Mchungaji Rwakatare kuhojiwa kwa kushindwa kutangaza mali

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mchungaji Rwakatare kuhojiwa kwa kushindwa kutangaza mali Na Agnes Mwaijega MBUNGE wa Viti Maaluma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatare, anatarajiwa kuhojiwa leo na Baraza la Maadili kutokana na kushindwa kuwasilisha fomu ya tamko kwa tume ya maadili juu ya mali anazomiliki. Kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizoainishwa na Tume ya maadili, kiongozi yeyote wa umma ni lazima ajaze fomu za matamko kila inapofika Desemba na kwamba kushindwa kufuata utaratibu huo kwa kiongozi yeyote ni kosa linalostahili hatua za kisheria. Pamoja na kuitwa mbele ya baraza kueleza sababu za msingi za kushindwa kujaza fomu hizo na iwapo maelezo yake hayataridhisha, Mchungaji Rwakatare anaweza kuchukuliwa hatua zaidi za kisheria. Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili Jaji Damian Lubuva, alisema madhumuni ya kuwaita viongozi mbalimbali ambao wameshindwa kuwasilisha matamko ya mali wanazomiliki kwa wakati ni hatua muhimu katika kuhakikisha kila kiongozi wa umma anaheshimu na kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na tume ya maadili ya viongozi wa umma. Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, Bw. Silvatory Machemli, ambaye aliitwa jana na baraza hilo, alisema sababu za kushindwa kujaza fomu hizo kuwa ni pamoja na tume ya maadili ya viongozi wa umma kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha fomu hizo zinawafikia. Alidai alishajaza fomu za matamko na kuzirejesha na kushangaa kuitwa tena kudaiwa. "Nashangaa kuona naitwa mbele ya baraza kuulizwa fomu ziko wapi wakati nilishajaza na sijawahi kupata barua zilizotumwa na tume ya maadili kupitia kwa spika kunikumbusha kujaza fomu hizo kama sijajaza," alisema. Alisema utaratibu unaotumiwa na tume ya maadili wa kumpa spika wa bunge barua za kuwakumbusha viongozi ambao hawajaza fomu siyo mzuri na hazikupaswa kupitia kwa kiongozi huyo, kwa kuwa hajui ambao hawajajaza fomu hizo kwa wakati, hivyo hutoa tangazo bila kusema nani anatakiwa kujaza. "Utaratibu huu siyo mzuri na wala tume haipaswi kumtumia spika wakati mhusika yupo," alisema mbunge huyo. Vyombo vya habari jana viliwataja wabunge wengine wanaotakiwa kuhojiwa kuwa ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe, Riziki Lulinda, Devotha Likokola, Felix Mkosamali na Kapteni John Komba.
 
2 Maoni: Anonymous said... kama wabunge wanajaza fomu za maadili mbona hatujawahi kusikia mafisadi wanachukuliwa hatua ya kuwa na mali nyingi? June 14, 2011 11:00 PM Mussa said... Yaani binada akipewa milima 2 ya dhahabu,atataka na wa 3 pia uwe wake. Tukumbuke kuwa kuna KUFA jamani! Tutaviacha tu. June 15, 2011 11:53 AM
 
Mchungaji Rwakatare atoampya Baraza la Maadili Wednesday, 15 June 2011 22:25 Nora Damian MBUNGE wa Viti maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare jana alitoa mpya mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma alikofikishwa kujieleza kwa nini hakujaza fomu ya kutangaza mali zake, baada ya kudai kuwa shetani ndiye amepoteza fomu hizo. Dk Rwakatare alisema hayo wakati akihojiwa na mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Katika utetezi wake, Dk Rwakatare alitumia maneno kama pepo, shetani na Mungu yalitawala.Mchungaji huyo alijitetea kuwa yeye alijaza fomu hizo na kuziwasilisha katika ofisi za bunge lakini hajui nini kilichotokea hadi fomu hizo zisifike kunakohusika. “Mambo mengine ni shetani tu, shetani ana nguvu sana kila mahali yuko,”alisema Mchungaji huyo na kuongeza kuwa:“Kazi yenyewe ya kujaza fomu ni ya dakika 10 tu sio kwamba unafanya mtihani Cambridge hivyo halikuwa zoezi kubwa kwangu hadi mimi nishindwe kujaza,”alisema.Alisema yeye hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba angeweza kuwa mmoja wa watu ambao hawakujaza fomu hizo kwasababu alizijaza na kuzirejesha Ofisi ya Bunge. Dk Rwakatare pia alionyesha nakala ya fomu hiyo anayodai kuijaza na kudai kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika fomu hizo na kwamba kila mwaka amekuwa akizijaza.“Tutaamini vipi kama nakala hiyo ni halali pengine ulikuwa nayo nyumbani na jana ukaitoa copy. Je hukusaini kokote wakati uliporudisha fomu hizo?" alihoji mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Akijibu swali hilo Dk Rwakatare alisema wakati wa kuchukua fomu hizo ilikuwa lazima kusaini lakini kurudisha haikuwa lazima. Baadhi ya mahojiano baina ya Mchungaji huyo na Mwanasheria huyo wa baraza yalikuwa hivi:Mwanasheria: Unasema ulijaza fomu, mbona hazikufika kwetu?Rwakatare: Hilo litakuwa ni pepo tu. Mimi nilirejesha na Mungu ni shahidi.Mwanasheria: Umeng’ang’ania shetani hivi huyo shetani ni nani?Rwakatare: Ni roho chafu ambaye kazi yake ni kuharibu na kufanya mambo yaende vibaya.Mwanasheria: Sasa huoni kama anakupeleka pabaya?Baada ya swali hilo, Mchungaji Rwakatare hakujibu kitu alikaa kimya. Mwanasheria huyo aliliomba baraza hilo litupilie mbali utetezi wa Mchungaji huyo kwa sababu amekiri kutofanya ufuatiliaji.Hata hivyo akizungumza nje ya baraza hilo na waandishi wa habari, Dk Rwakatare alisema tangu uanze mchakato wa fomu hizo, hajasafiri kwenda mahali kokote na kwamba anashangaa kwanini hawakumpigia simu kumuuliza kama alijaza au la.“Mimi sijasafiri kwenda kokote na wala nilikuwa sina wasiwasi kabisa kwa sababu nilijaza fomu na kuzirejesha, wangeweza kunipigia simu na ningeweza kuja,”alisema. Alipoulizwa na waandishi wa habari haoni kama kuna haja ya kuwakemea mashetani, Mchungaji huyo hakujibu kitu aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka.Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mpanda Vijijini kupitia CCM, Moshi Kakoso naye alifikishwa kwenye baraza hilo jana na kuitupia lawama ofisi ya bunge kwa madai kuwa alijaza fomu na kuzikabidhi kwa wahudumu wa ofisi hiyo.“Sijafurahia kuitwa katika baraza hili ni kitendo ambacho si kizuri. Naomba nipewe nafasi ya kujaza fomu nyingine ili nitekeleze sheria za nchi,”alisema Kakoso.Alisema yeye hana mali za kutisha kiasi cha kumfanya ashindwe kujaza fomu hizo na kulalamikia ofisi ya bunge kuwa haiko makini katika utunzaji wa kumbukumbu. Mbunge huyo pia alipoulizwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Damian Lubuva kuhusu kumpa muhudumu wa ofisi ya bunge nyaraka muhimu kama hizo, alijitetea kuwa hilo ni bunge lake la kwanza na kwamba alidhani kuwa alikuwa sahihi kumpa muhudumu huyo. “Hata mawasiliano ya barua kuja Mpanda yanachukua muda mrefu sana na kutufanya sisi wengine tuonekane tumekiuka sheria,”alisema Kakoso.Baada ya kusikiliza utetezi wa wabunge hao, Jaji Lubuva alisema watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.Baraza hilo litaendelea leo ambapo Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, diwani kutoka Geita Elias Okomu na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga Edwin
 
Sielewi anaogopa nn kutaja mali zake ambazo doubtlessly alizipata kabla ya kuwa mbunge.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom