Mchicha wa Dar

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
Wanajamii,

Nimetokea kuipenda sana Mboga ya mchicha kwani ina faida nyingi sana katika mwili wa mwanadamu.
swali: Haya maji yanayotumika kumwagilia mchicha hapa Dar huwa yanatoka wapi?

Mto msimbazi unajulikana sana kwa kilimo cha mchicha. Je haya maji ya mto Msimbazi chanzo chake ni nini?

wanajamii nisaidieni majibu!
 
Ukimchunguza alacho nyuki ; katu hutaionja Asali!

Vikiletwa mezani vifunike kwa damu ya YESU then kula!
 
hahaha wala usitake kufahamu mchicha unaokula unamwagiliwa na maji gani mama, ukifanya uchunguzi hutakula kabisaa. ushauri tu ni kwamba osha vizuri kabla ya mapishi na mwishowe funika kwa damu ya YESU, AMEN
 
You are there men!
To get the best out of Mchicha. Uwe umekula Nyumbani, Hapo utakua na uhakika kua umeoshwa vizuri.
Hili swali nimeuliza coz jana nimeingia ka mgahawa fulani karibu na Billionaires Club, Nilikula mchicha yaani mchanga Tupu. Nikapata wasix2 kuwa the mchicha was not properly washed. hapo ndo Idea ya Mto msimbazi ikanijia.
Good ukila mchicha wa home men. kwa kina mama nanihii acheni kabisaa tena msiguse.
 
Wanajamii.
Nimetokea kuipenda sana Mboga ya mchicha kwani ina faida nyingi sana katika mwili wa mwanadamu.
swali: Haya maji yanayotumika kumwagilia mchicha hapa Dar huwa yanatoka wapi?
Mto msimbazi unajulikana sana kwa kilimo cha mchicha. Je haya maji ya mto msimbazi chanzo chake ni nini?

wanajamii nisaidieni majibu!
Maji yanayotumika ni machafu sanaaaaa..............lakini kama ulivyokwishaambiwa, ukimchunguza kuku hutamla..........
1. umeshawahi kuona mikate invyotengenezwa bekari...????
2. umeshawahi kushuhudia mama baadhi ya mama ntilie wanavyotengeneza vyakula wanavyoviuza...???
3. umeshaona mbege inavyopikwa...........???
4. umeshawahi kuona packing ya karanga, miwa iliyokatwakatwa, ubuyu, etc jinsi inavyofanyika..................???

ukichunguza kila kitu hutakula kitu duniani...........HUYO MKEO/MUMEO HAKUWA NA 100% YA VIGEZO ULIVYOKUWA UNAVIHITAJI MTU WAKO AWE NAVYO.................. ukichunguza utaishia kutapika tuuuuuuu
 
Maji yanayotumika ni machafu sanaaaaa..............lakini kama ulivyokwishaambiwa, ukimchunguza kuku hutamla..........
1. umeshawahi kuona mikate invyotengenezwa bekari...????
2. umeshawahi kushuhudia mama baadhi ya mama ntilie wanavyotengeneza vyakula wanavyoviuza...???
3. umeshaona mbege inavyopikwa...........???
4. umeshawahi kuona packing ya karanga, miwa iliyokatwakatwa, ubuyu, etc jinsi inavyofanyika..................???

ukichunguza kila kitu hutakula kitu duniani...........HUYO MKEO/MUMEO
HAKUWA NA 100% YA VIGEZO ULIVYOKUWA UNAVIHITAJI MTU WAKO AWE NAVYO.................. ukichunguza utaishia kutapika tuuuuuuu

Kaka uko sawa! Ila hapo kwenye red kule kwetu Tarakea ni shaari kabisa
 
mkienda sokoni au barabarani utakapotamani kula vitu msichunguze vimetoka wapi vimetengenezwa wapi nyie kuleni kwa jina la YESU amen
 
Tatizo sio kuuosha mchicha vizuri. JE zile kemikali zlikzoko ndani ya huo mchicha utaziosha vipi? maji mengine yanatoka viwandani, maji taka nk. Ukiangalia maji ya msimbazi yana rangi nyeusi, kijani na wakati mwingine blue tena yana harufu sana, je kuosha ndiyo suluhisho?
 
Kikahe wacha kuumiza akili yako bure kichwa kitakuuma ukashindwa kutuletea mapoint ya maana hapa!

Unazungumzia contamination Bongo?!

Tukianza list itafika mpaka Tunduma;
 
Mto Msimbazi chanzo chake ni vilima vya Pugu kuleee Kisarawe... Yapo Fresh kabisaa ila kuanzia maeneo ya Pugu mnadani ndipo yanachukua waste zote za Machinjio,viwanda vya Nyerere Rd na Mandela Rd,Vinyesi vya binadamu,Dampo la Vingunguti ndipo yanaingia Bonde la Msimbazi zamani SUKITA hapo ndipo Mboga za jiji letu zinapotokea.
 
mi nashauri mle matembele na kisanvu, mara nyingi hizi zina unafuu. otherwise kama unapenda mchincha na una kaspace hata kidogo home, weka kibustani cha kishkaji panda mchicha, unakula kitu fresh. zaidi funika kwa damu ya Yesu kama walivyosema wadau, maana neno linasema kama ukimwamini na kumtegemea Mungu, hata ujapokula vya kufisha, hutakufa. can somebody say amen?
 
Lakini ukweli uko pale pale. Maji ya msimbazi ni machafu sana. Industrial wastes ndo hatari zaidi. Mdau TUSKER BARIDIII kaelezea hali halisi.
 
Mto msimbazi unajulikana sana kwa kilimo cha mchicha. Je haya maji ya mto msimbazi chanzo chake ni nini?
maji ya chooooni tu hayo...
 
Wanajamii.
Nimetokea kuipenda sana Mboga ya mchicha kwani ina faida nyingi sana katika mwili wa mwanadamu.
swali: Haya maji yanayotumika kumwagilia mchicha hapa Dar huwa yanatoka wapi?
Mto msimbazi unajulikana sana kwa kilimo cha mchicha. Je haya maji ya mto msimbazi chanzo chake ni nini?

wanajamii nisaidieni majibu!

maji mengi ya mito yamechanganyika na kinyesi kwa sehemu kubwa, pia kuna chemicals toka viwandani. Ni tatizo la miji mingi hasa dar ambako kila nyumba inajua yenyewe wapi kuelekeza maji machafu na ya ******. na hasa wakati wa mvua ambapo vyoo vingi vinatobolewa ili maji ya mvua yasafirishe uchafu uende kwenye mito.
lakini uchafu huu ni mbolea safi kwa mboga mboga hizo. na si mchicha tu ni pamoja na mboga nyingine.
cha msingi hapa ni kuwa hizo mboga zitakuwa na bacteria aina mbalimbali hivyo ukizinunua kuna taratibu za kufuata kama kuosha na kuzipika mpaka joto kiasi fulani (around 70 degree C bacteria wafe).
faida ya mboga za majani ni kubwa sana kwa afya zetu, kuliko shida ya kuzi process ili kuondokana na bacteria na amoeba nk.

ukikataa kula mchicha, hayo magonjwa utayapata kwa kula nyama kama ya ngombe na nguruwe wanaokula uchafu huohuo.
 
mi nashauri mle matembele na kisanvu, mara nyingi hizi zina unafuu. otherwise kama unapenda mchincha na una kaspace hata kidogo home, weka kibustani cha kishkaji panda mchicha, unakula kitu fresh. zaidi funika kwa damu ya Yesu kama walivyosema wadau, maana neno linasema kama ukimwamini na kumtegemea Mungu, hata ujapokula vya kufisha, hutakufa. can somebody say amen?
ameeeen,kumbe wa vijiweni tuko wengi,maana wengine tunaambiwa tunaongea km tuko kijiweni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom