Elections 2010 Mchungaji mwanjala kule Mbeya vijijini vipi?

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Wakuu mlioko mbeya tujulisheni maendeleo ya yule Mch. mwanjala aliyebebwa uchaguzi mdogo. Au pia anapumulia mashine? Na mpiganagi Sambwe Shitambala hatujapata updates zake, tafadhali zileteni hapa jamvini.
 
Mchungaji anafanya vizuri kuliko ambavyo alifanya kwenye uchaguzi mdogo.

Aliposhinda kaitumia vizuri nafasi hiyo kuchapa kazi na sasa wananchi wake wanamtaka.
 
Mchungaji anafanya vizuri kuliko ambavyo alifanya kwenye uchaguzi mdogo.

Aliposhinda kaitumia vizuri nafasi hiyo kuchapa kazi na sasa wananchi wake wanamtaka.

unauhakika? upo mbeya wewe?
 
kuna sehemu nimeona maandishi yanasema Mchungaji yuko hoi, tusubiri wakuu walioko mby watuletee updates.
 
Mch. Mwanjale ana wakati mgumu bado yuko ICU! Nguvu ya Sambwee Shitambala bado ni kubwa, wale wananhi wa Mbeya Vijijini wamekataa kudanganywa na mfano hapa juzi alipokuja Mgombea Mwenza wa CCM, Dr Bilali, wananchi wa Ilembo waligoma kusombwa kwenye malori kwenda kumsikiliza, waliendelea na shughuli zao.

Mpaka sasa kwa Mbeya, CCM wameshapoteza Majimbo ya Mbeya Vijijini na Mbozi Magharibi, labda itokee miujiza. Hayo ni majimbo ambayo CHADEMA wanao uhakika wa asilimia 80, wanachotakiwa kufanya viongozi wa CHADEMA ni kuwekeza kwenye majimbo hayo kwa kuwasaidia wagombea wao ili waweze kuwafikia wapiga kura kila kona ya majimbo hayo.
 
unauhakika? upo mbeya wewe?

Mbeya mjini na Mbalalai CHADEMA wana nafasi nzuri ya kuchukua kuliko Mbeya vijijini. Hakuna anayejua nini kitatokea siku ya uchaguzi ila kama unafuatilia Mbeya vijijini haiongelewi tena na sababu ni hiyo kwamba pamoja na CHADEMA kuwa na mgombea mzuri sana lakini mchungaji ameweza kuwafurahisha wananchi wa Mbeya vijijini kwa hicho kipindi ambacho amekuwa mbunge.
 
Back
Top Bottom