Mchumba wangu anatoka na baba yake mzazi, nifanyeje?

Dah mdogo wangu watafuta stress na kujitundika Au? Kama yote unayosema yametokea na ulienda dirishani kweli Wewe wataka Mungu akusaidie nini tena Jamani? Achana Naye wanawake wapo tu utapata! Kifo cha maumivu Kiko mbele mdogo wangu, aching na huyo mdudu Jamani.


Tuna miaka miwili tangu tuanze uhusiano,
Mwanzoni tulikuwa wapenzi wa kawaida ila baadaye tulikubaliana kuoana,
hivi karibuni nimemtambulisha kwetu kisha nikaanza maandalizi ya kwenda kwao
Ndipo nilipoanza kusikia maneno mengi kutoka kwa watu wa karibu na familia yao
mara eti huyu binti amewahi kutoa mimba ya babake mdogo,mara anatembea na baba yake!
awali niliyapuuza nikijua ni uzushi ila baadaye niliamua kumbana ili anipe ukweli,
ilichukua mda mrefu ila baadae alikiri kuwa na uhusiano na babake mdogo kijana aliyekuwa akiishi hapo kwao ila kwa sasa alishaondoka,pia alikiri kutoa mimba ya huyo baba mdogo ila anadai ni zamani kabla hatujafahamiana,alikana kutoka na baba mzazi,
Kwa kuwa nampenda naye anaonesha kunipenda nilisamehe ila siku moja wazazi wake walienda kwenye sherehe na kurudi saa 5 usiku mama akiwa amelewa ila baba yake hatumii kilevi,
Tulikuwa tunachart kwa sms na yeye ndiye aliyenifahamisha kila kitu,
Ilipotimu saa 6 usiku alidai anataka kulala hivyo tustop kuchat(ingawa kwa kawaida huwa anapenda tuchart mpaka saa 8)
tuliagana ila baada ya nusu saa niliamua kumpigia cm ili nimkumbushe kitu,
cha ajabu alipokea cm na kuongea kwa ukali huku akinieleza kuwa atanipigia baadae usiku huo!
nilianza kuhisi jambo baya hivyo nilikodi tax na kuelekea mtaa anapoishi,
nilipofika kwao nilienda mpaka kwenye dirisha la chumba chake ili nimgongee,
lakini kabla sijafanya chochote nilisikia sauti za watu wakifanya mapenzi!
nilijaribu kupiga cm yake akawa hapokei
nikaamua kurekodi sauti kupitia dirishani kwake!
mchezo huo ulidumu takriban DK45
ndipo nikapiga tena akapokea ila akawa haongei !
kwa jinsi nilivyompenda nilijipa moyo na kuondoka mpaka pembeni na nyumba yao nikakaa mpaka alfajiri ili nione nani atatoka ndani kwani niliamini aliingiza mtu bila wazazi kujua hivyo lazima atatoka mapema,
Lakn cha ajabu ilipotimu saa 11 alfajiri nikampigia tena cm akapokea nilipomweleza kwamba amenisaliti na kwamba nimeshuhudia nikiwa dirishani alianza kulia na kushindwa kuongea,!
mpaka kunakucha hakuna mwanaume aliyeonekana akitoka nje ndipo nilipoanza kuamini inawezekana alikuwa na baba yake mzazi kwani kipindi hiki hakuna kijana anayeishi hapo,
Kesho yake alikuja kwangu nikampa cm asikirize nilivyorekodi dirishani alisikiliza mwanzo mpaka mwisho akaanza kulia
akasema hakuwa na mwanamme ila alilala peke yake!
Kingine kinachofanya naamini anatoka na mshua wake:-
>yeye ni mtoto wa pili ktk familia ila anapendwa na baba kuliko watoto wote hata kadi za benki anatunza yeye!
>Haelewani na mama yake mzazi kila kitu ananunuliwa na babake!
>nyumbani wako waschana 3 ila wengine wanalala chumba cha pamoja yeye analala peke yake na chumba chake hakina mlango,
>Babake ni shabiki wa mpira mara nyingi akienda bar kuangalia mpira akirudi usiku wa manane humgongea dirisha huyu binti ndo amfungulie geti!
>Japo alikiri kutoa mimba ya babake mdogo inasemekana aliwahi pia kutoa mimba nyigine ya babake mzazi kwani majirani wanadai mimba ya kwanza alitoa akiwa form2 ya pili akiwa form 3 na hii ya mwisho ilijulikana mpaka shuleni na ilifika miezi mitano ila cha ajabu familia ilikuwa kimya!
>Maelewano ya kifamilia baina ya baba na mama yamepungua mpaka mama yake anataka kuondoka!
>watoto wote wanamtetea mama ila binti anamtetea baba na kusema mamake ana tabia mbaya!
Wadau mnaonizidi umri naombeni ushauri wenu,nampenda sana na nimeshajipanga kumwoa hata yeye ananipenda sana kwani alinivumilia nikiwa katika kipindi kigumu kimaisha, Ila katika hili niko njia panda...!
 
kweli umempenda huyo binti, na uchafu wote huo wa huyo binti bado unakuja kuomba ushauri!!
i thought umeshamwaga manyanga siku mingi mkuu,huyo mwanamke atakuwa na laana si bure!!
kimbia fasta
 
Mshukuru sana Mungu kwa kukuonyesha ukweli!hapo sipo achana hiyo na shukuru kwa yote!utapata kwingine huyo ni shetani ana ana laana!
 
Hebu tufanye mfano mtu anamshauri mtu aje atoke na mama yako utajisikiaje? hebu tuwapeni heshima stahiki mama zetu. wanahitaji zaidi heshima kuliko dharau ya kiwango hiki.

MI NACHOWAPENDEA WANAFUNZI WANGU KWENYE KUFAA UKALI WANAKUWA WAKALI KWELIKWELI!proud being ur mwalimu Asprin.tukutane darasani.
 
Last edited by a moderator:
Unless ni story ya kutunga kama alivyosema Dena Amsi ..lakini kama ni kweli sioni hata haja ya wewe kusubiri tukushauri. Hebu shirikisha ubongo wako kidogo utaona majibu yanapatikana. Baba mzazi na bintiye..lol!
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka na wewe ulishawahi kufanya mchezo huu na babaako sio bure. Ni busara gani ulioiona kwenye upuuzi alioandika Swts?

Hivi ktk hali ya kawaida huyo mwanamke akienda kwao hata msibani wewe huku nyuma unabaki na amani kweli? Bila shaka nyinyi wa njia moja, si bure wallah! Kwa hiyo unampenda Swts kwa kuwa unajua ukishabanjuliwa huko anakuhamishia mji mwingine, huko nako ukibanjuliwa anakuhamishia mji mwingine hivyo hivyo mpk mnatokea kuzimu kwa UKIMWI
usirudie kukurupuka kama hujaelewa ********
 
sasa mkuu hebu achana tu na huyo msichana ,kuna mambo tunayavumilia kwenye mahusiano lakini hiuli ni beyond borders i see!waache wapinduane marinda.kuna mabinti wengi tu wazuri wanafaa kuolewa!wala haina haja kubaki na hyo mwanamke,kwa kipi kwanza?
 
Unless ni story ya kutunga kama alivyosema Dena Amsi ..lakini kama ni kweli sioni hata haja ya wewe kusubiri tukushauri. Hebu shirikisha ubongo wako kidogo utaona majibu yanapatikana. Baba mzazi na bintiye..lol!
salaam my pacha!
hili kweli halina majdala though si unajua kuna mambo mengina huwa tunajiaminisha tunaweza kuyabadilisha tukishaoana?nafikiri ndo mleta mada anachojifariji!ukweli ni kwamba hili halina mabadiliko ya kiumbo wala kikemikali huyu mzee ataendelea kula mzigo hapo mpaka ukamilifu wa dahari!dah dunia inaenda wapi jamani!
 
Halafu ni ya uwongo kabisa!. Mwishoni anasema kuwa binti ndiye anayefungua Geti siku dingi akirudi kutoka kutazama mpira. Yeye usiku huo alipoenda kumrekodi Binti ni nani alimfungulia Geti? Kumbuka kuwa mama kalewa, hajiwezi na Dingi wakati huo anadoo na binti. Nani alimfungulia Geti?

Ha ha ha ha ha umeona eeehhhh?? Hakuna kitu hapa bana.............................
 
tunajua kupenda ni upofu lakini si ulemavu so jamaa kuwa makini na hakuna jambo ambalo litakufanya ujute kama utakapo kosea kuchagua mke wa kuoa dem kashatoa mimba karibu ya tano kingine anatembea na babazake tayali laana hiyo unaweza ukazani wanao kumbe shemeji zako lakini ni sawa kuwa wanawake wapo wengi lakini si wote waolewaji chukua muda tafuta asiye na laana oa sana mshilikishe MUUMBA kwa imani yako kuwa na siku njema.
 
Unless ni story ya kutunga kama alivyosema Dena Amsi ..lakini kama ni kweli sioni hata haja ya wewe kusubiri tukushauri. Hebu shirikisha ubongo wako kidogo utaona majibu yanapatikana. Baba mzazi na bintiye..lol!

SnowBall hebu msome gmosha48 hapa chini anavyosema..............

Halafu ni ya uwongo kabisa!. Mwishoni anasema kuwa binti ndiye anayefungua Geti siku dingi akirudi kutoka kutazama mpira. Yeye usiku huo alipoenda kumrekodi Binti ni nani alimfungulia Geti? Kumbuka kuwa mama kalewa, hajiwezi na Dingi wakati huo anadoo na binti. Nani alimfungulia Geti?

Kwaherini na asanteni
 
hapo hata sigeuki ni mbio mwanzo mwisho mtu na mzazi wake kha!
 
Hilo loki wazi wala huhitaji ushauri kwa kuwa umethibitisha mwenyewe achana naye, kama unaona ni vigumu kumwacha nenda ukaombewe inawezekana hizo roho chafu alizo nazo zimeisha kuvaa na wewe. Yaani huyo achana naye mara moja
 
halafu ni ya uwongo kabisa!. Mwishoni anasema kuwa binti ndiye anayefungua geti siku dingi akirudi kutoka kutazama mpira. Yeye usiku huo alipoenda kumrekodi binti ni nani alimfungulia geti? Kumbuka kuwa mama kalewa, hajiwezi na dingi wakati huo anadoo na binti. Nani alimfungulia geti?

gmosha48 na dena amsi you are great thinkers..i salute you. Mie nimeisoma kisha nikaanza kuona hii ni hadithi ya kutunga na isiyoleta sense hata chembe....

ila mtunzi kachukuwa hisia za wadau kirahisi sana bila hata kushitukiwa... nahisi jf imeingiwa na ombwe la great thinkers..ina fastest writers or wengi wetu hatujiongezi kufikiria kwa kina.

ni maoni tuu.
 
salaam my pacha!
hili kweli halina majdala though si unajua kuna mambo mengina huwa tunajiaminisha tunaweza kuyabadilisha tukishaoana?nafikiri ndo mleta mada anachojifariji!ukweli ni kwamba hili halina mabadiliko ya kiumbo wala kikemikali huyu mzee ataendelea kula mzigo hapo mpaka ukamilifu wa dahari!dah dunia inaenda wapi jamani!

sijambo pacha..ni kweli huyu mleta mada anatakiwa atambue 'mlamba asali halambi mara moja tu'...
 
Huyo mwogope kama ukoma.Nakushangaa hata sasa unaposema unampenda hata baada ya kutambua ukweli wote huo,kama unampenda wa hivyo kwa ajili awe mke wako basi anything in sketi unaweza ukaoa!Pole lakini nafikiri wote hamjazidiana upeo katika maadili,baba mdogo,mimba ya kwanza,mimba ya pili,baba mzazi na kurekodi juu hahaha basi naona wewe pia unakasoro!
 
Duh kama story ni yakweli huyo dada anaishi uswaz sana kama unaweza kwenda kukaa dirishani na kurecod kila kitu then ukalala nje kwao ujue nani atakae toka chumbani hyo hatari.ila una moyo wa jiwe au nawew ulikuwa unapandsha steam pale dirishani kwa kuskilizia game la demu wako.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom