Mchungaji Rwakatare naye atoa tamko...

Nilikuwa natazama Taarifa ya Habari ya Saa mbili ITV,, nikashangaa kusikia Walokole wa Mama Rwakatale wakisema Wanamshukuru Mungu kwa kuweza kutoa baraka zake kipindi chote cha uchaguzi kwa kufanikisha uchaguzi wa Huru na Wahaki,,

Mimi sina tatizo kwa kupitisha misa ya shukurani kwa Mungu kwani hakukuwa na riots na maandamano ya kijinga kwani uchaguzi umekwisha Salama lakini Hofu kubwa ipo kwenye Haki hapa..

Hivi nikweli hawa walokole wanajitambua kweli kabisa jamani
Nahisi hawajitambui na wala hawajui kuwa Tanzania ninini kinaendelea kuhusu uchaguzi huo

Huyo mama ni mnafiki,Anajua anachokifanya anatumia njia hiyo kufunika bihashara zake za madawa ya kulevya,hakuna ulokole hapo.Mungu Tusamehe.
 
hivi shehe MTOPEA yupo wapi?....... mwacheni huyu mama....... mtakusanyika dhidi yake...mtatawanyika kwa njia saba......! mtachimba shimo mumnase mtatumbukia wenyewe....!(HIZI NI AHADI MUNGU ALIWAHAIDI WAMCHAO KWA BIDII)
 
Hao ndio maajent wa yule mwovu wanaofanya kazi kwa kutumia jina la YESU.
 
Ifu yu kanti drinki milki, hwai kipu a kaoooooo!!

huyu maza ni aina ya pepo wanaoishi kufanya maombi ya kishetani kuwaombea mafisadi.

Mods, naomba msinipige ban. Pepo ni neno la kawaida tu.
 
Eti jamani, kwani si hata Dokta Slaa ni mchungaji?

Mhe.Dar Es Salaam

You have to think 2ic before you post anything! Soma hizi points 2 hapa chini.

  1. Dr.Slaa alisomea mambo ya Canon Law yanahusiana na Sheria na taratibu za Dhehebu la Kanisa Catholic. Lakini Dr. Slaa aliachana na kulitumikia Kanisa akaingia kwenye Siasa ili aweze kuwatumikia Watanzania wote kwa ujumla wao badala ya kutumikia kanisa la Catholic peke yake.
  2. Dr. Slaa hata kama angeendelea na huduma ya Kusimamia na Kuendesha Catholic Church bado anaruhusiwa na Maandiko yaani Biblia kumtumikia Mungu MAANA YEYE NI MWANAMME. Kwa taarifa yako mwanamme hazuiliwi kuhubiri Injili. Na bado he can do both, politics and Bible Ministry when he likes. Hakuna kizuizi. Je,Uliwahi kumsikia Askofu Macarios wa Cyprus?
 
Inawezekana wamemuachia Mungu ili ashughulike na hila zozote zilizofanyika za kuchakachua matokeo.
 
Mchungaji Rwakatare amenakiliwa na gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM akirejea kauli yenye utata ya kuwa JK ni chaguo la Mungu..........kauli hii ni tata ukizingatia upo ushahidi wa ya kuwa NEC haikufuata katiba ya JMT katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi wetu..........Ibara ya Na. 41(5) inayoitaka NEC kufuata taratibu za sheria ya uchaguzi haikufuatwa.................................swali kwa kada wa CCM ambaye amejibanza kwenye viti maalumu ni je hivi Mungu anachagua watu ambao wanawadhulumu wapigakura haki yao ya kimsingi ya kuchagua viongozi wawatakao?

Kwa lugha nyingine, je Mwenyezi Mungu anaafiki dhuluma kwenye jamii............huyo ni Mungu wa wapi huyo? Na Mchungaji Rwakatare alikutana lini na Mungu kama siyo anajikomba kwa JK kwa kumkashifu Mwenyezi Mungu pale ambapo anapomwingizia maneno kinywani mwake ambayo hakuyasema.............

Ushauri wangu kwa Rwakatare..........mpe Kaisari yaliyo yake lakini hakikisha kwanza unampa Mwenyezi Mungu yaliyo yake na haya elezea ukweli kuwa ulijitungia..........

One of the ancient philosopher contended: " Through people God made you a King and through the same people God may overrule your Kingship" Kwa maana hiyo Mungu kwa kutumia watu wake, (wa aina zote) kumweka JK Raisi wao. Sioni ajabu hapa labda kuanzia leo kupiga kura iwe dhambi
 
KULINGANA NA MAANDIKO MATAKATIFU MAMA RWAKATARE SIYO MCHUNGAJI . ANACHOFANYA MAMA RWAKATARE NI KUPINGANA NA NENO LA MUNGU. KWA HIYO ANACHOONGEA NI PUMBA TUPU. RAIS KIKWETE ATAKUWAJE CHAGUO LA MUNGU WAKTI AMEINGIA KWA KURA ZA WIZI? ASIDANGANYE WATU HAPA. PAMBAF KABISA! SINA HAKIKA KAMA ANA MUME.

BIBLIA INASEMA ,''SIMPI RUHUSA YA MWANAMKE KUFUNDISHA WALA KUMTAWALA MWANAMME............''.....MWANAMKE NA ANYAMAZE KATIKA KANISA..........''KAMA KUNA NENO NA AMWULIZE MME WAKE NYUMBANI MAANA NI AIBU KWA MWANAMKE KUNENA NDANI YA KANISA.....'' TUNASOMA BIBLIA TAKATIBU KUTOKA VITABU VYA 1 TIMOTHEO 2:11-14 NA 1 CORINTHIANS 14:34-38...

1 TIMOTHY 2:11-15

[11] Let the woman learn in silence with all subjection.
[12] But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence.
[13] For Adam was first formed, then Eve.
[14] And Adam was not deceived, but the woman being deceived was in the transgression.
[15] Notwithstanding she shall be saved in childbearing, if they continue in faith and charity and holiness with sobriety.

1 CORINTHIANS 14:34-37

[34] Let your women keep silence in the churches: for it is not permitted unto them to speak; but they are commanded to be under obedience, as also saith the law.
[35] And if they will learn any thing, let them ask their husbands at home: for it is a shame for women to speak in the church.
[36] What? came the word of God out from you? or came it unto you only?
[37] If any man think himself to be a prophet, or spiritual, let him acknowledge that the things that I write unto you are the commandments of the Lord.

Hii nimeipenda sana Huyu mama Rwakatale ninqani ajifanye yeye ni Mchungaji,, na sisi mbona hatutambui Mwanamke kuwa mchungaji? na maandiko yetu hayaruhusu kuwa yeye ni mchungaji?
 
Jamani tumuache mama wa watu ana haki ya kutoa shukrani kwa uteuzi wake, nadhani atakuwa kajichanganya kidogo si unajua ulimi hauna mfupa?

Tumwacheje wakati anawakamua 'kondoo' wake bila huruma! Habari ni kwamba kila akipanda madhibahuni kuhubiri lazima avae nguo mpya tena ya bei mbaya mno na harudii kuvaa nguo hiyo. Badala ya kutumia sadaka za kondoo wake kwa maendeleo yao na ya kanisa yeye anazitumia kujirembesha! Shame on her really! Utategemea nini cha maana kutoka kwa mtu kama huyo?
 
Siku hizi Kusafisha mafisadi na ufisadi dili. Yaani ukitaka upate pesa ya haraka simama jukwaani au kwa vyombo vya habari sema CHENGE NA LOWASA NI WATU SAFI WALIONEWA NA BUNGE. Nakwambia fasta kama ulikuwa na nyumba haijaisha atakuja kandarasi kuimalizia bila hata ya wewe kuwepo nyumbani. Hii ndo dunia zambi kubwa ya unafiki ndo imekuwa kimbilio la wenye tamaa. Nina uhakika Lwakatare anaijua zambi anayoifanya lakini kwa kuhisi kuna kichaka ameamua kujifichia hapo. Hongera Lwakatare utatughlibu lakini Mungu haghilibiwi
 
Mi sijui hilo Tamko aliwatoa kwa watanzania au kwa waumini wa Dini yake? maana ssis wakristo hatumtambui Rwakatalwe Kama Mchungaji
 
Yeye ni mtafuta/mtumia fursa kufanikisha malengo yake ya kujipatia fedha na umaarufu katika jamii. Kidunia, CCM inampa mtu nyenzo hizo na kidini, ukristo hasa wa kilokole ni dili kubwa sana ndani na nje ya nchi nyakati hizi. Nabakia kustaajabu tu uwezo wake wa kujitwisha mizigo mikubwa hivyo ya unafiki ili kufikia malengo yake. She must be a very very lonely person. Sijui kama ataimudu hali hiyo kwa muda mrefu bila kutetereka nafsi na akili. Whatever your take, that's a superwoman for sure!
 
What a shamefully mchungaji,yani kweli ukombozi umekaribia ,wale wote wanaojivua ngozi za fisi na kujivika ngozi za mbuzi wanaanza kuumbuka,kama ningekuwepo hapo kanisani,ningefanya wale wabunge wa chadema walivyofanya kwa jk,ni nge tumia demokrasia,kufikisha ujumbe kwa waumini yakuwa,nakutangaza hali ya hatari,mafisadi wameanza kuwatumia viongozi wa dini,nahisi mwisho wa dunia umekaribiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
1. Huyu mama vipi??? Au labda anachukua mfano wa Yakobo aliyejitwalia baraka za Esau mzaliwa wa kwanza tena kwa hila na akabarikiwa na Mungu!! Je, Mungu hakuliona hilo?? Mbona hajalikemea?? Au ulikuwa mpango wa Mungu??. Au Biblia ilichakachuliwa na Waandishi??
Kama ndio ndivyo basi licha ya kuwa mwanamke hafai kuwa mchungaji, lakini kama ni kwa mfano huo basi hata wakristo wa leo wanamkubali yakobo mwana wa isaka na ameambatanishwa na kizazi cha Yesu. Na ni kweli mungu alimbariki!!

Natoa hoja.

 
Msimlaumu huyu mama mnatakiwa mjue kwamba ameshaamua kuingia kwenye siasa and politics especially within ccm is all about hypocricy! Kwa hiyo sishangai kumuona mama rwakatare ameacha kuhubiri ukweli na kugeuka MNAFIKI na kuanza kupotosha waumini wake na umma kwa ujumla. Nasema ASHINDWE NA ALEGEE KWA JINA LA YESU KRISTU!
 
1. Huyu mama vipi??? Au labda anachukua mfano wa Yakobo aliyejitwalia baraka za Esau mzaliwa wa kwanza tena kwa hila na akabarikiwa na Mungu!! Je, Mungu hakuliona hilo?? Mbona hajalikemea?? Au ulikuwa mpango wa Mungu??. Au Biblia ilichakachuliwa na Waandishi??
Kama ndio ndivyo basi licha ya kuwa mwanamke hafai kuwa mchungaji, lakini kama ni kwa mfano huo basi hata wakristo wa leo wanamkubali yakobo mwana wa isaka na ameambatanishwa na kizazi cha Yesu. Na ni kweli mungu alimbariki!!

NACHELEA POST ZANGU KUFUTWA KILA MARA NIKIPOST. I REALIZED THAT LONG AGO. LAKINI NATIZAMA MAMBO KIUHALISIA NA KUTOA MAWAZO MBADALA. SUPER INTELLIGENT HUH!! IS WHETHER ADMINISTRATOR LIKE IT OR NOT BUT IF YOU HAVE FREE MIND YOU LIVE FREELY AND HAPPILY!!.

 
Aagh! Mama Lwakatare tena, we mama, give us a break plz! huyu si ndiyo yule aliwalipa pesa wale watoto wawili waliojifanya wameanguka pale kanisani kwake kutoka kwenye ungo eti walikuwa na bibi yao wanaenda kuwanga wakitokea Kilwa, uchunguzi baadae ukabaini kumbe ni watoto wa hapo mwananyamala na walikula dili na mama Lwakatare....sh****type! Huyu mama hana lolote wala msimshangae kumfagilia JK, nae ni walewale tu! anaishi kwa ujanja ujanja tu hapa mjini, anatumia advantage ya ujinga na kukata tamaa kwa waumini wake kuendeleza porojo na dhulma kwa mgongo wa INJILI, mie nasema siku Mungu akishuka halafu akaweka maovu yetu wazi, watu wengine sijui tutasimamia wapi! God have mercy on us!

Duh, mengine sikuwa nayajua.... kweli JF ni Home of Great Thinkers
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom