Mchungaji atupwa jela kwa kukataa kuapa mahakamani!

Hoja yako ni hafifu sana, kutii mamlaka siyo kufanya kila kinachoamriwa. Biblia inasema kila jambo lipimwe kama linaendana na maandiko ndiyo unalitii kama linapingana na maandiko unaachana nalo hata kama limeamriwa na askofu/rais/mahakama etc.

Hata hivyo kuapa mahakamani si lazima.

Taib mukulu..Taib.
 
Habari ndio hiyo ,huyu Mchungaji kakataa kuapa kuwa atasema kweli , kweli tupu na Mngu amsaidie.
Kimsingi ni kusema ataongea kweli tupu na akisema uongo kweli itamhukumu.
Sasa huyu Mchungaji uelewa wake ni mfupi sana.
Angejua tu , serikali nayo kupitia sheria inaheshimu sana dini, kiapo ni msingi wa kutengeneza ukweli katika kesi yenyewe, yeye anakataa sasa aeleweke vipi?

Kwa ushauri zaidi consult post #20..teh teh teh..
 
MCHUNGAJI Simon Kitwike wa madhehebu ya EAGT aliyehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kukataa kuapa mahakamani ameachiwa na kufungwa kifungo cha nje.

Akizungumza na Tanzania Daima nyumbani kwake, jana mara baada ya kutoka gerezani, mchungaji huyo alisema yeye alivamiwa na kundi la majambazi Oktoba 25 majira ya saa sita usiku na kuamliwa kutoa fedha, lakini ajabu anashangaa mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kukataa kuapa.

Kitwike alitaja mali zilizoibiwa siku hiyo kuwa ni pamoja na sh. milioni 1,212,000, godoro moja, seti moja ya runinga, redio mbili, rewinder moja, masanduku mawili yaliyokuwa na nguo za mchungaji huyo na simu za mkononi mbili vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 2.2.

Akizungumzia tukio la kufungwa mahakamani Februari 4 mwaka huu, Kitwike alisema hakukataa kuapa kwa kusudi bali aliiomba mahakama imruhusu kutoa ushahidi wake bila kuapa kwa kutumia kifungu katika kitabu cha maandiko matakatifu yaani Biblia kutoka Injili ya Mathayo 5:33-37.

Kifungu hicho kinasema "Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa usiape uongo ila mtimizie bwana japo zako lakini mimi nawaambia usiape kabisa hata kwa mbingu kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu"

Kabla ya Hakimu Nyasije Kajanja kutoa hukumu hiyo alimwamuru mchungaji huyo kusoma Waraka wa Warumi 13:1-2 unaosema, "Kila mtu na aitii mamlaka iliyokuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, na ile iliyopo imeamriwa na Mungu, hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao hujipatia hukumu".

Baada ya maelezo hayo, hakimu Kajanja alimsomea kifungu cha sheria na 198 (1) kama kilivyorekebishwa mwaka 2002 kinachokataza mtu kudharau amri ya mahakama na kuwa kuendelea kukataa kuapa ni kuvunja sheria na hivyo anatenda kosa la jinai.

Mchungaji aachiwa, afungwa kifungo cha nje
 
Hoja yako ni hafifu sana, kutii mamlaka siyo kufanya kila kinachoamriwa. Biblia inasema kila jambo lipimwe kama linaendana na maandiko ndiyo unalitii kama linapingana na maandiko unaachana nalo hata kama limeamriwa na askofu/rais/mahakama etc.

Hata hivyo kuapa mahakamani si lazima.

Mkuu ingependeza kama undetuelimisha ni kwa jinsi gani kuapa mahakamani sio lazima na kama kunasheria au hakuna sheria inayomlazimisha mtu kuapa.
 
Mchungaji ameachiwa na kufungwa kifungo cha nje. Yesu ni Mkuu na anaweza yote.
 
Mchungaji ana makosa. He quoted scripture out of context. This is a big problem with under-educated and self appointed religious leaders.

Hakimu anaadhibu wavunja sheria wote, kwa kufuatia sheria za Tanzania. Kama sheria inasema mtu aape, basi hakuna mtu kujikita kwenye uelewa mbaya wa Biblia na apone.

Umefanya sawa kabisa Mheshimiwa Hakimu. Ubarikiwe sana.

Abarikiwe na nani? Mchungaji yupo nje, hizo chuki zako hazina maana, na Biblia inaonekana huijuwi kabisaa.

Ni verse ipi ameisema out of context?
 
Last edited by a moderator:
Hivi kutokutii sheria ya mahakama kama hiyo ya kuapa ni kosa la jinai, ie. felony? Anyways, mchungaji anatumikia kifungo cha nje, sina uhakika hicho kifungo cha nje ndio kinakuwaje. Sasa akienda tena mahakamani hiyo Machi 2 atakubali kuapa au ndio huu mchezo utajirudiarudia? Kaazi kwelikweli...
 
Wakuu wenye ujuzi wa Sheria hebu tupeni mwangaza kidogo hapa juu ya mambo haya ya Ushahidi.
1. Hivi ni lazima kutoa ushahidi mahakamani ? na kama jambo nalijua na sitaki kutoa ushahidi kwa sababu zozote zile, sheria inasemaje?
2. Je ni lazima Shahidi aape kabla ya kutoa ushahidi wake?
3. Nini uzito wa kisheria wa ushahidi nje ya kiapo?
4. Je ni lazima Mahakama itoe hukumu kwa kuegemea kwenye ushahidi uliotolewa juu ya kiapo?
Mimi si mwanasheria lakini sidhani kama ni sahihi kumlazimisha mtu kutoa ushahidi. kwa fikra zangu ushahidi ni jambo la khiari, labda kwa kesi ambayo nawe ni mshtakiwa. na hiyo haitakuwa ushahidi bali ni utetezi ama kukiri kosa.

Naomba kupewa Mwangaza kidogo
 
Hoja yako ni hafifu sana, kutii mamlaka siyo kufanya kila kinachoamriwa. Biblia inasema kila jambo lipimwe kama linaendana na maandiko ndiyo unalitii kama linapingana na maandiko unaachana nalo hata kama limeamriwa na askofu/rais/mahakama etc.

Hata hivyo kuapa mahakamani si lazima.

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act)2002 inaweka sharti kuwa ushahidi mahakamani unatakiwa kutolewa kwa kiapo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 198(1)cha sheria hiyo kinachosema “Kila shahidi katika kesi ya jinai au shauri atalazimika, pasipo kupingana na sheria nyingine atatakiwa kuhojiwa kwa kiapo au uthibitisho kwa mujibu wa sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria.”

Na kwa mujibu wa Sheria ya Mwongozo wa Makosa ya Jinai (Penal Code)2002 Kifungu No. 114(1) juu ya Kudhihaki au Kudhara Mahakama inasema;-

a) Mtu yeyote akiwa kaika mazingira au mahali ambapo shauri linaendeshwa na mahakama na akaonesha kutoheshimu, iwe ni kwa matamshi au vitendo, kwa mujibu wa shauri hilo au mtu kwa yeyote anayehusika na shauri hilo.

b) Akiwa ameitwa kutoa ushahidi katika shauri mahakamani, akashindwakufika, au akiwa amefika akakataa kuapishwa au kufanya uthibitisho, au akiwa ameapishwa au amethibitishwa lakini akakataa,pasipo sababu inayotambulika kisheria, kujibu swali au kutoa karatasi au kitu chochote, au akikataa kuondoka mahakamani baada ya kuamriwa na mahakama kuondoka mahakamani hapo.

c) Akisababisha shauri kukwama au akisababisha usumbufu wakati shauri linaendelea kusikilizwa

“Mtu huyo atakuwa ametenda kosa la jinai na atakuwa na hatia na ataweza kuhukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi sita au kulipa faini isiyozidi shilingi mia tano”(hii shilingi mia tano kwa sasa imefanyiwa marekebisho, imeongezwa, but sijafanikiwa kuipata sheria iliyofanya marekebisho unaweza fuatilia hili)

Mkulu Nziku, Mchungaji hapo alichemka vilivyo hasa kwa kujifanya kichwa ngumu na kujifanya anaielewa Bible (he misinterpreted it), kiapo mahakamani ni lazima na sio hiari. Imewekwa bayana kama ni mkristo ataapa kwa Biblia, Muislam kwa quran na asiye na dini atapewa katiba mfano akina Kingunde na wenzie. Lakini kwa mtizamo wangu nadhani hili ni kosa la mfumo wote wa sheria Tanzania. Watu hawaelimishwi kuhusu sheria na haki zao. Kuna haja kubwa sana kwa kuwepo kwa mipango madhubuti ili wananchi waweze kuelewa walau sheria kuu za nchi na waweze kujua yapi ni majukumu na zipi nihaki zao (rights and responsibilities of citizens).
 
bm21 ahsante sana kwa ufafanuzi huo wa kisheria, lakini bado nina dukuduku lakufahamishwa kama ni lazima kwa mtu kutoa ushahidi. Sheria inalazimisha mtu kutoa ushahidi wa jambo alilolishuhudia?
 
Kwani lazima kuapa? Ni sheria gani inayolazimisha mtu kuapa? Je kama mimi ni mhindu, nitaapia kitabu kipi? Au kama ni rastafarian, nitaapia kitabu kipi? Au kama ni atheist, nitaapia kitabu kipi?

Mahakimu kama hawa ndio waliomhukumu kifo mbwa kwa kuitwa immigration. Uonevu mtupu.

Amandla....

Huyu mchungaji ni "conscientious objector". System yetu iko so primitive hatuna hata allowance for conscientious objectors.

Kama nguvu ya dola inataka kumhukumu mchungaji kwa makosa yake mengine, imhukumu.Lakini kumhukumu kwa kuwa mchungaji hatambui uwezo wa mahakama kumshurutisha kuapa ni tyranny.

Ni kweli imeandikwa "mpeni Kaisari ya Kaisari', lakini imeandikwa usilitaje bure jina la mungu wako, sasa kama kuapa kwa huyu mchungaji ni tantannomous na kumtaja mungu, na yeye hataki kumtaja mungu, mtamlazimishaje?

Unaweza ku judge a lot about a society by how it treats its children, the disabled, pregnant women and conscientious objectors.

What a shame!
 
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act)2002 inaweka sharti kuwa ushahidi mahakamani unatakiwa kutolewa kwa kiapo. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 198(1)cha sheria hiyo kinachosema “Kila shahidi katika kesi ya jinai au shauri atalazimika, pasipo kupingana na sheria nyingine atatakiwa kuhojiwa kwa kiapo au uthibitisho kwa mujibu wa sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria.”

Na kwa mujibu wa Sheria ya Mwongozo wa Makosa ya Jinai (Penal Code)2002 Kifungu No. 114(1) juu ya Kudhihaki au Kudhara Mahakama inasema;-

a) Mtu yeyote akiwa kaika mazingira au mahali ambapo shauri linaendeshwa na mahakama na akaonesha kutoheshimu, iwe ni kwa matamshi au vitendo, kwa mujibu wa shauri hilo au mtu kwa yeyote anayehusika na shauri hilo.

b) Akiwa ameitwa kutoa ushahidi katika shauri mahakamani, akashindwakufika, au akiwa amefika akakataa kuapishwa au kufanya uthibitisho, au akiwa ameapishwa au amethibitishwa lakini akakataa,pasipo sababu inayotambulika kisheria, kujibu swali au kutoa karatasi au kitu chochote, au akikataa kuondoka mahakamani baada ya kuamriwa na mahakama kuondoka mahakamani hapo.

c) Akisababisha shauri kukwama au akisababisha usumbufu wakati shauri linaendelea kusikilizwa

“Mtu huyo atakuwa ametenda kosa la jinai na atakuwa na hatia na ataweza kuhukumiwa kwenda jela kwa muda wa miezi sita au kulipa faini isiyozidi shilingi mia tano”(hii shilingi mia tano kwa sasa imefanyiwa marekebisho, imeongezwa, but sijafanikiwa kuipata sheria iliyofanya marekebisho unaweza fuatilia hili)

Mkulu Nziku, Mchungaji hapo alichemka vilivyo hasa kwa kujifanya kichwa ngumu na kujifanya anaielewa Bible (he misinterpreted it), kiapo mahakamani ni lazima na sio hiari. Imewekwa bayana kama ni mkristo ataapa kwa Biblia, Muislam kwa quran na asiye na dini atapewa katiba mfano akina Kingunde na wenzie. Lakini kwa mtizamo wangu nadhani hili ni kosa la mfumo wote wa sheria Tanzania. Watu hawaelimishwi kuhusu sheria na haki zao. Kuna haja kubwa sana kwa kuwepo kwa mipango madhubuti ili wananchi waweze kuelewa walau sheria kuu za nchi na waweze kujua yapi ni majukumu na zipi nihaki zao (rights and responsibilities of citizens).

Wewe unatuletea thesis zisizohusiana..

Kaa chini..
 
I don't see any criminal act done by the Pastor. To refuse to swear or give oath doesn't make someone criminal.

Uyo Mchungaji amekwenda mchomo kabisa na ,Jaji nae ni mbutwai ,nikianza na huyu jaji anataka kutuambia hizi mahakama hapa zinatoka kwa Mungu kwa kukariri mistari ya Warumi kutoka katika Biblia ?,haya ndio yale yale ya kutaka kuwaburuza watu gelezani,Jaji angelisema tu kuwa huu ni utaratibu wa tulio jiekea hapa Nchini.

Na huyo Mchungaji nae amijifanya mkakamavu wakati hakuelewa aya za Mathew na pengine hata ile ya James 5:12

Mchungaji alikurupuka tu maana haelewi kuwa kuna Common Oaths na Civil Oaths ,Mchungaji ameleta aya zinazopinga muumini kutumia common oaths ambazo hazina mpangilio wowote ule ,lakini zina ukweli si tumesikia mtu akisema ...kama kitu hiki si kweli basi nipo tayari kuuliwa ? Haki ya mama nitakuonyesha mimi ni nani na namna ya aina hizo ambazo zinakusudia kuwa kitu fulani kina ukweli ndani yake.

Lakini kwenye hili la pili ambalo linahusiana na mambo ya kimahakama ni vyema mchungaji angekamata kitabu anachokiamini na kwamba kutokana na imani yake na nguvu za kitabu chenyewe atakayosema au kutolea ushahidi ni kweli na hataweka uongo ndani yake kwa sababu amekamata kitabu chake kinachomfundisha kuwa mkweli,na hapa inakuwa kama anamuahidi Mungu na ikiwa atasema uongo basi adhabu ya Mungu wake imshukie ,ndio maana yake.

Tatizo walilonalo ndugu zetu hawa wa Kikristo wenye siasa kali wanaimani yao ile inayosema kuwa yeye hatasema uwongo hata siku moja au hatakuwa miongoni mwa wenye kusema uongo ,na siku zote ikiwa atasema ndio basi watu wafahamu kuwa alisema ni kweli au aliloulizwa na kulijibia ndio ndivyo lilivyo na hivyo hivyo akisema Hapana basi iamuliwe moja kwa moja kuwa kukataa kwake ni kweli. Hapo ndipo walipo wenzetu hawa ,lakini sioni sababu ya ukataaji kushika kitabu unachokiamini kiwe na nguvu juu yako kwa yale utakayoyajibu.

Ila kwa binadamu anaweza akakamata bibilia au msahafu na akasema uongo ikawa sawasawa na kutokukamata Lakini mbele ya Mungu haiwi sawa ,yaani kiakili tu ni vitu viwili tofauti kabisa na kama ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa kusema uongo basi yule aliekamata kitabu atapata adhabu kubwa zaidi kuliko yule ambae alitaka aonekane yeye ni msema kweli tu.

Na tatizo mahakama zetu hazijaweka utaratibu wa kumsikiliza mtu ambae atakataa kukamata kitabu cha dini yake hata ikiwa yule mtu atasema kuwa atakayoyasema yote yata kuwa ya kweli kwa kadiri anavyofahamu na hataweka uwongo ndani yake.

Sasa kwa wale watu wenye msimamo mkali angallieni hili pia Not being anti-religious or anything, but what if the bible was just fake? I mean one would swear to tell the truth, upon a book of lies ? Mchungaji ameingia mitini.

Lakini vilevile muitazame mahakama nayo ,naamini kabisa mahakama zinafahamu kuwa kufanya jambo hili la kula kiapo si lazima ,the idea is that, once the witness has taken this oath, they must tell the truth or be struck down by the righteous wrath of The Lord ,hivyo mahakama zinaamini kuwa zitamkwamisha mtu kwa kukamata kitabu chake ,sasa sijui mahakama zinawaamini vipi watu wanaokula kiapo kwamba wanayoyasema yote eti yatakuwa ni ya kweli ,ila wakikukamata umesema uongo watakusweka jela sasa wale mawaziri wa serikali ya Mheshimiwa Kikwete walio ondolewa walikula kiapo cha kuitumikia Nchi hii lakini leo hii wameonekana kwenda kinyume ,hivyo wanahitajiwa na mahakama au mahakama iwashitaki kwa kwenda kinyume na kiapo chao na wao wengine walikamata bibilia na na wengine misahafu. Nafikiri mahakama inaweza kumshitaki mtu ?
 
Last edited:
Wewe unatuletea thesis zisizohusiana..

Kaa chini..

Nimegundua lengo lako ni kupost bila kujali unapost nini. Sibishani na wewe. Mchambuzi atasema tatizo ni nini this is Uduld learning on the other hand, give critical argument not just critics.
 
Nimegundua lengo lako ni kupost bila kujali unapost nini. Sibishani na wewe. Mchambuzi atasema tatizo ni nini this is Uduld learning on the other hand, give critical argument not just critics.

Kajifunze kuongea kwanza..
 
Leo nimekula kiporo cha wali maharage asubuhi. Nimeshiba sana. Ngoja niende kibaruani
 
Back
Top Bottom