Mchungaji Rwakatare amtaja Shetani kujitetea

duh: sanaa 100%. Ila mchungaji usisahau kuorodhesha na ma cheni,mahereni,ma bracelet ya dhahabu uyavaayo tukiwa kwenye ibada.
 
Jamani nyie waongoza ibada hivi kweli shetani anaweza kuhamisha faili la mtu ? Mchungaji Rwakatare acha kum-tangiblize shetani.
What I (a born again) know is that satan is spirit(s) and some of the evils are done out of our conscience.
Lie not, trust in Jesus that ye be saved.
 
tulishasema DINI na SIASA viwe tofauti
tukasema pia BIASHARA na SIASA ziwe tofauti

sasa haya ndiyo matokeo yake, unamhoji mtu kwa nini then yeye anakwambia mpango wa shetani wa kupoteza form - wapi na wapi!!!
 
Kwa wanawake wa CCM morogoro wanaweza kujua nini alikifanya alipokuwa anautafuta ubunge wa viti maalumu kupiota wanawake wa CCM moro. Kweli shetani anamkabaa koo vibaya. Ninawaonea huruma waumini wake.
 
Nimeona jina la mhe.Mbowe, kati ya waliosalia kuhojiwa, akiwa pamoja na John komba. Mhe. mbowe km kiongoz wa kambi ya upinzan unapaswa kuwa mfano wa kuigwa na si kushutumiwa kutofata sheria na taratibu za mahal husika, hii itawapa mwanya wapinzani wako wasiasa kupata nafasi ya kuchafua sifa yko km kiongoz wa chama cha upinzan dhidi ya wapiga kura wako.
 
Shetani bwana yaani form zote hakuziona kaziona za mchungaji, mmhhh ashindwe na mama siku nyingine kemea kabla hujazirudisha maana ataiba tena huyo. sanaa inapofika mpaka kwa watumishi ni balaaa.
 
Huyu mama ni msanii tu,mtaalam wa ku brainwash watu apete.Haoni aibu kujiita mchungaji?
 
Hapo kuna watu wa aina mbili. Wanaoamini kuwa shetani yupo na anatenda, na wasioamini. Kifupi shetani ni kiumbe cha roho, kama vile malaika wengine, hivyo hatuwezi kuwaona kwa macho. Shetani ni kiumbe halisi, ukisoma katika Biblia , Ufunuo 12:7 - 12.
Shetani alitupwa hapa duniani, na ana hasira kali, akijua ana kipindi kifupi aje kuangamizwa pamoja na wafuasi wake.

Ndio maana kuanzia 1914 hali inazidi kuwa mbaya katika dunia nzima!!!!! Tuliozaliwa baada ya 1914, huenda isiwe rahisi kuona tofauti, lakini kwa kusoma historia ya dunia kabla ya 1914, tutaona wazi.
Mama Rwakatare hakukosea kumtaja shetani, ila kamtaja kwa watu ambao wanahitaji ujuzi zaidi juu ya shetani.
Vilevile shetani anaweza kufanya kazi kwa mtumishi wa Bunge(ambaye inasemekana aliipokea form ya mama Rwakatare), pia anaweza kufanya kazi kwa mama Rwakatare(ambaye anadai aliikabidhi form). Mimi na wewe hatujui, Mungu na mama Rwakatare ndio wanaoujua ukweli.

Kama tungeruhusiwa kutoa maoni, binafsi ningemshauri Mh. Lukuvi, amsamehe kwa kuwa huenda ni mara ya kwanza.
Vilevile ningemshauri mama Rwakatare aachane na mambo ya siasa, kwa kuwa Biblia inaita "ukahaba wa kiroho" (Ufunuo 17:5) kuwa katika siasa za ulimwengu, hapo hapo kiongozi wa dini.
Mengine nitayasema baada yan kusikiliza mchango wenu wana JF. Nisiwe mbinafsi kuchonga saaanaaaa!!!!
Ciao.
 
hata wachungaji ambao wanaaminiwa na kondoo wao wanafikia mahali wanadanganya hadharan jaman! nina mashaka na uchungaji wake
 
Huyu ameamua kusingizia shetani..kwani mtu akishakuwa mzembe kisingizio inakuwa hasa shetani..lakini mwingine akikosea anasema uvivu/uzembe nk.
 
Huyu ameamua kusingizia shetani..kwani mtu akishakuwa mzembe kisingizio inakuwa hasa shetani..lakini mwingine akikosea anasema uvivu/uzembe nk.

Huyu mama alikuwa anataka ubunge ili apate kuendeleza shughuli zake za kibiashara. Niliwahi kusema toka mwanzo hafai kuwa mbunge kwani ni mfanyabiashara anayetumia jina la uchungaji vibaya. CCM lakini hakuna wa kumwambia kitu maana wafanyabiashara ni wengi.
 
duh: sanaa 100%. Ila mchungaji usisahau kuorodhesha na ma cheni,mahereni,ma bracelet ya dhahabu uyavaayo tukiwa kwenye ibada.

Pole sana kwenye Ibada - unakwenda kuabudu au kuangalia hivyo ulivyotaja hapo juu??? Angalizo: ukiwa kwenye ibada elekeza mawazo yako kwa Yesu na sio walivyo-vaa wengine - hapo ni pamoja na Mch. Mheshimiwa G. Lwakatare.

Mradi una-abudu - Mungu atakupa na wewe siku moja - kazana kumwabudu Mungu -
 
imebidi nicheke tu maana nimekumbuka wakati niko form tw0 seminarini miaka hiyo ku....ilitokena nikaumia mguu wakati wa mechi then jumatatu nikaavaa viatu na kuingia darasani ..sasa wakati nikiwa darasan mguu ukauma sana na nikaamua kurudi chumbani kuvua viatu ili nivae open shoes...sikuomba ruhusa kuingia room...na ndipo baba ngombera (rector)akanikamata na liponiuliza nilijibu sikuomba ruhusa ya kuingia room..aliponibana sana nikasema nilipitiwa na shetani.....nakumbuka alinipa adhabu ya kukaa chini ya mwembe toka asubuhi hadji jioni ili nijadili na huyo shetani kwa nini alitoka huko na kunichukua darasanio had chumbani bila ruhusa......

ndipo nikajua shetani wa mtu ni mtu mwenyewe na mawazo yake......

mkuu hapo kwenye green nilikua sijui kumbe ndiyo hivyoooooo!!!!!!!!
 
shetani ana kazi kweli kweli............. mume/mke akifumaniwa shetani kanipitia.............mafile ya wachungaji nayo yanalindwa na shetani................pale tunaposhindwa kuwajibika lawama zinakwenda kwa shetani
 
Hapo kuna watu wa aina mbili. Wanaoamini kuwa shetani yupo na anatenda, na wasioamini. Kifupi shetani ni kiumbe cha roho, kama vile malaika wengine, hivyo hatuwezi kuwaona kwa macho. Shetani ni kiumbe halisi, ukisoma katika Biblia , Ufunuo 12:7 - 12.
Shetani alitupwa hapa duniani, na ana hasira kali, akijua ana kipindi kifupi aje kuangamizwa pamoja na wafuasi wake.

Ndio maana kuanzia 1914 hali inazidi kuwa mbaya katika dunia nzima!!!!! Tuliozaliwa baada ya 1914, huenda isiwe rahisi kuona tofauti, lakini kwa kusoma historia ya dunia kabla ya 1914, tutaona wazi.
Mama Rwakatare hakukosea kumtaja shetani, ila kamtaja kwa watu ambao wanahitaji ujuzi zaidi juu ya shetani.
Vilevile shetani anaweza kufanya kazi kwa mtumishi wa Bunge(ambaye inasemekana aliipokea form ya mama Rwakatare), pia anaweza kufanya kazi kwa mama Rwakatare(ambaye anadai aliikabidhi form). Mimi na wewe hatujui, Mungu na mama Rwakatare ndio wanaoujua ukweli.

Kama tungeruhusiwa kutoa maoni, binafsi ningemshauri Mh. Lukuvi, amsamehe kwa kuwa huenda ni mara ya kwanza.
Vilevile ningemshauri mama Rwakatare aachane na mambo ya siasa, kwa kuwa Biblia inaita "ukahaba wa kiroho" (Ufunuo 17:5) kuwa katika siasa za ulimwengu, hapo hapo kiongozi wa dini.
Mengine nitayasema baada yan kusikiliza mchango wenu wana JF. Nisiwe mbinafsi kuchonga saaanaaaa!!!!
Ciao.

Bado ni vigumu kuthibitisha mawasiliano ya Mungu na Rwakatale na ushuhuda wa Mungu kwamba fomu zilipelekwa bungeni na ndipo tunasema utetezi wa kisiasa hauwezi kukidhi matakwa ya Mungu mwenyezi..... kachanganya dini na siasa majibu hayana budi kuwa ya kisiasa.... mwishowe nao mafisadi watajitetea kwamba Mungu ndiye anajua kwamba hawajatuibia.
 
Back
Top Bottom