Mchungaji Msigwa afunguka bungeni; uchumi hauombewi bali wazinzi

baajun

Senior Member
May 19, 2012
199
6
https://www.facebook.com/chademadiaspora

MCHUNGAJI MSIGWA, MBUNGE IRINGA MJINI AFUNGUKA BUNGENI-UWOGA, NGONJERA, MANENO YA USWAHILI, KUJIPENDEKEZA,UNAFIKI VINAHARIBU TAIFA LETU.

AKILI YEYE MCHUNGAJI HAOMBEI UCHUMI- UCHUMI UNAKWENDA KWA PRINCIPLES SIO MAOMBI. WANAO OMBEWA NI WAZINZI, WANAO FUMANIWA NA WAKE ZA WATU NA MAPEPO-UCHUMI HAUOMBEWI NI PRINCIPLES- DAMN IT!

ASEMA CCM WAMECHOKA-NI WAO WAMETUWEKA KWENYE MATATIZO HAYA NA BADO WANA THE SAME LEVEL OF THINKING.

AMQUOTE Albert Esteen" PROBLEMS CANNOT BE SOLVED BY THE SAME LEVEL OF THINKING THAT CREATED THEM"

https://www.facebook.com/chademadiaspora
View attachment 56883https://www.facebook.com/chademadiaspora View attachment 56884 View attachment 56884
 
Msigwa ametoa speech nzuri sana leo.
amesema maneno ya khanga, woga na unafiki haufai wakati idadi kubwa ya wananchi wakiwa kwenye tabu.
 
Kuombea uchumi si jambo baya. Katika makanisa yetu kila mara tunauombea. Tunachoomba ni Mungu kuwafungua watu ufahamu na kuwapa ubunifu, maarifa na nguvu ili waweze kuzalisha na kujiletea maendeleo. Jambo baya ni kubweteka na kufikiri muujiza utakuja bila kuushughulisha ubongo wako kubuni la kufanya (kwa msaada wa Mungu) na hiyo mipango unayokuwa nayo kuiweka katika matendo. Maendeleo hayahitaji mtu mvivu wa kufikiri au mvivu kufanya kazi.
 
Tena akamnukuu Apostle Paul aliposema, asiyefanya kazi na asile wala hakusema asiyefanya kazi aombewe. Kwa hiyo wavivu wote wanyimwe chakula. CCM tuwanyime kura ili wakose kula.
 
Ha ha ha, hakika hapo amemsema Mwigulu Nchemba. Watu wanajua kuumbua!
 
attachment.php
MWIGULU%2BNCHEMBA.jpg

Msigwa amjibu Mwigulu
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amejibu pendekezo la Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba la kutaka wapinzani waombewe, akisema hakuna kanuni yoyote ya uchumi inayosema Serikali ikiendesha mambo isivyo yanafanyika maombi.

Badala yake, alisema
yeye ambaye ni mchungaji huwa wanaombea wazinzi na watu waotembea na wake za watu, na si matatizo ya kiuchumi.

“Inashangaza sana kuona watu wanaunga mkono bajeti…, kila mwaka deni la taifa linaongezeka na sasa limefika Sh20 trilioni, fedha ambazo ukizigawanya kila Mtanzania atakuwa anadaiwa Sh400,000” alisema Msigwa.

“Nilivyokuwa naona wabunge wamevaa suti na wanachangia hoja bungeni nilipenda jambo hilo na kutamani siku moja niwe mbunge, lakini baada ya kuingia bungeni nimegundua kuwa hakuna kitu.”

Alisema bunge hilo hivi sasa halieleweki na kwamba mbunge mwenye elimu ya kutosha akisimama kuchangia hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa darasa la pili.

“Yaani mbunge profesa akisimama kuchangia hoja huwezi kumtofautisha na mtoto wa darasa la pili, watu wenye akili, akili zao wameziweka mfukoni na kuweka ushabiki wa vyama mbele, tumekuja bungeni kumaliza matatizo sio kuongeza matatizo” alisema Msigwa.

Huku akitumia mifano ya wanasaikolojia mbalimbali Msigwa alisema ni aibu kuona Watanzania wanazidi kuwa maskini harafu kila mwaka yanayozungumzwa ni tofauti na yanayotendeka.

“Ufikie wakati wabunge tutambue kuwa tumekuja hapa bungeni kuwatumikia wananchi, Watanzania waliotuchagua wanateseka na wabunge hapa bungeni mnazungumza maneno ya khanga tu,” alisema Msigwa.

Kwa staili hii kuna haja ya Mchungji Peter Msigwa kuwa na chmba ya confession chamber pale bungeni, huenda kuna wabunge wanaofanya uzinzi na kutembea na wake watu.
 
Nimeipenda hii, katika watu nilio wadharau ni huyo mwigulu .kwanza anajiona amesoma kuliko watu wote hapa TZ , pili ana madharau sana , na mwisho hajui hata kujenga hoja .
 
Hata wale mababu wanaozini na vijukuu kama anavyofanya huyo tumbo tumbo na kale katoto kanakoozea segerea wanastahili maombi.
 
Nimeipenda hii, katika watu nilio wadharau ni huyo mwigulu .kwanza anajiona amesoma kuliko watu wote hapa TZ , pili ana madharau sana , na mwisho hajui hata kujenga hoja .
Katika watu wanaoongoza kuchukiwa sasa hivi Tanzania ni pamoja na huyu jamaa Mwigulu Nchemba, kalewa sifa vibaya mno anaona kununua madawati na kupeleka kwenye mashule kwa fedha zisizo ndiyo kumsaidia mwananchi, ifike mahali hii tabia ya wabunge kugawa fedha au kusema natoa fedha kutoka mfukoni kusaidia wananchi kwa shughuli za maendeleo ikome, siyo jukumu la mbunge kutoa fedha za maendeleo! something must be done with this crazy ideas. Kasoma lakini hajaelimika, bahati mbaya zaidi CCM wakampa cheo cha uweka hazina kwa hiyo anajiona yeye ndiye mwenye chama, ni zaidi ya Nape sasa hivi, hata katibu mkuu hamfikii achilia mbali kutudharau watanzania. "Mwigulu, you must control your thoughts for the sake of your leadership".
 
Uzinzi noma, hasa taifa likiwa officially linakutambua kama wewe ni kinara wa uzinzi Tanzania
 
Katika watu wanaoongoza kuchukiwa sasa hivi Tanzania ni pamoja na huyu jamaa Mwigulu Nchemba, kalewa sifa vibaya mno anaona kununua madawati na kupeleka kwenye mashule kwa fedha zisizo ndiyo kumsaidia mwananchi, ifike mahali hii tabia ya wabunge kugawa fedha au kusema natoa fedha kutoka mfukoni kusaidia wananchi kwa shughuli za maendeleo ikome, siyo jukumu la mbunge kutoa fedha za maendeleo! something must be done with this crazy ideas. Kasoma lakini hajaelimika, bahati mbaya zaidi CCM wakampa cheo cha uweka hazina kwa hiyo anajiona yeye ndiye mwenye chama, ni zaidi ya Nape sasa hivi, hata katibu mkuu hamfikii achilia mbali kutudharau watanzania. "Mwigulu, you must control your thoughts for the sake of your leadership".

Si hilo tu, bali kila anakopita wenye wake zao wako makini kutokana na tabia yake aliyoonyesha alipokuwa kwenye kampeni kule Igunga ingawa funikafunika haiachi harufu na inzi kurukia mzoga.
 
Msigwa ametoa speech nzuri sana leo.
amesema maneno ya khanga, woga na unafiki haufai wakati idadi kubwa ya wananchi wakiwa kwenye tabu.

Mbona mimi nilimsikia akinukuunukuu watu walioishi miaka ya 1800 bila kutoa mchango mbadala. Kisha nikamsikia akisema tu kwamba kuna vipaumbele ambapo wao wachungaji wanatoa kipaumbele kuwaombea wazinzi.
 
Back
Top Bottom