Mchungaji Getrude Rwakatare na posho bungeni - ajibu kiujanja ujanja

consigliori

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
392
89
Leo nimemsikia Mchungaji Getrude akihojiwa na Clouds FM, alipoulizwa kuhusu swala posho bungeni akajibu " siwezi kulizungumzia hili, mimi ni mtu mdogo sana. Zikiwepo nitazichukua zisipokuwepo hazinikeri. Mimi kazi yangu ni kusaidia wananchi na wanawake wenzangu"

Ameamua kuwa neutral ili upande wowote utakaoshinda awe safe.
 
Leo nimemsikia Mchungaji Getrude akihojiwa na Clouds FM, alipoulizwa kuhusu swala posho bungeni akajibu " siwezi kulizungumzia hili, mimi ni mtu mdogo sana. Zikiwepo nitazichukua zisipokuwepo hazinikeri. Mimi kazi yangu ni kusaidia wananchi na wanawake wenzangu"

Ameamua kuwa neutral ili upande wowote utakaoshinda awe safe.

Huyo Rwakatale ni tapeli wa mgongo wa dini kama akina Joshue, upako etc. Wanapandia matatizo ya wanyonge-wagumba, mahanisi, matatizo ya ndoa etc. wakiwaaminisha kuwa nguvu ya mungu itawaondolea yote hayo!!! while has and will never happen on this planet of ours!!!! Yule wa upako anapokea hata senti ya walala hoi pale jukwaani, utapeli hata kwa masikini hawa!!!! knowing for sure kwamba he will never alleviate their sufferings!!!
 
hivi huyu mama huwa anaongea chochote huko bungeni au ndo sampuli ya john komba.
 
Huyu na anaofanana nao kwa staili ya kuingia mjengoni wanatekeleza wajibu wao "VITI MAALUMU" hawajiamini kabisaaaaa!!!
 
[h=2]MCHUNGAJI RWAKATARE AMRITHI SALOME MBATIA[/h]
→ December 18, 2007 →



rwakatarebc.jpg
Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana chini ya Mwenyekiti wake,Rais Jakaya Kikwete,imemthibitisha Mchungaji Dr.Getrude Rwakatare kuwa mbunge wa viti maalumu,kurithi nafasi ilioachwa wazi na marehemu Salome Mbatia aliyefariki Octoba mwaka huu kwa ajali ya gari.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar jana mara baada ya kikao cha kamati kuu,katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi,Bw.John Chiligati,alisema kufuatia uamuzi huo, mchungaji Rwakatare sasa ni Mbunge mteule akisubiri kuapishwa wakati wa mkutano ujao wa Bunge utakaofanyika januari mwakani.
 
[h=2]Monday, March 31, 2008[/h] [h=3]Mama Rwakatare na Misukule[/h] Week mbili zilizopita tuliambiwa na watu walioudhuria ibada kanisani kwa mchungaji Rwakatare na hata vyombo vilireport kuwa kuna watoto wawili (Ramadhani na Yusufu) waliodai kuwa ni misukule na kuwa walianguka wakati maombi na ibada ya nguvu ikiendelea kanisani hapo.Mwandishi wetu wa sayuni alikuwepo ibadani hapo na alituletea habari hiyo mchana huo huo wa jumapili.Ila mlima sayuni tulisita kidogo kuzitangaza hapa habari hizo hasa kwa kuzingatia nature ya tukio lenyewe.
Siku chache tangu Mch. Rwakatare atangaze kisa cha watoto hao kudondoshwa na nguvu ya maombi kanisani hapo, jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni na mganga (Daktari) mmoja wa kitengo cha magonjwa wa akili muhimbili walisema kuwa watoto hao hawakuwa misukule na ni matapeli wanaojulikana.Polisi walidai kuwa watoto hao wenye umri kati ya miaka 7 na 10 walishawahi kukamatwa kwa utapeli huo na kanisa moja la kipentekoste manzese na walipobainika kuwa walikuwa na njama za kujipatia kipato kwa udanganyifu walipelekwa kituo cha polisi.Kamanda wa polisi mkoa wa kipolis kinondoni ndg Jamal Rwambow, alisema kabla ya kujifanya wameanguka katika kanisa hilo la Mchungaji Rwakatare, hivi karibuni, watoto hao walifanya jambo kama hilo Januari 6, mwaka huu katika eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam.
Watoto hao walidaiwa kuanguka kanisani hapo mikocheni B assemblies of God wakati wakisafiri kwa ungo kutokea mwanza kuelekea mtwara.Na kwamba wao makazi yao ni makaburi ya kindondoni jijini Dar wanapofukua makaburi na kula nyama za watu.
Kisa hiki kimezua mjadala mpya kuhusu maombi ya kuombea misukule hapa nchini.
Sisi kama wanasayuni tunasema kuwa
1.Iwe kwa njia yoyote ile injili lazima itahubiriwa kila mahali ili iwe ushuhuda kwa watu wote na hapo huo mwisho ndipo utakapo kuja.Biblia inasema iwe kwa hila au kwa ukweli injili inahubiriwa.
2.Ni ushauri wetu kuwa ni vyema tuwe makini na roho zidanganyazo makanisani ili kuepuka kuutia aibu mwili wa Kristo.
3.Tunamuheshimu Mch. Rwakatare kama mtumishi wa Mungu na tunatambua mchango wake kwenye jamii yetu.Tunaomba wakristo wawe wanajifunza Biblia kwa umakini zaidi ili wasitumbukie kwenye mitego ya shetani.
4.Ni vyema wakristo tujue kuwa sisi sote ni mwili wa Kristo na shetani amefurahi sana kusikia habari hii na hata kusema kuwa "kiko wapi sasa...tulisema ninyi ni wasanii"...sasa naomba ndugu zangu wapendwa katika Bwana tuwe tunapima mambo maana wakati mwingine shetani anaweza kuleta jambo hili kwa mtindo huu kumbe akawa na lengo la kutuchafua wakrsito wa kweli.
5.Ni vyema tusisahau kuwa shetani ni baba wa uongo tena kweli haipo ndani yake.Kama watoto wale walienda kanisani na kudai kuwa wameanguka kwa nguvu ya maombi..kanisa likawaamini...then wakaenda hospitali na kukiri kuwa walidanganya habari ya kuanguka kwao na pia jamii ikawaamini....je tunaweza vipi kuthibitisha habari wanayoidai sasa kuwa walidanganya nayo ni ya ukweli...?
NB: Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya akili hospitali ya muhimbili akihojiwa na ITV alidai kuwa watoto hao wanaugua ugonjwa unaitwa saikosis ambao humfanya mtu kutunga habari na kuifanya kuwa ya kweli hata kama ni uongo...Sasa cha kujiuliza hapa ni kuwa bado tuendelee kuamini habari hii ya wagonjwa hawa wa saikosisi?
Mwandishi wetu wa mlima sayuni alituambia kuwa watoto hao waliletwa kanisani hapo wakiwa na mavumbi mwilini na michubuko sehemu sehemu inayodaiwa ilitokana na kuanguka kwao na kujeruhiwa na kuwafanya watu wengi waamini habari hiyo..

Mungu atusaidie katika kutafakari jambo hili.
 
[h=2]Mchungaji Rwakatare amtaja Shetani kujitetea [/h]
Mchungaji Rwakatare atoampya Baraza la Maadili

Mwananchi - Thursday, 16 June 2011
Nora Damian

MBUNGE wa Viti maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare jana alitoa mpya mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma alikofikishwa kujieleza kwa nini hakujaza fomu ya kutangaza mali zake, baada ya kudai kuwa shetani ndiye amepoteza fomu hizo.
Dk Rwakatare alisema hayo wakati akihojiwa na mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.

Katika utetezi wake, Dk Rwakatare alitumia maneno kama pepo, shetani na Mungu yalitawala.Mchungaji huyo alijitetea kuwa yeye alijaza fomu hizo na kuziwasilisha katika ofisi za bunge lakini hajui nini kilichotokea hadi fomu hizo zisifike kunakohusika.

"Mambo mengine ni shetani tu, shetani ana nguvu sana kila mahali yuko,"alisema Mchungaji huyo na kuongeza kuwa: "Kazi yenyewe ya kujaza fomu ni ya dakika 10 tu sio kwamba unafanya mtihani Cambridge hivyo halikuwa zoezi kubwa kwangu hadi mimi nishindwe kujaza,"alisema.

Alisema yeye hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba angeweza kuwa mmoja wa watu ambao hawakujaza fomu hizo kwasababu alizijaza na kuzirejesha Ofisi ya Bunge.

Dk Rwakatare pia alionyesha nakala ya fomu hiyo anayodai kuijaza na kudai kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika fomu hizo na kwamba kila mwaka amekuwa akizijaza.

"Tutaamini vipi kama nakala hiyo ni halali pengine ulikuwa nayo nyumbani na jana ukaitoa copy. Je hukusaini kokote wakati uliporudisha fomu hizo?" alihoji mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.

Akijibu swali hilo Dk Rwakatare alisema wakati wa kuchukua fomu hizo ilikuwa lazima kusaini lakini kurudisha haikuwa lazima.

Baadhi ya mahojiano baina ya Mchungaji huyo na Mwanasheria huyo wa baraza yalikuwa hivi:

Mwanasheria: Unasema ulijaza fomu, mbona hazikufika kwetu?

Rwakatare: Hilo litakuwa ni pepo tu. Mimi nilirejesha na Mungu ni shahidi.

Mwanasheria: Umeng'ang'ania shetani hivi huyo shetani ni nani?

Rwakatare: Ni roho chafu ambaye kazi yake ni kuharibu na kufanya mambo yaende vibaya.

Mwanasheria: Sasa huoni kama anakupeleka pabaya?Baada ya swali hilo, Mchungaji Rwakatare hakujibu kitu alikaa kimya.

Mwanasheria huyo aliliomba baraza hilo litupilie mbali utetezi wa Mchungaji huyo kwa sababu amekiri kutofanya ufuatiliaji.

Hata hivyo akizungumza nje ya baraza hilo na waandishi wa habari, Dk Rwakatare alisema tangu uanze mchakato wa fomu hizo, hajasafiri kwenda mahali kokote na kwamba anashangaa kwanini hawakumpigia simu kumuuliza kama alijaza au la.

"Mimi sijasafiri kwenda kokote na wala nilikuwa sina wasiwasi kabisa kwa sababu nilijaza fomu na kuzirejesha, wangeweza kunipigia simu na ningeweza kuja," alisema.

Alipoulizwa na waandishi wa habari haoni kama kuna haja ya kuwakemea mashetani, Mchungaji huyo hakujibu kitu aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mpanda Vijijini kupitia CCM, Moshi Kakoso naye alifikishwa kwenye baraza hilo jana na kuitupia lawama ofisi ya bunge kwa madai kuwa alijaza fomu na kuzikabidhi kwa wahudumu wa ofisi hiyo.

"Sijafurahia kuitwa katika baraza hili ni kitendo ambacho si kizuri. Naomba nipewe nafasi ya kujaza fomu nyingine ili nitekeleze sheria za nchi,"alisema Kakoso.Alisema yeye hana mali za kutisha kiasi cha kumfanya ashindwe kujaza fomu hizo na kulalamikia ofisi ya bunge kuwa haiko makini katika utunzaji wa kumbukumbu.

Mbunge huyo pia alipoulizwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Damian Lubuva kuhusu kumpa muhudumu wa ofisi ya bunge nyaraka muhimu kama hizo, alijitetea kuwa hilo ni bunge lake la kwanza na kwamba alidhani kuwa alikuwa sahihi kumpa muhudumu huyo.

"Hata mawasiliano ya barua kuja Mpanda yanachukua muda mrefu sana na kutufanya sisi wengine tuonekane tumekiuka sheria,"alisema Kakoso.

Baada ya kusikiliza utetezi wa wabunge hao, Jaji Lubuva alisema watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.

Baraza hilo litaendelea leo ambapo Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, diwani kutoka Geita Elias Okomu na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga Edwin


Kweli shetani mbaya sana. Kwanini anamfanyia hivi Mchungaji Rwakatare?
 
[h=2]Monday, February 11, 2008[/h] [h=3]Mchungaji Getrude Rwakatare akabidhi kanisa TAG?[/h]
















Habari zilizotufikia zinasema kuwa mch. Getrude Rwakatare amemwandikia barua askofu mkuu wa TAG , Mwenisongole kumjulisha nia yake ya kulikabidhi kanisa hilo kwa TAG kwa kipindi chote ambacho yeye atakuwa mbunge ila kwa sharti kwamba atampendekeza yeye mchungaji atakaye simamia kanisa kwa kipindi hicho chote.

Katiba ya TAG hairuhusu mchungaji yeyote kuwa mwanasiasa hali inayoonekana kuwa ngumu kwa Mch. Rwakatare.

Hata hivyo Jumapili iliyopita Mch. Rwakatare amekaririwa akikanusha vikali habari hizi kuwa amelikabidhi kanisa kwa TAG wakati akihubiri katika ibada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa mbunge iliyofanyika kanisani hapo mikocheni "B" Assemblies of God.

Baadhi wa washirika wa kanisa hilo wamesema kuwa kuna mgawanyiko umeanza kujitokeza miongoni mwa washirika na baraza la wazee hasa kwa wale wanaounga mkono uamuzi wake wa kujiingiza katika siasa na wale wanaompinga.

Sayuni blog itawaletea habari zaidi kadri tutakavyopata habari kutoka katika vyanzo vyetu.
 
Hivi aliyehuza kanisa la Kariakoo karibu na shule ya Uhuru na kuifanya kuwa maduka ya simu si huyu Dr. Rwakatare? nasikia mchungaji mwingine alizitafuna hela akamjengea mwanae wa kike nyumba kubwa na kununua magari kibao.
 
Upendo gani huu wa kutaka kujitajirisha mwenyewe, na kuacha kondoo wako wanahaha kwa njaa?
 
Back
Top Bottom