Mchumba asiye mwaminifu hupata mwenye ndoa asiyemwaminifu!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,139
Mchumba asiye mwaminifu huwa mwenye ndoa asiyemwaminifu!

Swali:
Habari za kazi kaka naomba nisaidie naangamia kwa kuwa na mawazo yasiyo na msingi na kuumiza afya yangu, kweli nateseka mno.
Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 29, nilikuwa na relation ya kwanza ambayo ilidumu kwa miaka mitatu lakini kikubwa kilichotufanya tusaparete ni dini yeye muislam mie mkristu.
But baada ya muda kupita nikapata mvulana mwingine kwa kweli nilifurahi toka siku ya kwanza kwa kuwa wote ni wakristu na nilimuona kwamba anampenda Mungu kwa matendo yake lakini kadri tulivyoendelea na relation nikagundua ana affair na wasichana wengine.

Niligundua kupitia simu yake ya mkononi, nikamwambia na nikampa masharti kama ananipenda anipeleke kwao kunitambulisha na akafanya hivyo, haijapita mwezi bado anaendelea na hao wasichana wengine tena akiwa anakuja kwangu anawambia wasitume msg wala kupiga simu, lakini pia nimegundua ana relation mpya kaanzisha tena kwa mwanamke mwingine yani kichwa kinaniumwa!

Maswali
Je, Ni kweli mwanaume wa hivi anarekebishika kweli?
Je, kwa nini anakuwa na wasichana tofauti tofauti?
Na nikajaribu kupeleleza kwao nikaambiwa ni mimi peke yangu nilipelekwa kutambulishwa.
Je, kweli anafaa kuwa mume?
Maana sihitaji kuwa nabadilisha wanaume kila siku nahitaji kupata ushauri wa kuwa kama anabadilishika bora nitulie nae kuliko kufuata mwingine na kila siku kuwa na wanaume tofautitofauti.
Kweli nampenda kwasababu familia yao ipo katika misingi ya dini imara.

Nimeelemewa na mawazo.

Ni mimi dada Yamenikuta.

MAJIBU YA SWALI LAKO

Pole sana dada Yamenikuta!

Kama mmoja ya watu ambao hupokea maswali mengi yanayohusiana na ndoa na uchumba au mahusiano kwa ujumla, ukweli kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusiana na suala la wanandoa kuoa wrong partner, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wa hawa ambao wameoana na wanaume/wanawake wasiofaa wanakiri kwamba walikuwa wanajua na kufahamu fika kwamba wachumba zao walikuwa na tatizo hata kabla ya kuoana, kwa kuwa walikuwa wamependa (fall in love) au pendana kwa muda mrefu au muda wa kuoa ulikuwa umefika waliamua kwa hiari zao kuendelea na mahusiano wakitegemea kwamba siku moja watabadilika.

Je, tunaweza kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?
Hivyo basi dada Yamenikuta, ni jambo la busara na hekima kubwa kuwa makini na maamuzi unayofanya hasa baada ya kukutana na mwanaume ambaye ameshindwa kutembea katika ahadi kamili za msingi wa mahusiano yenu na kutegemea kuwa na ndoa yenye baraka.

Usikubali kuoana naye kwa sababu eti unampenda sana na umekuwa naye kwa muda mrefu katika mahusiano kabla ya kuoana.
Urefu wa mnahusiano kabla ya kuoana (uchumba) au wewe kumpenda na kujioana huwezi kuishi bila yeye hauna uhusiano wowote na afya ya ndoa yako baadae kama huyo mchumba wako ameshindwa kuwa mwaminifu kabla ya kuoana.
Tabia alizonazo kabla ya kuoana haziwezi kubadilika ghafla baada ya kuoana.
Mwanaume asiyemwaminifu kabla ya kuoana hatakuwa mwaminifu baada ya kuoana pia.
Ndoa huwa haibadilishi mtu kiburi chake, hasira zake, umalaya wake, wizi wake, tabia zake chafu sana sana ndoa hufunua hizi tabia na kuziweka mezani uzione.

Usijidanganye mwenyewe na kujipa moyo, utaangukia pua!

Kile unachoona sasa ndicho utakachopata ukioana naye.

Si kweli kwamba huyo mwanaume anampenda Mungu kwa matendo kama ulivyosema na sijajua ulitumie vigezo gani kwani kutembea na wanawake wengine ni uthibitisho kwamba dini yake ni ovyo.

Pia yeye kukupeleka kwa wazazi wake (baada ya wewe kumlazimisha kama uthibitisho kwamba anakupenda) kukutambulisha si jambo kubwa sana ambalo linaweza kumfanya mwanaume mhuni asiwe mhuni bali ni taratibu tu za kuwaambia wazazi kwamba huyu ni mtarajiwa (siyo mke) hii ina maana hata kesho anaweza kuamka na kumtambulisha mwingine.

Pia wazazi wake kuwa wanadini wazuri haina maana mtoto wao naye atakuwa na dini nzuri na kukuhakikishia maisha safi ya ndoa, hata hivyo dini nzuri kwa maana ipi ? kwenda kanisani au kuona wagonjwa au jinsi wanavyoishi?

Ni kweli kama wewe upo makini na dini yako uamuzi wa kuchangua mume ambaye dini zinafanana ni wa busara sana unaweza kusoma hapa

Sasa tuje kujibu maswali yako.
Mwanaume wa aina hiyo huwa harekebiki na Mungu anakupenda sana kwamba amekuondoa kwenye shimo ambalo ungeingia kutoka ingekuwa kazi ya ziada, hivyo furahi na amini kwamba Mungu anaweza yote na shukuru kwa kukuonesha kwamba huyo mwanaume hafai.

Ni ngumu sana kukubali kwamba mwanaume huyo hafai kwani inaonesha ulimkabithi moyo wako wote hata bila kuchunguza vizuri ni wapi moyo wako unaweka.

Suala la kwa nini anakuwa na wasichana wengi naamini yeye ndiye anajua hata hivyo inaonesha kwamba hata kama anakupenda ana tabia mbaya ya uhuni kiasi kwamba hawezi kuwa na wewe tu bila hao wanawake wengine.

Na je anafaa kuwa mume, ukweli ni kwama hafai na kimbia na mwogope (kama njaa) kwa maelezo zaidi kuhusu kujua anafaa au hafai au ni yeye au si yeye wa kuoana naye soma hapa

Usijifariji kwamba eti afadhari ubaki naye yeye ili usionekane unabadilisha wanaume, ukweli huyo hafai na pia kama wewe umezoea kuwa na mwanaume na kumpa mwili wako ni kweli hisia zako zitakuwa zimeumia zaidi, wakati mwingine ukipata mchumba hakikisha humpi mwili wako kwanza hadi ndoa
 
Back
Top Bottom