Mchumba ninayekaribia kumuoa simuelewi

Ni kweli. Je kuna namna unahisi labda nitumie kumfanya aweze kujihusisha na mambo ya usafi/kupika?

..........Ipo!, ni kumpiga chini tu ndo anaweza kujihusisha na mambo ya usafi/kupika akiwa kwao. vinginevyo muoe tu kwasababu nafsi yako imelalia upande huo wa kumuoa na hakikisha dawa za kutibu presha na maumivu ya kichwa hazikauki nyumbani kwako mkiishi nae pamoja kama mke na mume..
 
mtoa mada hivi kwani at first ulimpendea nini? je ulichofikiri kwamba ni sababu ya kumpenda bado kipo ama hakipo? Pia hili swala la mtu kisirani nazid kuliona tena hapa jamvii hivi huyu ni mtu wa namna gani hadi aitwe kisirani?

Sababu ya kumpenda bado ipo na haishikiki/haielezeki(intangible)
 
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.

Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa

Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.

1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.

2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.

Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?

Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.

Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!

Ushauri

Mkuu, Oa hii headache halafu uweke kabisa order ya maboksi mawili ya Hedex kila mwezi pale Shelys Pharmaceuticals...

Unanikumbusha mpenzi wangu wa kwanza niliyeanza naye toka primary school, nikakaa naye 13 years kwa style hiyo hiyo ya kuwa mbali mbali mara zote,mpaka baada ya ku-graduate...tumelazimika kuachana baada ya finaly kugundua hatuendani,na wote tulilia siku hiyo maana it had been such a long journey..

...tabia za ukubwani ndio zinazomatter sababu maisha ya ndoa sio ubishoo na usista duuu tu,,,its about hustling together and supporting one another..she cant,,,dump her really quick!!
 
kaka huyo mwanamke ni kizaz cha Ipad, hawajaumbwa kwa ajil ya kuolewa. hao wanafaa kuwa magirlfriend tu then unaachana nae na kutafuta kizaz cha wanawake wa desktop, hao hawana usumbufu hata urud sa 8 usiku utamkuta anakungoja huku anajisomea ufunuo wa Yohana taratibu, tofaut na hao kizaz cha Ipad ukichelewa nae anatoka usiku kuzurura
 
kaka huyo mwanamke ni kizaz cha Ipad, hawajaumbwa kwa ajil ya kuolewa. hao wanafaa kuwa magirlfriend tu then unaachana nae na kutafuta kizaz cha wanawake wa desktop, hao hawana usumbufu hata urud sa 8 usiku utamkuta anakungoja huku anajisomea ufunuo wa Yohana taratibu, tofaut na hao kizaz cha Ipad ukichelewa nae anatoka usiku kuzurura

Hahaha, Ufunuo wa YOHANA taratibu wakati mtu mzima unapiga MASANGA
 
ukiona manyoya kashaliwa bro jipange coz dada zetu wanajengaga foundation mapema ukioa hata glas utatoa mwenyewe man na bado kirambasi ya mimba utadata
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom