Mchungaji wa CUF? Seriously tunahitaji majibu toka CUF!

Status
Not open for further replies.
Nimefikiria kama Mtatiro ni Mkiristo safi asingekubali kufanyiwa dhiaka ktk dini yake, basi kama kuna ushahidi kuwa ni Mchungaji fake basi wampeleke mahakamani.

Mkuu ushahidi hauwezi kupatikana kwa kuwa kila kukicha kuna watu wanajiita wachungaji wengine mitume na wengine manabii. Mungu pekee ndiye ajuae nani fake na nani si fake sisi wanadamu hatuwezi kamwe kujua hayo mambo.
 
wekeni clip tumtathmini huyo mjungaji...vilevile tunatakiwa tujue ametoka dhehebu/kanisa gani...wasifu wake...
 
Wakuu mi nilikwepo eneo la tokio kwanza yule mchungaji alipo kuwa akisali watu walikuwa wanacheka kwa kejeri,wengine walikuwa wanakimbizana yani kwa kifupi mambo yalikuwa hayaeleweki ila ilipo fika zamu ya shee kila m2 alikuwa kimya na kuheshimu sala
 
Clip ya nini wakati ,maswali yamelekezwa kwa CUF. CUF walikuwa na wapiga picture wao.Hao akina ritz kazi yao ni kupoteza attention na wapo tayari kuweka uongo wanaoweza uita majina mazuri wapendayo.

CUF ndio wanapoteza credibility hapa kam ahawana majibu, kama hawana mahusiano mazuri na makanisa kiasi cha kuweza omba mchungaji credible ni tatizo, kama wameamua kwenda kwa kanjanja ni tatizo, kama wameamua fanya mizaha wakidhani ukristu ni mwepesi nitatizo....hakuna Mchungaji anayefanya mambo ya catholics na catholics hawana mchungaji.CUf waje toa majibu hapa
 
Jaribu tena baadae. Kalale kwanza.

Kulala lazima nilale lakini huwa sinyamazishwi kwa na kelele labda hujasoma my footer.Distractions ni trick primitive sana hata wanyama na ndege hutumia kulinda watoto.Sidhani kama unaweza zitumia vyema kama hao wanyama na ndege wanao cheza na adui ili awakibize wampeleke mbali na kiota/shimo la wanao.CUF lazima wapitie scrutin kila siku kama CDM ndio waingie/na kubaki vichwani mwa watu.
 
Weka kando yote ,waliohudhuria wamevunja recodi ,sio CCM wala shoga yao Chadema ,nilijua tu CUF itatoa somo.
 
Awe neutral kwenye mkutano wa siasa? Yaani kwamba kaalikwa tu akaombee mkutano na kuondoka ili awe neutral! Wangemuita Mch. Rwakatare labda.

Kama alikuwa ni ulamaa na kaamua kuudhihaki ukristo basi damu yake na iwe juu yake na hadi vizazi vyake vya saba. Mungu mwenye enzi ataupatiliza uzao wake kwa kuwa
Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu; na wote tuseme
amin.
Hui hofu juu ya Dini nyingine itatuweka pabaya hivi karibuni. Arusha masheikh feki walipandishwa NMC grounds na hakukua na thread ya kulizungumzia hilo, hebu tujadili
yanayojenga yaliyoletwa na yatokanayo na mkutano huo na kama yana tija kwa taifa! Udini hautatufikisha mahali.
 
Weka kando yote ,waliohudhuria wamevunja recodi ,sio CCM wala shoga yao Chadema ,nilijua tu CUF itatoa somo.

Distractions ni trick primitive sana hata wanyama na ndege hutumia kulinda watoto.Sidhani kama unaweza zitumia vyema kama hao wanyama/ndege wanao cheza na adui ili awakimbize wampeleke mbali na kiota/shimo la wanao.Wao hufanya vizuri sana kwa vile ndio njia ya kuokoa haki ya kuishi kwa wanao.Sasa nyie wenye hila hamuwezi ifanya vyema kwa vile mmechukua nafasi ya adui na si mzazi wa viumbe.

Kwa ujumla kondoo hufaahamu bwana wao na asiyeingilia mlango huwa hamwakilishi mwenye kondoo.
 
Hui hofu juu ya Dini nyingine itatuweka pabaya hivi karibuni. Arusha masheikh feki walipandishwa NMC grounds na hakukua na thread ya kulizungumzia hilo, hebu tujadili
yanayojenga yaliyoletwa na yatokanayo na mkutano huo na kama yana tija kwa taifa! Udini hautatufikisha mahali.

"Waovu wawili hawafanyi mwema hata mmoja"
Sasa ulisubiri hii thread ije ndipo uulize?Kwanini usijiulize nini kimewaogopesha CUF kumwita credible pastor anayeaminika kuwa ange represent kundi lake vyema?

We kaulize kama watu wengine mikoani waliogomea sensa na hawana kundi la kuandamana kama nao waliachiwa ,ungekuwa umefanya la maana.

Kama wew ni msemaji wa CUF basi toa maelezo na si kuvuruga thread.
 
CUF wapo wapi watupe majibu tuone kama tunahitaji kuhoji vingapi kati ya wanavyotuletea ni fake?Au lini wataacha fake..tuna maswali mengi.Ikiwepo hiyo ya sijui $ ngapi kwa kila raia...prof hajasema kama ni endelevu au? na imapct yake kwa uchumi wa nchi ,familia na watu binafsi..nadhani kafanya tafiri za kutosha kwenye hilo.Pia watu kuishi kwa kupokea hela ya bure fixed amount no matter how much efforts you do/don`t put to earn it, kama ina afya kwa ustawi wa nchi na jamii?

Nategemea kafanya sana research katk hayo maeneo aliyobobea na anaweza tuagizia library ya kuweza pata hizo reports kam si kudownload.
 
kama ikithibitika si mchungaji halali basi wahusika wachukuliwe hatua kali. lakini pia sitashangaa siasa za sasa mithiri ya msafara wa mamba kwani kenge hawakosekani humo.
 
CUF wamekuwa wakiponzwa na vijimipango vidogo vidogo sana!.. Wapo tayari kubamiza kichwa ukutani kwa sababu wameumwa na chawa. CUF ina maamuzi yanayoweza kuidhalilisha daima!..
 
Katika mkutano wa CUF leo mchungaji aliyesimama kufungua kwa ibada ameonyesha mapungufu mengi.

Ila mojawapo ni haya kwanza hajui tofauti ya madhehebu. Catholics hawana mchungaji, na hivyo mchungaji kufanya ishara ya Catholics ni shida kwa kanisa lake.

Pia alikuwa akionyesha tabasamu linaloweza tafsiriwa kuwa hakuwa serious au alikuwa akiigiza na hivyo na kusubiri muda wa kumaliza.

Muda wote kulikuwa na watu wakicheka wakati wa maombi ya ufunguzi, na "mchungaji" alipokuwa akishuka alipeana mikono na watu kwa staili inayoweza tafsiriwa kama pongezi kwa "umejitahidi igiza"

Mchungaji aliyesimama kaonyesha mambo yenye kuleta maswali haya:

-Je huyu hakuwa mchungaji feki?

-Na kama ni mchungaji kabisa ,basi atakuwa ni kanjanja na hivyo kuongeza swali. Kwanini CUF-wachague hiyo njia?

-Je CUF wana ni thabiti ya kuweka uwakilishi wa kidini wenye heshima katika maombi ya ufunguzi?

Ningependa sana CUF waje weka wazi hii habari.

Mods: Naomba msiitoe hii. It's serious.
Kwa hiyo huamini kwamba mchungaji anaweza kuwa mwana CUF?.. isipokuwa anaweza kuwa chama gani?... Hivi kweli ndio uwezo wako wa kufikiri yaani mchungaji hawezi kuwa CUF kukaribishwa CUF halafu unasema watu wengine wana Udini sio wewe...
 
Mbona mnaweweseka sana na CUF ndo wamerudi ulingoni nyie wachungaji wa chadema tafuteni pakutokea.Mchama unaowachukia waislamu ni bora ufee
 
Kwa hiyo huamini kwamba mchungaji anaweza kuwa mwana CUF?.. isipokuwa anaweza kuwa chama gani?... Hivi kweli ndio uwezo wako wa kufikiri yaani mchungaji hawezi kuwa CUF kukaribishwa CUF halafu unasema watu wengine wana Udini sio wewe...

Unaruhusiwa kusoma ulicho quote kwanza kabla ya kukimbilia.Angalia status yako hapa JF(verified user) sijui senior expert etc.kma husomi between line kuna shida.Mimi sijaongelea kuhusu mchungaji kuwa mwana CUF. Ila behaviour yake tangu alipopanda jukwaani, na jinsi alivyosali ni ushahidi kuwa hakuwa hata Mkristu.

Mkandara sikia kama ulivyosoma footer yangu mimi ni radical haswa na Real mzalendo na si wa kubeep.napata kichefuchefu kuona watu kama wewe mnaweza andika vizuri kwa uafasaha halafu hamjui mnachoandika wala kusoma, na mara nyingine intentionally mnataka brainwash ,slander , seduce watu, .Hapa nipo busy nafanya kazi,ila napenda sana kufanya multiple things at the same time,kufanya brain yangu isiwe idle kama task haioccupy brain vya kutosha.

Kama vile umekuja kwa kunipania.Nadhani ungeweza saidia toa majibu logical kwa cuf.
 
Mbona mnaweweseka sana na CUF ndo wamerudi ulingoni nyie wachungaji wa chadema tafuteni pakutokea.Mchama unaowachukia waislamu ni bora ufee

To maelezo halafu ujibu maswalai mengine kabla ya kujifanya kuwa chama chako ni bab kubwa.Wala hakuna aliyeleta udini hapa.Hapa ni kutaka kujua huyo mchungaji mliyempandisha jukwaani.Kama CUF imapungukiwa moral standards hivyo basi tujue cha kufanya.

Kama hawana majibu ya haya mambo vipi wataweza jibu matatizo ya wananchi?CUF wanacheza ,mkutano wa leo una mapungufu mengi sana.Sioni cha kujivunia kwani kwa watu makini wanaona kuwa CUF hata ulingini haifikia bila kutelza na kurudi katik uvundo.Chama kinachoamini kugawa hela, sijui kama kina kichwa.Hembu watupe majibu hapa tuone kama CUF kina kichwa au ndio CCM wameshakifunga ndani ya gunia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom