Mchungaji asimamishwa kwa uzinzi

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
UONGOZI wa Kanisa la Evangelistic Assembles Of God Tanzania Jimbo la Dodoma, limemsimamisha na kumfutia leseni ya huduma ya kiroho nchini mchungaji wake kutokana na kupatikana na hatia ya uzinzi.

Uamuzi huo umetokana na mchungaji huyo kukutwa akifanya tendo la ndoa katika nyumba ya wageni iliyopo mjini hapa.

Akitangaza kumfukuza na kumzuilia huduma mchungaji huyo, Askofu wa Jimbo la Dodoma, Jackson Madelemo, alisema kanisa kupitia uongozi wa ngazi ya jimbo umeamua kumsimamisha na kumfukuza kutokana na tabia hiyo ambayo haiendani na huduma ya kiroho.

Askofu Madelemo alisema kitendo cha mchungaji huyo kimeliaibisha kanisa na kwamba hawezi kuendelea na kazi ya kumtumikia Mungu.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa mchungaji wa kanisa hilo mbele ya waumini waliohudhuria ibada, Askofu Madelemo alisema mchungaji huyo amekuwa akituhumiwa kwa makosa mengi ya uzinzi, lakini kwa kuwa uongozi wa jimbo haukuwa na ushahidi ulijaribu kufumbia macho huku akiitwa katika vikao vya mara kwa mara.

“Sisi kama viongozi wa kiroho tulijitahidi kuhakikisha tunamweka chini mchungaji wetu ili aweze kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na kumsihi kuachana na tamaa za mwili, lakini dhambi hiyo imeendelea kumtafuna mpaka leo hii tunapochukua hatua ya kumfutia huduma yake,” alisema.

Source: Tanzania Daima
 
Wakuu samahani kama itakuwa si mahala pake mtanisamehe lakini mm nilipendelea iwepo hapa. Kumbe wachungaji hawaruhusiwi kumegea kwenye nyumba za wageni angekuwa anachunga kondoo na kulia mle mle zizini asingetimliwa.
 
Kwani alikuwa anamegana na nani? isije ikawa alikuwa mkewe? cmhungaji wa kilokole alikuwa bado hajaoa?
 
Huyo anaenda kuanzisha kanisa lake muda si mrefu.
Usishangae likaitwa Kanisa la miujiza ya Bwana.
 
wanamuonea!UZINZI NI PART YA MAZOEZI
Jasiri haachi asili. Mila is there to stay bwana harusi!

Kwani alikuwa anamegana na nani? isije ikawa alikuwa mkewe? cmhungaji wa kilokole alikuwa bado hajaoa?
Hommie bana! Angemegana na mkewe angesimamishwa?

kwani ukioa ndo humegi nje?
:eek::D!!

Bwana Arusi.................... kuna aloiba password yako!
Kwani vipi mjukuu?

ni mimi bwana harusi HIMSELF
Afadhali umemjibu mwenyewe, nadhani hatauliza tena.
 
wanamuonea!UZINZI NI PART YA MAZOEZI

mmmh! Mpwaaz mazoezi yepi unayazungumzia hapa?

@Fidel chanzo chako si sahihi sana; Askofu Madelemo ni mtumishi wa Pentecostal Holyness na si EAGT; pili Jina la Mchunaji halipo; unajua anaitwa nani ili tuweze kukamilisha hii news yako!
 
kwani ukioa ndo humegi nje?

supposedly not!

Nilikuwa nafikiria kuwa kama aliamua kudumisha mila na mkewe mazingira tofauti!

ina maana mtu anakuwa mchungaji na huku hajaoa? wanamdhania malaika au inakuwaje?
 
supposedly not!

Nilikuwa nafikiria kuwa kama aliamua kudumisha mila na mkewe mazingira tofauti!

ina maana mtu anakuwa mchungaji na huku hajaoa? wanamdhania malaika au inakuwaje?
Hommie usisahau mapadre hawaoi!!
 
Hommie bana! Angemegana na mkewe angesimamishwa?

Asingesimamishwa ilanapata picha hapa kuwa alikuwa anadumisha mila hovyo hovyo,

ananikumbusha mayasa wa mwanakijiji na limjamaa la prado kumbe mchungaji magomeni....
 
Hommie usisahau mapadre hawaoi!!

hommie kwani walokole wana mapadri? wao wanawaita wachungaji..hilo la mapadri nalijua, sasa nilifikiria kwa vile wamekuwa wakilalamika sheria ngumu za mapadre wakatoliki kuwa hawaruhusiwi kuoa kwa mfano, basi wao wangeweka sharti kuwa kabla hujawa mchungaji, uwe umeoa kwanza...

hivi tunaweza kuwa na Rais asiye na mke eeh hommie?
 
Askofu Madelemo alisema kitendo cha mchungaji huyo kimeliaibisha kanisa na kwamba hawezi kuendelea na kazi ya kumtumikia Mungu
Makanisa ya Afrika yanawatu wakali sana, wakati wenzao Ulaya wana hata Maaskofu Mashoga na wanawasmamehe, sembuse huyu anayewafanyizia mademu...kaazi kwelikweli.
 
hommie kwani walokole wana mapadri? wao wanawaita wachungaji..hilo la mapadri nalijua, sasa nilifikiria kwa vile wamekuwa wakilalamika sheria ngumu za mapadre wakatoliki kuwa hawaruhusiwi kuoa kwa mfano, basi wao wangeweka sharti kuwa kabla hujawa mchungaji, uwe umeoa kwanza...

hivi tunaweza kuwa na Rais asiye na mke eeh hommie?
Napata kigugumizi hapa. Kwa wakatoliki ni sharti padre asioe.
Hivi kwa protestanti (walokole to be precise) ni sharti kwa mchungaji kuoa? Haruhusiwi kuishi kiseja?
Hapo kwenye bold, labda Rais mwenyewe asiwe JK. Hahahaha!
Sijui katiba inasemaje. Unajua mi mvivu sana wa kusoma ile kitu. Najua kuna limitations za umri lakini kwenye marital status sina uhakika. Where is our bht?
 
sijui yuko wapi when we need her the most?

manake logically anaishije kiseja na anatakiwa kuhubiria watu wengine wenye ndoa zao..aah sielewi bana sijui wenyewe wako wapi watusaidie
 
sijui yuko wapi when we need her the most?

manake logically anaishije kiseja na anatakiwa kuhubiria watu wengine wenye ndoa zao..aah sielewi bana sijui wenyewe wako wapi watusaidie
Ngoja nimuulize Geoff - hapana, yule ni mlei. Fidel?... Katekista. Nguli?.... Mkatekumeni. JS?.... Sista yule. Dah! Nani sasa? Mj1? Anaweza kuwa WAWATA yule. Ahaa. Charity............! Wapi Charity atufafanulie hii kitu? Ngoja niingie hewani fasta.
 
Back
Top Bottom