Mchezo mchafu kumchagua DG mpya NHC

Wakati mnaendelea kubishana kwenye episodes za MENGI vs ROSTAM

Nadhani mnajua jamaa wako kwenye process ya kumchagua DG mpya pale NHC lakini cha ajabu waziri husika na kigogo fulani wa IKULU wanatuhumiwa kuwa amekuwa instrumental katika kuvuruga process nzima ili jamaa wa nyumbani kwao apate na wamefika hatua ya kubadilisha hata matangazo ili kumuaccomodate candidate mmoja

Ukistaajabu ya musa utashangaa ya firauni

Na tangazo la pili lilikuwa scaled down hata masharti ya elimu ili jamaa apate tuu

anyway hiyo ndio habari..sasa tegeemni wengine kuja tutetea huu fisadi

Naomba kuchangia machache kwa ufahamu wangu wa mambo ya ajira kwenye vyeo vya CEO.

1. GT anasema vigezo vilishushwa ili kumu-accomodate mtu... mimi nakataa kilichoshushwa lazima itakuwa accademic qualification ambazo kama unahitaji results zaidi hazimati sana... mfano Temu CEO wa Dahaco/Swissport amepata masters juzi juzi tu baada ya kuwa CEO of a performing company for years.

2. Nyinyi mnao-question hizo system ndio umsio-jua corporate world iko vipi?

3. Watu wazuri kwenye soko la ajira hawaombi kazi,,, that is a fact... ndio maana corporate organisation wanavyowatumia recrutment agency... hao recruitment agency ndio wana-poach watu from one company to another.

4. Tutofautishe kuajiri na sheria ya PPRA. kule PPRA lazima ushindanishe walioomba kazi... kwenye ajira ukiona waliomba wote ovyo u find plan B. that what Ikulu did. bravo Ikulu... they will understand baadaye.

5. A good bachelor degree is quite sufficient for many CEO kama wana experience, attitute na behaviour nzuri... CEO sio academicians hauhitaji kuwa na PHD za Washington University... na mara nyingi watu wenye madegree mengi ni watu wa theories... CEO sio mtu wa theory ni mtu wa making things happens.

6. Ndio maana interview za Ma-CEO ni tofauti sana.... wakati mwingine ni kumjua mtu anajua mambo yanayoendelea duniani kwenye corporate world kwa kiasi gani.... sio kupandishana vyeo ati nilikuwa principal economist pale wizara ya mambo ya ndani... bla bla bla... its about what you have done...

6. Naona uvivu naishia hapa... nadhani hamtaelewa hata nisemeje.
 
Naomba kuchangia machache kwa ufahamu wangu wa mambo ya ajira kwenye vyeo vya CEO.

1. GT anasema vigezo vilishushwa ili kumu-accomodate mtu... mimi nakataa kilichoshushwa lazima itakuwa accademic qualification ambazo kama unahitaji results zaidi hazimati sana... mfano Temu CEO wa Dahaco/Swissport amepata masters juzi juzi tu baada ya kuwa CEO of a performing company for years.

2. Nyinyi mnao-question hizo system ndio umsio-jua corporate world iko vipi?

3. Watu wazuri kwenye soko la ajira hawaombi kazi,,, that is a fact... ndio maana corporate organisation wanavyowatumia recrutment agency... hao recruitment agency ndio wana-poach watu from one company to another.

4. Tutofautishe kuajiri na sheria ya PPRA. kule PPRA lazima ushindanishe walioomba kazi... kwenye ajira ukiona waliomba wote ovyo u find plan B. that what Ikulu did. bravo Ikulu... they will understand baadaye.

5. Naona uvivu naishia hapa... nadhani hamtaelewa hata nisemeje.

Yote hayo unayoyasema yanamaanisha kuwa hakuna haja ya kuwa na process. Kama hilo ni kweli kwanini walipoteza muda kwenye process ambayo the outcome had already been predetermined. Sawa sisi hatujui corporate world.. niambie corporate world ya nchi gani ambapo Rais anakuwa na uamuzi wa mwisho wa kumteua mtu ambaye tayari alikuwa anamtaka na wakapoteza muda kufanya head hunting and all the bs just to end up overruled?

Labda wewe ndio hutuelewi au hutaki kuelewa pointi yetu unafikiri ni mjadala unamhusu Mchechu per se.. it is bigger than Nehemiah mkuu.
 
Walifanya hivyo ili wawapumbaze Watanzania labda kwenye kampuni binfsi ambazo Wanasiasa wanakuwa na hisa nazo ila ni vigumu sana katika ulimwengu huu kujua ni vipi imekuwa hivyo. Lakini kingine labda because it is a government ndio maana wanafanya hivyo
 
Yote hayo unayoyasema yanamaanisha kuwa hakuna haja ya kuwa na process. Kama hilo ni kweli kwanini walipoteza muda kwenye process ambayo the outcome had already been predetermined. Sawa sisi hatujui corporate world.. niambie corporate world ya nchi gani ambapo Rais anakuwa na uamuzi wa mwisho wa kumteua mtu ambaye tayari alikuwa anamtaka na wakapoteza muda kufanya head hunting and all the bs just to end up overruled?

Labda wewe ndio hutuelewi au hutaki kuelewa pointi yetu unafikiri ni mjadala unamhusu Mchechu per se.. it is bigger than Nehemiah mkuu.

MM,

  1. Yes, duniani labda ni nchi yetu ambayo inamhusisha Rais kwenye uteuzi. Sina hakika... lakini hata hivyo hata hizo nchi nyingine ni uhakika agency akishamaliza kazi yake anapeleka mapendekezo na majina zaidi ya 1 na huenda pungufu au sawa na matatu kwa mwenye kampuni yake... na sidhani agency ndiye anasema huyu ndiye... tatizo letu ni kwamba agency alitakiwa apeleke kwa board ya kampuni na sio kwa Rais.
  2. Mwenye thread yake amesema vigezo vilishusha mimi nadhani vilipandishwa.. yaani walionyesha kwamba academics zisiwe ndio kigezo tu. na Huenda aomba vigezo vibadilishwe akawa huyo huyo recruitment agency.
  3. Process zenu za uagiri ndio ziliweka maCEO mlio nao... sasa kama jamaa wanabadilika na kuwa na mfumo wenye upana. na kwenye interview inarudi kwenye masters etc... baada ya wote kushikana mashati kwenye vigezo vingine.
Mwisho my points:

Interview ya CEO sio sawa sawa na kulinganisha ma-contractors wa kujenga nyumba as per PPRA procedures. it is quite different game and stories all togther... and the most success CEO have also be those who possess more proffesional qualifications and experience as opposed to academic qualifications.... to me a bachelor degree is the base... the rest ni mauza uza...

Samahani kwa ukali wa post yangu iliyopita. Nawatakia kila la kheri na Mwenyezi Mungu awafunulie hekima wenzenu walizotumia ambazo hawajaziweka wazi hapa. AMEEEn
 
headline_bullet.jpg
Adaiwa kumteua kinyemela Mkurugenzi wa NHC
headline_bullet.jpg
Mchakato wadaiwa kutumia Sh. milioni 82
headline_bullet.jpg
Mwenyewe aziita tuhuma ni za kipuuzi

Chiligati%2818%29.jpg

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati

Mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC), umegharimu Sh. milioni 82, imebainika.
Mchakato huo ambao uliendeshwa na kampuni ya Price WaterHouse Coppers (PWC) ambayo ilikuwa mshauri mwelekezi, kwa takribani miezi mitatu, haukufanyiwa kazi na badala yake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, aliamua kumteua bosi mpya wa NHC kwa kutumia Sheria Na. 2 ya 1990 inayounda shirika hilo, kifungu cha 18 (1).
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa bosi huyo mpya wa NHC, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Nehemia Msechu (37), ameelezwa kutokuwa na sifa za kusimamia shirika hilo. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Msechu (37) ni mmoja kati ya watu waliowania nafasi hiyo wakati ilipotangazwa na kampuni ya PWC, lakini hakuitwa kwenye usaili kutokana na kutokuwa na sifa muhimu za kushika wadhifa huo.
“Pamoja na kwamba Msechu aliomba nafasi hiyo, hakuwa ‘short listed’, kibaya sana, kama serikali ilijua ina mtu wake ambaye ingemteua, kwa nini walitumia Sh. milioni 82 kumlipa mshauri mwelekezi wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu,” kilieleza chanzo chetu.
Chanzo hicho pia kilieleza kuwa iliyokuwa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, ilipitia orodha ya waombaji iliyowasilishwa kwake na kampuni ya PWC na kupendekeza majina matatu ya wakurugenzi wa vitengo ndani ya NHC ambao pia waliomba nafasi hiyo na kuonekana kuwa na sifa, lakini wizara ilipuuza mapendekezo hayo na kuamua kufanya uteuzi.
“Bodi ilifanya hivyo kwa kuamini kuwa watu wenye sifa na uzoefu wa kutosha kuhusu shirika hilo ni wafanyakazi wenyewe, hiyo pia tulidhani ingewapa wafanyakazi motisha ya kufanyakazi kwa bidii,” alisema mjumbe mmoja wa bodi ya NHC iliyomaliza muda wake.
Waziri Chiligati alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema ni maneno ya hovyo na majungu ambayo yatawapotezea Watanzania muda.
“Hilo la hela muulize Katibu Mkuu, maana ndiye anayetoa fedha naamini yeye atakuwa na taarifa zaidi kuliko mimi,” alisema.
Alipoulizwa sababu za kuajiri mshauri mwelekezi wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo wakati sheria inampa nguvu ya kumteua mtu mwenye sifa, alikwepa kujibu na kumwelekeza mwandishi amuulize Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi.
Alieleza kuwa uteuzi wa Mkurugenzi wa NHC, unapitia mikononi mwa watu wengi na kwamba kama angekuwa na kasoro, zingebainika mapema.
“Sikumteua mimi mwenyewe, amepita mikononi mwa watu wengi vikiwemo vyombo vya dola, hivi kama hakuwa na sifa, zisingebainika?” alihoji Chiligati na kuongeza “Hayo ni maneno ya hovyo tu na majungu ambayo tukiyafuatilia yatatupotezea tu muda,”
Shirika hilo kwa sasa linajipanga kujiingiza kwenye biashara ya kujenga nyumba katika mikoa yote na kuziuza kwa mkopo nafuu kwa Watanzania wa kipato cha chini na kati.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Kama president wa nchi ana shahada moja tu, sioni ubaya kwa mtu mwenye shahada mmoja kuwa DG wa NHC. Suala la muhimu kabisa ni kuwa je uwezo anao?. Wengi saaana tunakubali kuwa uwezo huo anao na ameshaonyesha huo uwezo wa kiutendaji.

Hayo mengine ni wivu, kukwama kwa wapambe n.k. Kuna mtu namfahamu alishatangaza mtaani na watu wlikunywa bia kuwa atakuwa DG wa NHC, sas unafikiri huyu mtu anasemaje kuhusu Mchechu?Hii pia ilitokea wakati wa kuteuliwa DG wa TI, watu walimwaga hivyo hivyo.
 
headline_bullet.jpg
Adaiwa kumteua kinyemela Mkurugenzi wa NHC
headline_bullet.jpg
Mchakato wadaiwa kutumia Sh. milioni 82
headline_bullet.jpg
Mwenyewe aziita tuhuma ni za kipuuzi

Chiligati(18).jpg

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati

Mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC), umegharimu Sh. milioni 82, imebainika.
Mchakato huo ambao uliendeshwa na kampuni ya Price WaterHouse Coppers (PWC) ambayo ilikuwa mshauri mwelekezi, kwa takribani miezi mitatu, haukufanyiwa kazi na badala yake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati, aliamua kumteua bosi mpya wa NHC kwa kutumia Sheria Na. 2 ya 1990 inayounda shirika hilo, kifungu cha 18 (1).
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa bosi huyo mpya wa NHC, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Nehemia Msechu (37), ameelezwa kutokuwa na sifa za kusimamia shirika hilo. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Msechu (37) ni mmoja kati ya watu waliowania nafasi hiyo wakati ilipotangazwa na kampuni ya PWC, lakini hakuitwa kwenye usaili kutokana na kutokuwa na sifa muhimu za kushika wadhifa huo.
“Pamoja na kwamba Msechu aliomba nafasi hiyo, hakuwa ‘short listed’, kibaya sana, kama serikali ilijua ina mtu wake ambaye ingemteua, kwa nini walitumia Sh. milioni 82 kumlipa mshauri mwelekezi wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu,” kilieleza chanzo chetu.
Chanzo hicho pia kilieleza kuwa iliyokuwa bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, ilipitia orodha ya waombaji iliyowasilishwa kwake na kampuni ya PWC na kupendekeza majina matatu ya wakurugenzi wa vitengo ndani ya NHC ambao pia waliomba nafasi hiyo na kuonekana kuwa na sifa, lakini wizara ilipuuza mapendekezo hayo na kuamua kufanya uteuzi.
“Bodi ilifanya hivyo kwa kuamini kuwa watu wenye sifa na uzoefu wa kutosha kuhusu shirika hilo ni wafanyakazi wenyewe, hiyo pia tulidhani ingewapa wafanyakazi motisha ya kufanyakazi kwa bidii,” alisema mjumbe mmoja wa bodi ya NHC iliyomaliza muda wake.
Waziri Chiligati alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema ni maneno ya hovyo na majungu ambayo yatawapotezea Watanzania muda.
“Hilo la hela muulize Katibu Mkuu, maana ndiye anayetoa fedha naamini yeye atakuwa na taarifa zaidi kuliko mimi,” alisema.
Alipoulizwa sababu za kuajiri mshauri mwelekezi wa kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo wakati sheria inampa nguvu ya kumteua mtu mwenye sifa, alikwepa kujibu na kumwelekeza mwandishi amuulize Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi.
Alieleza kuwa uteuzi wa Mkurugenzi wa NHC, unapitia mikononi mwa watu wengi na kwamba kama angekuwa na kasoro, zingebainika mapema.
“Sikumteua mimi mwenyewe, amepita mikononi mwa watu wengi vikiwemo vyombo vya dola, hivi kama hakuwa na sifa, zisingebainika?” alihoji Chiligati na kuongeza “Hayo ni maneno ya hovyo tu na majungu ambayo tukiyafuatilia yatatupotezea tu muda,”
Shirika hilo kwa sasa linajipanga kujiingiza kwenye biashara ya kujenga nyumba katika mikoa yote na kuziuza kwa mkopo nafuu kwa Watanzania wa kipato cha chini na kati.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Hivi huyu mkuu Chiligati,anajua madhara ya majibu yake kwa umma kweli?

Mbona hayo ni maswali yaliyo ndani ya uwezo wake tu kuyajibu?

Halafu kwenye hii,habari..Mhh,i guess JF inaweza kuwa kituo/kisima cha dataz kwa waandishi/vyombo vya habari bongo.Tuzidi kuipa JF heshima yake kwa michango ya uhakika na yenye intergrity zaidi
 
Maumivu ya kichwa huanza polepole,
kwani hata richmond na Rada si walikatraa hivihivi kwanza?

lakini hii naona kama itakuwa na tofauti kidogo kwani Chiligati keshaanza kumuua Katibu Mapeeeeeemaaaa
 
-Huyu mkuu Chiligati somo la public relations inawezekana halikuwepo ktk syllabus ya Masters yake ya Public Admin. Yaani,kazi ipo hapa
 
Ila jamaa angeweka wazi kila kitu kwa kutoa ushirikiano na waandishi wa habari.Hajui hilo jambo linaigusa jamii kwa kiasi gani

Hizi mbinu ambazo viongozi(in this case watawala) wanazotumia kukwepa wajibu wa msingi haziwezi kutufikisha mahali pazuri sana au penye usalama.gharama za kupuuza ni kubwa ni kubwa kuliko kutekeleza wajibu
 
Hivi Chiligati kwa nini huwa anajiamini hadi anapitiliza? Kama vili halijalijali.

Halafu jamani, yale yale tunayopigia kelele kila siku. Waandishi wa Tanzania na makosa ya matamshi/ maandishi. Ile kampuni inaitwa Price Waterhouse Coopers wao wameandika Coppers!!

Halafu huyu mkurugenzi mpya jina lake la ukoo ni Mchechu au Msechu?
 
Kama utaratibu unaruhusu Waziri kuwa na last say sioni kwa nini Chiligati alaumiwe kwa kuutumia utaratibu huo badala yake tutake utaratibu ufutwe ama ufanyiwe marekebisho.

Mambo mengi ambayo huwa yanapitishwa na bunge kwa ajili tu ya convinience ya wakati fulani badala ya kuangalia upeo wa muda mrefu matokeo yake ndivyo yanavyoweza kuwa - matumizi mabaya ya taratibu zilizopo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom