Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana uteuzi wa mchezaji bora Duniani katika mabara mbalimbali ila mpka sasa nashindwa kuelewa ni vigezo gani wanavitumia wenzetu wa mabara mengine kwani uteuzi wao ni tofauti kabisa na unaofanywa na bara la Africa CAF.
Ukiangalia orodha ya wachezaji bora katika mabara tofauti South America South American Footballer of the Year - Wikipedia, the free encyclopedia
Europe :Ballon d'Or - Wikipedia, the free encyclopedia Asia : Asian Footballer of the Year - Wikipedia, the free encyclopedia
Ukianza na Brazil Kaka, Ronaldinho, Ronaldo na wengine wengi wote hao wamewahi kuwa wachezaji bora DUNIANI ila hata mara moja hawajawahi kushinda tuzo ya mchezaji bora America ya Kusini, kwanini...?
Sababu ni moja wao na wengine woote isipokuwa Africa, wanathamini mashindano yanayofanywa ndani ya mabara yao na best player anatokana na katika mashindano ya vilabu ndani ya bara lao.
Tukirudi Ulaya wachezaji wote niliowataja hapo juu wa brazil pamoja na waafrika kama George weah wamewahi kuwa wachezaji bora Ulaya ingawa wao sio wazaliwa wa hapo..., Simple because wanacheza katika vilabu vya Ulaya.
Sasa iweje huku kwetu Africa kila mwaka mchezaji bora wa Africa anatoka Ulaya? je wanatumia vigezo gani kumpata huyo mchezaji? mwisho kwa mchezaji aliyekuwa anachezea ndani ya bara la Africa kuwa mchezaji bora ilikuwa mwaka 1985 mchezaji toka Morocco Mohammed Timoumi aliyekuwa akiichezea FAR Rabat ndiye alishinda tuzo hiyo..., je hii ni sawa?
ni sawa kulinganisha wachezaji wanaocheza Champions league, EPL, La Liga na makombe yetu ya vilabu Africa..?,
Je huyu tumuite Mchezaji bora wa Africa au Mchezaji bora Muafrica.., maana kwa utaratibu huu hata kaka akija kucheza Africa hawezi shinda tuzo hii maana inaonekana jambo la kwanza hapa tunaloangalia ni uafrica na sio mchezaji anachezea wapi
Wana Jamii hebu nisaidieni katika hili labda mimi sielewi vizuri