Mchungaji anaswa akimuogesha mke wa mtu

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
AMA KWELI dunia imekwisha, makanisa, watumishi wa Bwana wanazidi kumtia hasira Mungu kila kukicha, Afrika ndiyo inaongoza. Mtumishi mmoja wa Mungu nchini Ghana amenaswa hivi karibuni akimwogesha mke wa mtu ambaye ni muumini wake kwa madai anamtakasa.

Picha ya mtumishi huyo ilipigwa kwa siri na kamera ndogo iliyotegwa eneo la tukio.

Habari zinasema mtumishi huyo (jina lake halikupatikana mara moja) alimwogesha mwanamke huyo wakati wa mfululizo wa maombi ya utakaso maarufu kwa jina la Deliverensi.

Baada ya kumaliza kumwogesha, alimfuta maji kwa taulo na baadaye kumpaka mafuta aliyodai yana upako wa ki-Mungu ‘Anointed'.

Ni vyema jamii ikaangalia upya sera za makanisa, hasa ya kiroho, wanayojiunga nayo kwani mengi hayafuati maagizo ya Mungu bali shetani.
 
Tatizo liko wapi kama mchungaji anampa utakaso muumini wake mwili mzima?
 
jamii itaangaliaje upya hili wakati lipo ki-imani zaidi na muumini amekubaliana na hali halisi! Labda kuwekwe mipaka ya imani ikiwa inawezekana.
 
ndo maana imeandikwa tuzichunguze hizo roho... Si kila anayeibuka na kuhubiri umkimbilie......matokeo yake ndo hayo....
 
hakutupia??? kama hakutupia inaweekana kweli ni upako

Wala usitetee upumbavu mkuu. Hakuna dini wala dhehebu linalomwabudu na kumheshimu Mungu lenye taratibu za kishetani kama hizi. Wala hakuna maandiko yoyote yanayoruhusu upuuzi kama huu.
 
jamii itaangaliaje upya hili wakati lipo ki-imani zaidi na muumini amekubaliana na hali halisi! Labda kuwekwe mipaka ya imani ikiwa inawezekana.

Imani gani ya kukaa uchi kama sio dini ya kumwabudu shetani hiyo? Kama ndio hivyo basi uwe unaingia kanisani au msikitini ukiwa uchi.
 
Hayo ndiyo mambo mutakayayakuta kwa akina Anthon Lusekelo, Gwajima , Kakobe na akina Mwingira. Na utagundua kuwa victims wengi akina mama katika mtego huu. Nayo inatokana na imani haba kutoka kwenye madhehebu yao ya awali kwa hiyo wasimlaumu mtu kwa udhalilishaji huu.
 
Hivi ile scandal ya Josephat Mwingira mwana wa kunyumba ya kuendekeza libeneke na mke wa mwanasheria na muumini wake mtiifu hadi alitoa kiwanja kama sadaka na Mwingira akajenga jengo lake binafsi, imeishia wapi?

Mwenye updates atujuvye.

AMA KWELI dunia imekwisha, makanisa, watumishi wa Bwana wanazidi kumtia hasira Mungu kila kukicha, Afrika ndiyo inaongoza. Mtumishi mmoja wa Mungu nchini Ghana amenaswa hivi karibuni akimwogesha mke wa mtu ambaye ni muumini wake kwa madai anamtakasa.

Picha ya mtumishi huyo ilipigwa kwa siri na kamera ndogo iliyotegwa eneo la tukio.

Habari zinasema mtumishi huyo (jina lake halikupatikana mara moja) alimwogesha mwanamke huyo wakati wa mfululizo wa maombi ya utakaso maarufu kwa jina la Deliverensi.

Baada ya kumaliza kumwogesha, alimfuta maji kwa taulo na baadaye kumpaka mafuta aliyodai yana upako wa ki-Mungu ‘Anointed’.

Ni vyema jamii ikaangalia upya sera za makanisa, hasa ya kiroho, wanayojiunga nayo kwani mengi hayafuati maagizo ya Mungu bali shetani.
 
Weni yanawashinda mpaka wanaachia ngazi kwa kushinikizwa na hata wakiwa nje ya kanisa hawaachi vituko, tumesikia ex padre maarufu sana Tanzania akitembea na mke wa mtu.
 
Hayo ndiyo mambo mutakayayakuta kwa akina Anthon Lusekelo, Gwajima , Kakobe na akina Mwingira. Na utagundua kuwa victims wengi akina mama katika mtego huu. Nayo inatokana na imani haba kutoka kwenye madhehebu yao ya awali kwa hiyo wasimlaumu mtu kwa udhalilishaji huu.

Usiniambie mkuu. Kumbe haya mambo yapo kwa akina Anthon Lusekelo, Gwajima , Kakobe na akina Mwingira?
 
Hivi ile scandal ya Josephat Mwingira mwana wa kunyumba ya kuendekeza libeneke na mke wa mwanasheria na muumini wake mtiifu hadi alitoa kiwanja kama sadaka na Mwingira akajenga jengo lake binafsi, imeishia wapi?

Mwenye updates atujuvye.

Hiyo kesi mbona sijwahi kuisikia mkuu? Embu nipe details, ilikuwaje?
 
Back
Top Bottom