yesu Kristo, uwelewe wazi kuwa mzee huyu alikuwa anafanya uinjilisti kwenye eneo la kijijini lililogubikwa na umaskini, kitu kilichowafanya wakazi wa eneo hilo wawe na shida za kudumu, kwa vyovyote vile kama mchungaji huyu alikuwa amesimama kwenye zamu yake lazima alikuwa anamzigo wa kuwaombea hawa watu ili mungu awafungue na kuwatatulia matatizo hivyo basi naamini dhamira na mzigo uliokuwa ndani ya mzee huyu ndiyo ilimfanya apewe neema hiyo. mchungaji huyo amezuia dawa hiyo isitoke kiholela kwani inaweza kutumiwa vibaya na kuleta athari, hata hivyo hajaficha mti unaotumika, hata wewe ukitaka nenda kauchemshe hujazuiwa, aidha uelewe wazi kuwa mti huo una sumu kali ila muujiza uliuopo mpaka sasa hakuna mtu aliyedhurika na dawa ya mti huo hivyo kufanya jambo hili liwe muujiza. Hata hivyo kwenye haya mambo ya imani ni vema kuchukua tahadhari unapojaribu kuyazungumzia kwani unaweza ukajikuta unaingia kwenye shida usiyoitegemea sioni kama una hoja yenye mantiki unapohoji kwanini mzee huyo hafiki mikoani. Kuna watu wanasafiri kwenda Nigeria kuombewa na TB Joshua sasa ungehoji kuwa kwanini watu wanaenda huko wakati hapa tanzania kuna watumishi kibao.Sipingi na wala sitapinga wagonjwa kumiminika kwenda Loliondo kupata dawa ya magonjwa sugu inayotolewa na Mch. Mstaafu Ambilikile. Lakini kama anayosema ni kweli basi Mungu aliyempa uwezo huo atakuwa ni Mungu ambaye mm simuabudu. Tujiulize ni Mungu gani atampa mtu kuponya watu na kumzuia mtu huyo kuitoa dawa hiyo nje ya mazingira yale aliyopo? Mungu wa Mch. Mwasapile ni mchoyo kwa sababu kulazimisha dawa hiyo itolewe eneo moja tu ni uchoyo na upendeleo. Najiuliza wagonjwa mahututi walio kule Mtwara wataweza kusafiri mpaka Loliondo kupata hiyo dawa. Uchoyo mwingine wa Mungu wa Mwasapile ni kwamba kama dawa yake haiwezi kutolewa na mtu mwingine then Hospitali zetu za kule Songea haziwezi kunufaika nayo. Je mchungaji akipatwa na umauti sasa ni nani atatibu badala yake kama ni yeye tu anaruhusiwa na huyo Mungu wake kutibu? Bado Yesu alipewa uwezo wa kuponya lakini alikuwa anaweza kutoa uponyaji popote duniani? Nahitimisha kwa kusema Mch. Mwasapile ni mungu-mtu na anatumia matatizo ya binadamu vibaya na naapa kuwa Mungu wa Mchungaji huyu siwezi kumuabudu.