Boflo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 4,384
- 4,409
Mchezo wa Kiduku Unavyowadhalilisha Wanaume
Mtoto wa kiume akiwa amevaa kanga akikata mauno katika mashindano ya KIDUKU yaliyohudhuriwa na mamia ya watu Friday, April 23, 2010 12:14 AM
Fainali ya mashindano ya kucheza mtindo wa taarabu unaoitwa KIDUKU ambao vijana wa kiume huvaa nguo za kike na kukata mauno kama wanawake itafanyika mwanzoni mwa mwezi ujao huku shutuma kali zikiwaendea waandaaji wa mashindano hayo kuwa wana malengo ya kuwaharibu watoto wa kiume. Mtindo wa KIDUKU uliobuniwa na mtangazaji mahiri aliyekuwa akitangaza
katika kituo cha televisheni ya Afrika Mashariki EATV, Maimartha wa Jesse umekuwa gumuzo katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na jinsi mchezo huo ulivyo wahusisha vijana wenye umri chini ya miaka 18.
Wengi wa vijana huwa ni watoto wa shule za msingi na sekondari wengine wakitokea tu mitaani kushindana kucheza mchezo wa Kiduku.
Hivi karibuni Maimartha aliandaa shindano la kumtafuta bingwa wa kiduku mwaka 2010 ambalo limewashirikisha vijana toka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Miongoni mwa vikundi vinavyoshiriki ni Vidoleki, Mazombi, Wanaume fasti, Wakali wa kitengo, Wakupoteza, Stavanga na Mazombi.
Katika shindano hilo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya dola 250, mshindi wa pili atapata music system na watatu ataambulia feni. Fainali ya mashindano hayo itafanyika Mei 2 mwaka huu katika ukumbi wa Travertine uliopo magomeni.
Hata hivyo shindano hilo wengi wamelibeza kutokana na kuonekana linawadhalilisha watoto wa kiume hasa hasa wanafunzi ambao huingia kushindana wakiwa wamevalia sare za shule.
Kwa upande mwingine wapenzi wa muziki wa taarab wamekuwa na maoni tofauti kutokana na vijana hao kucheza huku wakiwa wamevalia nguo za akina dada jambo ambalo wengi wanalihisi kuwa linaweza likawa ni njia mojawapo ya kuwapotosha vijana hao kwa kujiingiza katika njia ya uasherati ikiwa ni pamoja na kuwa mashoga.
Mmoja wa wazee aliyehudhuria katika mojawapo ya mashindano haya [Jina Kapuni] alisema kuwa wizara ya utamaduni, burudani na michezo inapaswa kuangalia na kupitia baadhi ya mashindano kama haya.
"Mashindano haya yalipaswa yawahusishe wanawake na si watoto, lingine angalia ndugu mwandishi vijana wanakesha hapa na wanakuja na sare za shule zao inamaana wakitoka hapa wanaunganisha kwenda shule je watasoma nini huku wakiwa na usingizi?", aliuliza mzee huyo.
Wadadisi wa mambo wameomba mchezo wa Kiduku usiwahusishe watoto wa kiume la sivyo vijana hao watakuwa mashoga kwani sehemu kama hizo huhudhuriwa na mashoga ambao wamekuwa wakiwarubuni vijana hao kwa vijisenti vidogo pia sehemu kama hizo ndizo zenya makuadi wa kutafuta vijana wanaotaka kwenda na wakati kwa kufanya mapenzi kinyume na maaumbile yao.
Mei 2 mwaka huu ndio fainali ya kumpata bingwa wa kucheza KIDUKU.