Mchungaji Mwasapile kuhamisha utoaji tiba

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,513
19,998
Mchungaji Mwasapile kuhamisha utoaji tiba Send to a friend
Monday, 21 March 2011 21:06
0
digg

Mchungaji Ambilikile Mwasapile
Kizitto Noya na Venance George,Loliondo
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapile amesema hivi karibu atahamisha utoaji wa tiba katika eneo analoishi sasa na kwenda sehemu ambayo itakuwa na nafasi kubwa zaidi, kwa lengo la kupanua huduma na kubadilisha mazingira anayoishi.
Akizungumza juzi mchana kijini hapo, mchungaji huyo alisema yeye si mganga wa kienyeji, bali anatibu kwa miujiza ya Mungu na kusisitiza kwamba ili mgonjwa apone anatakiwa kuwa na imani katika huduma hiyo.
"Nataka nieleze kidogo kuwa mimi si mganga wa kienyeji. Tiba yangu ni miujiza ya Mungu ambaye ameamua kuliweka neno lake katika mti huu ili lilete uponyaji.
Ameamua kuukomesha ugonjwa wa Ukimwi duniani kabisa," alisema mchungaji huyo na kuongeza:
“Kwa wale wanaoumwa Ukimwi wanapokunywa dawa hii wanapona kabisa. Tiba itaanza kujidhihirisha ndani ya siku saba. Lakini wadudu hata kama bado watakuwapo, hawatakuwa na nguvu na katika kipindi cha miezi mitatu, wadudu wote watakufa kabisa.
 
Pia akumbuke kulipa kodi ya mapato TRA ,kwani anapata si chini 20 m kwa siku bana
 
huyu ni mganga tu.wote waliokwenda kwake wako njiani kuchukiwa na wenzao kwakuwa kwa muda wote huo walikuwa wakiambukiza tu.huyu ni mchochezi......mganga wa kienyeje na mpiga ramri.
 
huyu ni mganga tu.wote waliokwenda kwake wako njiani kuchukiwa na wenzao kwakuwa kwa muda wote huo walikuwa wakiambukiza tu.huyu ni mchochezi......mganga wa kienyeje na mpiga ramri.
Tena ukikaa vibaya atakupiga bao huyu babu,maana unaonekana muoga,unamuogopa,wakati ni mkombozi aliyetumwa na Mungu kufanya kazi ya mungu!!
 
huyu ni mganga tu.wote waliokwenda kwake wako njiani kuchukiwa na wenzao kwakuwa kwa muda wote huo walikuwa wakiambukiza tu.huyu ni mchochezi......mganga wa kienyeje na mpiga ramri.

Kwakuwa umezoea kwenda kwa waganga unafikiri kila kitu ni ugangaaa tuuuu
 
Back
Top Bottom