Mchungaji Gwajima Kuueleza Umma Kesho kuhusu Mkenya wa Ulimboka

Ukitulia na kufikiria kwa undani sana unaweza kuona hii picha kwamba imetengenezwa kati ya polisi na huyo mchungaji. Subirini mtaona
 
mchungaji naye huyo yupo kwenye system! kesho mtasikia majibu yake! kama kova tu,sema yeye ataanzia mwisho kuja mwanzoni!:spy:

Nakuunga mkono mkuu. Hapa kuna mchezo unachezwa, wajinga ndo waliwao
 
Sasa jamani,tangu lini taarifa za kiintelijensia zikatolewa kanisani?
mkuu inategemeana na mazingira ya tukio lenyewe,kova alisema jamaa alikutwa kanisani,kwaniyo kanisa nayo inaplay part yake
 
Baada ya mbinu zote kushindwa wanalazimisha watuhumiwa atawageuka watashangaa na kumuua tu stay tune
 
Filam nynine iyo!! Mchungaji umehaidiwa nin? U kuu wa mkoa,au wilaya?? Wadanganyeni wazee wa Ccccmambwe,,so vijana!
 
Ukitulia na kufikiria kwa undani sana unaweza kuona hii picha kwamba imetengenezwa kati ya polisi na huyo mchungaji. Subirini mtaona
..
Yote tisa kumi hatujabeba Maboga Bali vichwa .. Na vichwa vyetu vitajua .. Mbona mechi bado mbichi hata haftaim bado, nisikilize matamko ya Ulimboka akija .. MbonA patajaa..
 
Kova amejichanganya sehemu mbaya .....atajuta kulihusisha hili kanisa la gwajima..tutegemee makubwa kesho...

Alafu hili kanisani ndio alienda Dr Mwakyembe kipindi kile cha Pollonium, Samweli Sitta alivyopewa mic akabwatuka sana, umesahau mkuu?
 
Baada ya kufanya bidii za maksudi kutaka kujua sakata hili la shambulizi la Mwenyekiti Wa Jumuia ya Madaktari TZ, Dr. Steve Ulimboka pamoja Na madai yaliyotolewa Jana Na Kamanda Kova kwamba Kuna Mtu anaedaiwa kuhusika Na utekaji Na shambulizi Hilo aliyejitokeza kujisalimisha ndani ya Kanisa linaloongozwa Mch Josephat Gwajima, pamoja Na utata uliosambaa juu ya matamshi hayo, nimebahatika hatimae kuongea na Mchungaji huyo..

Yeye mwenyewe Kwanza amekiri kusikia taarifa hizo Na pia maelfu ya watu miongoni mwao ni washirika NOa watu wengine nje ya Kanisa nao wamekuwa wakimtafuta ili kupata ukweli Wa matamshi hayo ya Polisi

Mchungaji huyo ambaye Kwa mtazamo ni mpole, mkimya Na mwenye maneno yaliyonyooka, akasema kwamba kuna taarifa aliletewa Na walinzi wa Kanisa kwamba kuna kijana mdogo tu alikuwa akidai yeye ndiye Kinara wa sakata Hilo la kumteka daktari huyo..Na walinzi Hao wakampeleka kituoni Na kumkabidhi huko.. Sasa cha Ajabu ni taarifa ya Jana ya jeshi la polisi juu ya uhusika wa tukio Hili..

Na yeye Kama kiongozi imemgharimu kuwaita Upya wale walinzi Na kupata kutoka kwao taarifa hiyo Na hatimae kesho kwenye Ibaada maalum ataelezea Mkasa wote ulivyokuwa ili jamii ielewe nini kilichojiri..

Nimepitia comment nyingi za watu humu kila Mtu akinadi Na kusema lake, wapo wanaotukana Na wapo wanalalamika Kwa namna wajuao.. Labda nitoe rai kwamba ni vema tuwe Na subira Na kupata Picha kamili hiyo kesho..

Mimi mwenyewe nitawahi mapema Na Kama kawaida ya TAMKO nitawajuza kila kitu..matusi kejeli si mahali pake nadhani kuna kamchezo kanaendelea ambako lazima kafichuliwe sasa.. Jambo Hili si Dogo linagusa masikio ya mataifa mengi Kwa sasa..

..

I simply can't wait...namuamini na kumkubali sana gwajima,ni zaidi ya mchungaji,he talks about life na yote yanayotokea katikati yetu na kuyarelate na mambo ya kiroho..ninaweza tu kumlinganisha na mwakasege kwa ualimu uliotukuka..nakumbuka nilishangazwa one day nikimsikiliza akizungumzia kuhusu ile ajali ya mv spice islanders na kuirelate na nguvu na mipango ya kishetani na mapepo in the most amazing way...najua kesho ni kesho,serikali itatoka damu.wamepotea njia.watajuta.
 
Huyo mchungaji anataka sadaka kubwa kesho.

mkuu yaani hujamumunya maneno umeongea ukweli mtupu. mpka ayatoe kanisani na kama vile kuna mkutano wa waandishi wa habari? kwanini aisende ukumbi wa habari maelezo? akili kumkichwa
 
Mtazamo wangu unafanana na wako. Na taarifa kawapa mapemaaa-Kesho! Wahi Upate Story Live; Usisubiri kusoma katika magazeti ya udaku!

Mkuu.umewahi kufika kwa Gwajima wewe?la hasha,mimi sio mwendaji wa kila siku..lakini unajua ni kwanini serikali imelazimika kumruhusu afanyie huduma tanganyika packers?ni kwa sababu kanisa lake huwa linatapika..sio tu kujaa..its probably the biggest congregation anywhere in Tanzania..na huyu jamaa ni mfanyabiashara pia.I doubt kama ana njaa na hizo shilingi zako chache..we nenda mikono tupu tu,hamna shida.
 
We ndo gwajima?
..
Ha ha Haa.. Haya bwana mkulu, ila Kwa Jinsi Bukoba ilivyo Na wasomi wengi waliotulia sidhani Kama mbichwa huu unatokea pande hiyo.. Nakwambia kesho ntakuwa hapo live nikikujuza kila kinachoendelea halafu wewe unasema mimi ndiye yeye.. Sasa yeye atakujuza vipi Na hapo hapo anaongea.. Vichwa vingine BWANA havipendi kabisa kufikiri
 
Kwa nn ajisalimishe kanisani.tena kanisa la viongozi wa ccm wanalopendelea kwenda
 
Kova amejichanganya sehemu mbaya .....atajuta kulihusisha hili kanisa la gwajima..tutegemee makubwa kesho...

Na mchungaji itabidi afanye jitihada ya ziada. Watu jana wamelaani kitendo cha mchungaji kutotunza siri za watu wanaoungama
 
Tusubiri kesho. Lakini ukweli huyu Mchungaji si pandikizi la CCM maana anawakandia sana hasa JK
 
Nimepita hapo kanisani kwake, sijaona Kanisa wakulu, ni Uwanja tu mkubwa wazi wa kilichokuwa kiwanda cha nyama-Tanganyika Packers LTD, embu Tujuzane watu wanakaaje hapo.. Wakuu au kuna mahema wataweka AMA vipi, nimepita Na mkweche wangu hapo ni wazi tu .. Embu mdau anayeelewa atujuze zaidi..
 
Muvu inazidi kunoga sehemu yakwanza na ya pili tayari sehemu ya tatu ni mchungaji Gwajima usikose ndugu mtazamaji
 
..
Ha ha Haa.. Haya bwana mkulu, ila Kwa Jinsi Bukoba ilivyo Na wasomi wengi waliotulia sidhani Kama mbichwa huu unatokea pande hiyo.. Nakwambia kesho ntakuwa hapo live nikikujuza kila kinachoendelea halafu wewe unasema mimi ndiye yeye.. Sasa yeye atakujuza vipi Na hapo hapo anaongea.. Vichwa vingine BWANA havipendi kabisa kufikiri

Tamko we vipi....Mbona mama Josephine alikuwa kwenye msiba wa regia na alikuwa natupa updates. Unaweza ukawa gwajima na Laptop au Black berry pale madhabahuni. Pili inawezekana unajitolea kutujuza yatakayoendelea hapo kwa gwajima kesho ili Ujue ni mwana JF yupi ataungana na wewe alafu umfanye kama Ulimbokanization..... unaona sasa kumbe kichwa yangu inafikiri. Pia Usibishe kuwa ukienda pale then usitoe sadaka.......utaonekana ni sawa na aliyemteka ulimboka na utakamatwa......kama huna sadaka ni PM nikutumie kwa M pesa
 
Back
Top Bottom