Mchungaji wa CUF? Seriously tunahitaji majibu toka CUF!

Status
Not open for further replies.
Mkuu siku hizi dini na hasa UDINI ni siasa. Mkutano wa jana umedhihirisha hivyo bila chenga.

Mimi sikubaliani na wewe! Fahamu kwamba CUF, CCM au CDM wanavyoitisha mikutano ya siasa hawaendi makanisani au misikitini kuhamasisha waumini wa dini kuhudhuria mikutano. Udini ni propaganda inayopandikizwa na kundi la watu fulani ili malengo yao ya kisiasa yatimie.

Tusitumie muda mwingi kuwashughulisha watanzania na mambo ya Udini,ukabila,ukanda. Chama cho chote makini chenye sera za maslahi ya Taifa kitapata ufanisi tu, nafikiri mafanikio hayo umeanza kuyaona kwenye baadhi ya vyama, 2015 utaona matokeo yake
 
Nimefikiria kama Mtatiro ni Mkiristo safi asingekubali kufanyiwa dhiaka ktk dini yake, basi kama kuna ushahidi kuwa ni Mchungaji fake basi wampeleke mahakamani.
Mtatiro ni muislam safi, hana uhusiano wowote na ukristo. Kama hujui uliza uambiwe sio kukurupuka tu na kuwavika watu imani zisizowahusu.
 
Kama kuna mistake kubwa ambayo CUF waliifanya jana ni ku-Fake jambo tena kwenye issue sensitive kama dini.

Haitaji hata kujiuliza, kwa muumini wa kikristo hasa mkatoliki alichokiona ni maigizo ya dhihaka kwa imani yake, haya ndio makosa waliyofanya CCM pia wakati wa mkutano wao pale jangwani kwa ku-Fake tukio la watu kurudisha Kadi za Chadema.

It is primitive and very poor political tactic.
 
Kuna picha ya mtatiro ana sigda niliwahi iona humu,mwenye nayo atuwekee tafadhali.
Mbona zipo nyingi tu tena nyingine akiwa anaswali!

Bahati mbaya hapa natumia simu ya mchina, nikiweza nitajaribu ku-upload hizo picha but zingine mpaka nipata concent yake kwa kuwa ni mtu ninafahamiana naye.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom