Ni kigeugeu,wanajuwa hana madhara makubwa kwa serikali,lakini anayo madhara kwa upinzani kwasababu anatumika kuzigawa kura za upinzani na hatimaye ccm kushinda.Shida ni kwamba haaminiki huyu,na anapenda sana pesa kuliko hata hayo ya kuwakomboa watanzania,yeye anapiga kelele ili mkono uende kinywani,rejea ile issue ya RA,kule Mara kwenye uchaguzi wakati wa kifo cha Wangwe pamoja na ile kesi aliyoifunguwa eti amekamatwa makalio yake.Huyu ni pesa tu zinamzidia hata uzalendo.wenyewe wanasema hana madhara ndio maana huwa wanamwachia
ngoja tusubiri kesi yake dhidi ya askofu mokiwa
andika zaid kama hivi watu wakaelewa:
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi, dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.
Akizungumza na mtandao huu baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".
huyu mtikila ni jembe lakini nashindwa kuelewa ni kwa nini inakuwa ngumu sana kumwingiza kwenye mapambanao na makamanda wenzake,jamaa anafaa sana kutetea anachokiamini,wapi Kayinga msaidizi wake,nakumbuka enzi zile alikuwa mchungaji pale shule ya uhuru Kayinga alikuwa habanduki ubavuni mwake