Mchungaji Msigwa atakiwa kutoa Uthibitisho wa Madai yake Bungeni leo

watoe kwanza maamuzi ya lema vs pinda ndio msigwa nae apeleke ushahidi na sio kuwatishia 2.
Mkuu umenena vema. Ni vema spika akatoa maamuzi ya ushahidi wa Lema ili watu tujue kama Lema alisema uongo ama Waziri Mkuu ndiye aliyesema uongo. Bunge haliwezi kuwa linaomba uthibitisho kwa matamushi yaliyotolewa hadharani lakini uthibitiho na maamuzi havitolewi hadharani. CHADEMA wadai maamuzi ya uthibitisho wa Lema vinginevyo mambo ya kutaka uthibitisho itakuwa ni kupoteza muda wa bunge na wabunge.
 
Mimi nilihesabu nikachoka

msafara.JPG
Thanx sir/madame
Lukuvi shule hana na inaonekana anabifu na kamanda Msigwa that is why alikuwa kimbelembele kuomba utaratibu kwa mwenyekiti. Elimu yake ndogo itayagharimu magamba coz alikurupuka tu kutaka uthibitisho bila kujua aliyokuwa anayaongea Msigwa hata mtoto wa shule ya msingi angeweza kuthibitisha.
 
...........Kwa hakika hatuna serikali...tuna wahuni waliojikusanya kufanya mambo yao wanavyotaka,inaonekana hawa wamejipanga kuangusha nguvu ya CDM......
 
Chadema kuna vichwa bana..wasomi wachache magamba yana ha ha,..ile mbaya 2015 lazima kieleweke.
 
Jamani hivi ikitokea siku moja spika wa Bunge la Tanzania Mh. Anne Makinda akabadilishana na Spika wa Bunge la Kenya, Mh. Marende ili Makinda aendeshe bunge la Kenya japo kwa siku moja na Marende aendeshe la Tanzania kwa siku moja katika sprit ya EAC, mnadhani nini kingetokea kwa mama Makinda? Kwa jinsi wabunge wa Kenya wanavyochachafyana kwenye bunge huenda spika wetu akakimbia kwa kushindwa kuongoza bunge!! Kinachotokea kwenye bunge letu ukilinganisha na kinachotokea kwenye Bunge la Kenya, ya kwetu ni cha mtoto!!
 
Kuhusu msururu ni kweli nakumbuka nilikuwa tz kipindi icho na ni kweli kuyahesabu mpaka nikachoka ila nilichokea kwenye gari la 32 na tulikaa zaidi ya 2 hrs kungoja mheshimiwa apite
 
hivi jamani naomba kuuliza bunge la jamhuri ya tanzania, wabunge wa chadema wanafikia idadi ya 250?
Wamelifunika mno bana. Napendekeza idadi yao ipunguzwe ili kubalance equation.
.
 
Jamani hivi ikitokea siku moja spika wa Bunge la Tanzania Mh. Anne Makinda akabadilishana na Spika wa Bunge la Kenya, Mh. Marende ili Makinda aendeshe bunge la Kenya japo kwa siku moja na Marende aendeshe la Tanzania kwa siku moja katika sprit ya EAC, mnadhani nini kingetokea kwa mama Makinda? Kwa jinsi wabunge wa Kenya wanavyochachafyana kwenye bunge huenda spika wetu akakimbia kwa kushindwa kuongoza bunge!! Kinachotokea kwenye bunge letu ukilinganisha na kinachotokea kwenye Bunge la Kenya, ya kwetu ni cha mtoto!!

Ndo maana Wakenya wanatudhalau sana.
 
hivi jamani naomba kuuliza bunge la jamhuri ya tanzania, wabunge wa chadema wanafikia idadi ya 250?
Wamelifunika mno bana. Napendekeza idadi yao ipunguzwe ili kubalance equation.
.

Na mimi nashangaa. Hivi wabunge wa CUF wapo au walienda holiday wote?
 
Ushauri wangu kwa mchungaji; Waulize ni nani kafukuzwa kazi au yuko gerezani kwa kuua watu Arusha na Mara. Kama hakuna huo ni udhibitisho tosha kuwa serikali inaua watu wake.
 
Mch Msigwa ni kichwa balaa IRINGA huwaambii kitu kuhusiano na MSIGWA,Mpaka sasa tangia kaingia barabara mbili zimetengenezwa vizuri,mradi wa maji taka umekamilika,maji safi kufikia mwezi wa 9 mwaka utakuwa nao umekamilika.BIGUP MSIGWA,VIVA CHADEMA
 
Bungeni kumeniboa, watu hawana la kuchangia juu ya bajeti ila vijembe tu vya uvyama. Msigwa ana wakati mgumu, mara serikali imeua, ana kesi mbili za kuthibitisha mauaji na matumizi ya msafara, nadhani kunachumvi kazidisha, haijawahi tokea barabara kufungwa hadi masaa 5.
Kaka mimi naishi Iringa ni kweli barabara ilifungwa masaa matano,na juzi tena alivyokufa mama Makinda,barabara kutoka IPOGORO,kupitia SAMORA,kwenda KIHESA mpaka kwenda IKULU ilifungwa kwa masaa mawili.
 
Hv askari sio serikali jamani..sasa wanataka uthibitisho upi? Askari wameua liko wazi sana..nadhani kuna shinikizo toka nje ya bunge jamani.
 
Kuna haja ya Chadema kutafuta mbinu mbadala ya kukabiliana na hujuma za kiti cha spika ANNA MAKINDA
 
Hv askari sio serikali jamani..sasa wanataka uthibitisho upi? Askari wameua liko wazi sana..nadhani kuna shinikizo toka nje ya bunge jamani.

Serikali ni dola na dola ina vyombo vya mabavu navyo ni pamoja na polisi. Sasa kukana kwamba polisi si serikali ina maana serikali inajikana!! Tunakoenda watavikana vyombo vyote vya serikali sijui itakuwaje hapo!!!
 
Mimi ninakushangaa sana wewe unaesema mchungaji hana akili,kazi ya mchungaji unaijua? Kukemea maovu, mchungaji kakemea maovu,kasema kweli,na kuhusu wzr mkuu kutumia magari 50 na ndege mbili ,ujue wzr mkuu ni mnafiki,hawezi kataa shangingi, alafu msafara gharama zake zikawa sawa na gari alilokataa, nasema huyo mtoto wa mkulima anatuzuga 2,
 
Lukuvi anaendelea kutoa ufafanuzi wa kuhusu madai kuwa magari yamewahi kusimama kwa muda wa masaa 10 na pia kuwa na msafara wa magari 52 Iringa na ndege 2 katika msafara wa Waziri Mkuu katika ziara yake Iringa ambayo anayataja kama matumizi mabaya ya Rasilimali za Umma...Hebu tazameni Bunge kama mpo karibu na TV kuna mambo hayapo sawaMhagama: Anaongea kwa jazaba kali kumwelewesha Mchungaji nini cha Kufanya kwa kumtaka kuthibitisha ama kufuta kauli yake kama alivyotakiwa katika muongozo wa Mh. LukuviMchungaji: Anathibitisha kuwa madai yake ni kweliMhagama: Anamwambia Mchungaji sawa na kuwa utaratibu utafuatwaAnapigwa utaratibu tena kwa kusema kuwa Mbunge wa kwanza Mwanamke si Ana Makinda walikuwepo akina Bini Titi Mohamed na kwamba inaonekana mchungaji hakusoma vizuri takwimu alipokuja katika siasa awe makini asije kuwapoteza kondoo wake (Hili la nini sasa)Wadau tazameni mambo haya kuna kampeni nzito hapa
Kuthibitisha! ukweli? Ukweli ni nini? Nani mwenye mamlaka ya kuuthibisha? Anatumia misingi na vigezo gani kuupima ukweli?
 
Back
Top Bottom